Utafiti wambeba Magufuli urais 2015

Utafiti wambeba Magufuli urais 2015

rebeccamrema

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2014
Posts
334
Reaction score
196
jembe.jpg

Utafiti waonyesha Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuwa Rais

Na Mwandishi Wetu

WAKATI kesho Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikitarajia kufanya uzinduzi wa kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Taasisi ya Maendeleo, Vijana, Uongozi na Utawala Bora(YDG) imetoa utafiti na kuonyesha mgombea wa nafasi ya Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli anaongoza.

Utafiti huo ulitolewa jana mjini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo, Christopher Maganila, ambaye alisema katika utafiti walioufanya kuwa endapo uchaguzi mkuu ungefanyika leo, Dk Magufuli angeshinda nafasi hiyo.

Alisema matokeo hayo, yanaonyesha Dk. Magufuli angeshinda kwa asilimia 45, huku mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa angekuwa na asilimia 10.5, huku asilimia 35 wakisema hawajaamua mgombea gani anaweza kuwa Rais kwa kuwa ni bado mapema mno.

Matokeo hayo pia yalionyesha kuwa wagombea wengine wangepata asilimia 0.1 hadi 5 huku asilimia 8 wakionekana wakisema hawajui ni mtu gani anafaa kuwa Rais kati ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafasi hiyo.

"Huu ni utafiti huru na umefanikiwa kufika kwenye kila mkoa lakini kwa wilaya moja kwa kuwa tumeamua kuwahi ili kuona mwamko wa wananchi katika kupiga kura na kuchagua mgombea wanayemhitaji,''alisema.

Hata hivyo, Katibu huyo mtendaji alisema sababu nyingi walizoonekana kuzitoa wananchi kuwa Dk. Magufuli atakuwa mtendaji na mtu mwenye upeo mkubwa wa kufanya kazi endapo akipewa ridhaa.

Kwa mujibu wa Katibu huyo, alisema anaamini uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa huru na haki kwa kuwa wananchi wameonekana kuwa na mwamko katika kuchagua kiongozi atakayewaongoza.
 
Mbona hili likowazi tena sana, hata mwaka 2005 uPM ungekwa wa kupigiwa kura Magufuli angemgalagaza EL kwa mbali. Sema ndio hivyo tena wakati ule uPM kigezo kimojawapo kilikuwa ni urafiki wa kutokukutana barabarani.

katika mwaka Lowassa anashindwa kwa aibu ni mwaka huu na mafuriko yake ya kusombwa kwaa hela
 
View attachment 278949

Utafiti waonyesha Magufuli ana uwezo mkubwa wa kuwa Rais Na Mwandishi Wetu WAKATI kesho Chama Cha Mapinduzi(CCM) kikitarajia kufanya uzinduzi wa kampeni zake kwenye viwanja vya Jangwani, jijini Dar es Salaam, Taasisi ya Maendeleo, Vijana, Uongozi na Utawala Bora(YDG) imetoa utafiti na kuonyesha mgombea wa nafasi ya Urais wa CCM, Dk. John Pombe Magufuli anaongoza. Utafiti huo ulitolewa jana mjini Dar es Salaam na Katibu Mtendaji wa taasisi hiyo, Christopher Maganila, ambaye alisema katika utafiti walioufanya kuwa endapo uchaguzi mkuu ungefanyika leo, Dk Magufuli angeshinda nafasi hiyo. Alisema matokeo hayo, yanaonyesha Dk. Magufuli angeshinda kwa asilimia 45, huku mgombea wa CHADEMA Edward Lowassa angekuwa na asilimia 10.5, huku asilimia 35 wakisema hawajaamua mgombea gani anaweza kuwa Rais kwa kuwa ni bado mapema mno. Matokeo hayo pia yalionyesha kuwa wagombea wengine wangepata asilimia 0.1 hadi 5 huku asilimia 8 wakionekana wakisema hawajui ni mtu gani anafaa kuwa Rais kati ya wagombea waliochukua fomu za kuwania nafasi hiyo. “Huu ni utafiti huru na umefanikiwa kufika kwenye kila mkoa lakini kwa wilaya moja kwa kuwa tumeamua kuwahi ili kuona mwamko wa wananchi katika kupiga kura na kuchagua mgombea wanayemhitaji,’’alisema. Hata hivyo, Katibu huyo mtendaji alisema sababu nyingi walizoonekana kuzitoa wananchi kuwa Dk. Magufuli atakuwa mtendaji na mtu mwenye upeo mkubwa wa kufanya kazi endapo akipewa ridhaa. Kwa mujibu wa Katibu huyo, alisema anaamini uchaguzi wa mwaka huu, utakuwa huru na haki kwa kuwa wananchi wameonekana kuwa na mwamko katika kuchagua kiongozi atakayewaongoza.

wamedanganya lowassa ndo raisi
 
Inafurahisha sana kuona wagonjwa mahututi wakipeana moyo namna hii, sio mbaya....
Endeleeni kujifariji.
 
Magufuli, CCM hawana kazi tena, kwishaaaaaa wezi wakubwa hawa.. !!

Lowassa hadi sasa katika MEDIA ZOTEEEE, yuko above 80%.......average za kura za maoni....!!

Magufuli akipata 18% ya total vote ya Urais... ashukuru Mungu..!! CCM hali ni mbayaaaa, mbayaaa sanaaa....!!! kifo lazima... imeharibu nchi hii kila kitu
 
Mbona hili likowazi tena sana, hata mwaka 2005 uPM ungekwa wa kupigiwa kura Magufuli angemgalagaza EL kwa mbali. Sema ndio hivyo tena wakati ule uPM kigezo kimojawapo kilikuwa ni urafiki wa kutokukutana barabarani.

nashangaa watanzania wanasahau magumu aliyotusababishia edo,leo wanaandamana nae mitaani
 
Magufuli, CCM hawana kazi tena, kwishaaaaaa wezi wakubwa hawa.. !!

Lowassa hadi sasa katika MEDIA ZOTEEEE, yuko above 80%.......average za kura za maoni....!!

Magufuli akipata 18% ya total vote ya Urais... ashukuru Mungu..!! CCM hali ni mbayaaaa, mbayaaa sanaaa....!!! kifo lazima... imeharibu nchi hii kila kitu

above asilimia 80 anapata nyumbani kwenu, sio Tanzania hii,we unadhani ufisadi wake anaupeleka wapi
 
Magufuli, CCM hawana kazi tena, kwishaaaaaa wezi wakubwa hawa.. !!

Lowassa hadi sasa katika MEDIA ZOTEEEE, yuko above 80%.......average za kura za maoni....!!

Magufuli akipata 18% ya total vote ya Urais... ashukuru Mungu..!! CCM hali ni mbayaaaa, mbayaaa sanaaa....!!! kifo lazima... imeharibu nchi hii kila kitu

lakini bandiko mbele yetu linaonyesha bwana MAGUFULI ndiye aongozaye, labda tujuze zaidi mkuu kuhusu hayo uyasemayo.
 
Inafurahisha sana kuona wagonjwa mahututi wakipeana moyo namna hii, sio mbaya....
Endeleeni kujifariji.

wagonjwa mahututi mnao ukawa huoni leo alikua anajikoholea bila mpangilio mmfyyuuu
 
Ukawa linda kura..mabadiliko asubuhi na mapema kabisa
 
Back
Top Bottom