Utajiri halali! Dhana isiyo na chembe ya ukweli

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
361,176
Reaction score
831,950
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..

Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....

Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja
 
Ayubu yule wa kwenye biblia hakuwa na utajiri wa halali? Mshana Jr
Unaujua msoto alioupitia??? kutoka kuwa tajir namba moja duniani mpak kuwa fukara namba moja duniani lakn jamaa kasimamia ukucha kumtegemea Mungu....Tajir gan wa sasa anaweza pitia msukosuko kama huo akabaki upande wa Mungu?? biashara ikiyumba kidog tu anakimbia kwa mganga wake au freemason...
 
Anaweza kutoa kafara ukoo mzima alimradi tu asimame tena
 
Nyakati za Biblia sio nyakati tulizonazo sasa, ndio maana hata baada ya kujaribiwa hakuanguka dhambini

Ila kwenye thread yako umenikumbushia mzee mengi.. Maana nasikia yeye ni muumini wa freemason, sasa kwenye ile misaada anayotoa + party za vilema huenda anachukua nyota za watu na anatoa kafara in the process Mshana Jr
 
Explanation nayo ijua ya huo msemo wa ngamia ni rahisi kupita kwenye tundu la sindano uliko tajiri kuingia kwenye ufalme wa mbinguni ni kwamba mtu mmoja uwezi kuwatumikia mabwana wawili either utambatana huyu na kumwacha huyo.. Pia hapa alimaanisha Tajiri hawezi kushikana na mali pamoja na mungu ivyo atashika kimoja kati ya mungu au mali na mara nyingi matajiri wanashikana na mali kuliko mungu ivyo inapelekea kwenda motoni
Ikiwa utajiri ni tiketi ya kwenda motoni nategemea mfalme selemani atakua akiongoza kwa maana alikua akimiliki karibia nusu ya mali ya dunia
Cha msingi ni kutenda yalio mema na ya kumcha mungu ili siku ya mwisho twende kwake mbinguni
Tuwe matajiri kihalali zio mali za zuluma, tutende yaliyo mema, tushike amri zake TUTAKUTANA MBIGUNI HATA KAMA DUNIANI TULIKUA MATAJIRI
 
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..

Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....

Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja
utajiri wa billgate microsoft owner ni magumashi?

?
 
sikubaliani na wewe
 
Ila kwenye thread yako umenikumbushia mzee mengi.. Maana nasikia yeye ni muumini wa freemason, sasa kwenye ile misaada anayotoa + party za vilema huenda anachukua nyota za watu na anatoa kafara in the process Mshana Jr
You never know..... Ukiwa na hela mingi lazima utafute namna bora kiupande mwingine kuzilinda
 
Utajiri wa haki unaosema haupo una thamani gani naamanisha ni kuanzia kummiliki asset zaidi ya bilion moja au uwe na asset kiasi gani
 
Utajiri una viwango, tajiri wa wilayani si lazima awe tajiri wa mkoani, tajiri wa Tanzania si lazima awe wa Africa... But vyovyote iwavyo yeyote aanzaye kuelekea kwenye utajiri hujisogeza zaidi kwenye mambo yasiyo haki
 
Maneno ya Mungu yanasema hivi.... Ni rahisi kwa ngamia(sio mnyama) kupenya kwenye tundu la sindano kuliko tajiri kuurithi ufalme wa Mungu....!
Warithi wa ufalme wa Mungu ni akina nani? Wana sifa na vigezo gani? Ni wanyofu na wasafi wa moyo, watenda haki waliojitenga na dhambi na matendo yote ya giza, wasiodhulumu wala kupora cha mhitaji...
Ili uweze kuwa tajiri ama ili uweze kuupata utajiri kwa kiasi kikubwa itabidi ujitenge na matendo ya unyofu, huruma, utu wema na ushikamane na ulimwengu wa giza, makafara dhuluma na ni lazima uwe na roho ngumu na katili japo kwa kificho....!
Itabidi utafute njia za kupata bidhaa kwa bei rahisi sana halafu uuze kwa faida kubwa
Itabidi uwe mkwepa kodi na mdanganyifu kwenye mapato kwa nia ya kutunisha kibubu chako
Itabidi ununue hata kuuza mali ya wizi, dhuluma ama magendo ili tu usitetereke kiuchumi
Itabidi waajiriwa wako uwalipe kidogo lakini wazalishe kingi
Itabidi ufanye makafara na ushirikina kwa nia ya kulinda utajiri na himaya yako
Itabidi utumie mbinu zote halali na haramu ili kuendelea kukuza na kutunisha akaunti zako na biashara zako..

Ukishafanikiwa kimaisha na kuwa mfanyabiashara tajiri kwa viwango tofauti, kiunafiki kabisa na kuficha makucha yako, utairudia jamii kwa kutoa sadaka, misaada na zaka kwenye nyumba za ibada na majukwaa ya kijamii.. Hutafanya kwa siri kwakuwa unataka usafishike mbele za macho ya jamiii... Lakini kile unachokoa ni sehemu ndogo kabisa kwenye kile ulichowaibia wale unaowapa kwa mlango wa misaada....

Yote juu ya yote tunauhitaji utajiri kwa nguvu zetu zote ili kukidhi mahitaji ya natamanio ya kimwili na starehe za dunia, sifa na utukufu wa kununua.... Lakini asikudanganye mtu hakuna utajiri wa haki hata siku moja
Hoja yako unataka aminisha jamii kuwa umaskin ni sehemu ya utakatifu,,na mtu kuwa na Mali ni dhambi kwa mtazamo wako duni kwamba Mali au utajiri lazma udhulumu,uibe,unyonye watu nk..
Sio kweli sabb kuna utajiri unaopatikana kwa haki na unaopatikana nje ya haki..pande zote mbili kuna mchakato wake!!

Usitake kuturudisha kwenye wokovu wa kimaskini kama wa enzi zileeeee...afu mnageuka na kutucheka eti mbona wanasema Mungu wao tajiri wakat wao maskini..

Fedha na dhahabu ni Mali ya Bwana..mithali...
 
Utajiri una viwango, tajiri wa wilayani si lazima awe tajiri wa mkoani, tajiri wa Tanzania si lazima awe wa Africa... But vyovyote iwavyo yeyote aanzaye kuelekea kwenye utajiri hujisogeza zaidi kwenye mambo yasiyo haki
Kwamba hakuna kiwango kamili cha kuanzia utajiri.. Kama ni kulingana na mazingira unaweza ukataja hivyo viwango
 
Back
Top Bottom