Junius
JF-Expert Member
- Mar 11, 2009
- 3,181
- 139
BAADHI ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Zanzibar (CCM) wameshtushwa na ripoti za utafiti zilizotolewa na Kampuni ya Synovate ambayo imempa nafasi kubwa ya uongozi katika uchaguzi mkuu wa 2010 Maalim Seif Sharif Hamad na kufuatiwa na Dk Mohammed Gharib Bilal na kusema kuwa hawakubaliani na utafiti huo.
Kwa mujibu wa utafiti huo uliowajumuisha na kuwahoji wananchi 2000 Tanzania nzima juu ya viongozi waliopo madarakani na wengine wanaotarajiwa kuingia katika kinyanganyiro cha urais katika uchaguzi mkuu ujao imetoa matokeo kwamba kwa upande wa Zanzibar Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad anaongoza katika kinyanganyiro hicho kwa kupata asilimia 28
Pia utafiti huo umempa nafasi ya pili Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) na Waziri Kiongozi Mstaafu, Dk. Mohammed Gharib Bilal kwa kupata asilimia 24 Wakati Waziri Kiongozi wa sasa Shamsi Vuai Nahodha akipata asilimia 10 na Makamu wa Rais Dk. Ali Mohammed Shein akipata asilimia 2.
Wakizungumza nje ya ukumbi wa mkutano wa Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui jana wajumbe hao kwa masharti ya kutotajwa majina yao gazetini wamesema utafiti uliofanywa haukuzingatia vigezo halisi vinavyohitajika na hivyo hawawezi kuuamini.
Wamesema utafiti uliofanywa ni wa uongo fekina hauna sifa ya kuitwa utafiti kwani baadhi ya wasomi hutafuta njia ya kuwafurahisha wagombea jambo ambalo wamesema hawakubaliani na utafiti huo kwa kuwa jambo la uchaguzi linahitaji uwanja mpana wa kisiasa na sio kwenye karatasi katika ilivyofanywa kwa kuulizwa watu wachache kwa vigezo visivyojulikana.
Wamesema kwamba utafiti huo huenda haukuzingatia vigezo sahihi na ndio maana ukawa na upungufu kwani haiwezekani utafiti wa nchi nzima ukafanywa kwa kuwauliza watu 2000 pekee wakati tanzania ina wananchi zaidi ya milioni 30.
Mimi sidhani kama huo utafiti upo sawa kwa sababu kwanza utafiti huo umefanywa wapi, katika mazingira gani na akina nani waliohojiwa maana inawezekana ukenda sehemu moja ukawauliza watu 1,000 kuhusiana na mtu mmoja ambaye ni kwao na ana nafasi kubwa unategemea watu hao wakwambie nini hawamtaki? alihoji Mjumbe huyo wa NEC.
Wajumbe hao wamesema kwamba haiwezekani Chama Cha Wananchi (CUF) kikapewa kuendesha serikali hata kama kitashinda kwa kuwa Zanzibar lazima iendelee serikali ya Mapinduzi na iwapo CUF itapewa kuendesha serikali Mapinduzi yatakufa ambapo lengo la mapinduzi ni kutaendeleza.
Hatutaki kusikia tafiti za kijinga kama hizo hapa eti nini? Seif awe rais wa Zanzibar wapi labda aende kuwa rais wa Pemba huko lakini hapa sisi hatuwezi hata siku moja kumpa nafasi ya kuwa yeye rais kwani wana mapinduzi wapo wapi hata Seif atawale? Hilo haliwezekani kabisa kabisa nenda kaandike hivyo hebu nenda nenda kule alaaa hii ni nchi ya kimapinduzi hakuna mambo ya kura hapa kura ni utaratibu tu lakini nchi hii itaendelea kuongozwa kimapinduzi na sio kwa karatasi
Hata hivyo wajumbe wengi wameoneshwa kukerwa na utafiti huo ambao umempa nafasi ya pili Dk Bilali ambapo Mjumbe mwengine amesema kutokana na vigezo vilivyotumika haoni kama Dk. Bilal anaweza kupewa nafasi kubwa kiasi hicho.
Amesema nafasi aliyopewa Dk Bilali haimsatahikii kutokana na kuwa hana umaarufu mkubwa unaofikiriwa na watu wengi ambapo alisema licha ya kuwa Dk. Bilali ni mjumbe wa NEC na pia aliwahi kuwa waziri kiongozi wa Zanzibar lakini uzoefu wake katika siasa ni mdogo na pia hana jambo kubwa ambalo amelifanya katika Chama Cha Mapinduzi.
Mimi ni maarufu kuliko yeye kwa sababu mimi nimeshawahi kushika nyadhifa mbali mbali katika chama chetu nikianzia chini hadi juu taifa na nimeanza siasa tokea nikiwa mdogo lakini tumuulize yeye anatoka wapi na amefanya nini katika chama? amehoji Mjumbe huyo ambaye yeye pia anatajwa kutaka kuwania nafasi ya urais Zanzibar.
Akizungumza na gazeti hili Mjumbe mwengine wa NEC Zanzibar ambaye ni Waziri wa Serikali ya Muungano amesema utafiti uliofanywa ulikuwa wa kujifurahisha nafsi zao wenye kufnaya tafiti hizo pamoja na wakubwa waliowatuma kufnaya tafiti hizo ambapo haiwezekani utafiti umpe nafasi kubwa Dk. Bilal.
Ahhh mimi hizi tafiti huwa siziamini kwa kikubwa kipi cha kupewa nafasi ya pili huyo Dk. Bilali mimi kwa kweli nadhani huyo Dk. Bilali amewatuma hao wanaojiita wasomi wamfanyie utafiti lakini ni bure tu wewe ngoja huo uchaguzi uje utashangaa kitakachotokea alisema.
Mjumbe huyo amewakumbusha wasomi wenye kufanya tafiti mbali mbali katika mambo ya siasa kuacha kutumia kigezo cha umaarufu kwani suala la umaarufu halina nafasi katika siasa za Tanzania kwa kuwa huko nyuma imeshawahi kutokea mtu asiyekuwa maafuru kushinda na kuchaguliwa kuwa rais kuliko aliyekuwa maarufu.
Ngoja nikwambie unakumbuka mgombea wa urais wa Zanzibar mwaka 2000 alikuwa nani? Unakumbuka kama Dk. Bilali si ndio alikuwa maarufu jee kapata? Na jee nani alitarajia kama Amani Karume atakuwa rais yeye si aliangushwa kwa kura nyingi sasa na watu pia hawakumtaka lakini jee hakuwa rais? Kwa hivyo kigezo cha kuwa maarufu kisitumike kabisa? Alikumbusha Mjumbe huyo ambaye ni waziri katika serikali ya Muungano na anatajwa kuwa na nafasi katika kinyanganyiro cha urais Zanzibar.
Akizungumza na Mwananchi Mwenyekiti wa Vijana wa CCM, Hamad Masauni Yussuf amesema kwanza hajui vigezo gani vilivyotumika katika utafiti huo lakini wananchi wengi bado wana kasumba kwamba Chama Cha Wananchi (CUF) bado kina ngome yake kubwa huko Pemba jambo ambalo amesema kwa sasa ni kinyume.
Amesema sio kweli kwamba CUF wana nafasi kubwa ya kushinda urais kwa Zanzibar na pia huko Pemba hali hivi sasa imebadilika ambapo CUF wana nafasi ndogo sana ya kushinda kwa kuwa wananchi wengi wa kisiawa hicho wamekata tamaa na viongozi wao na chama chao hivyo CCM ina nafasi kubwa ya kushinda katika kisiwa hicho.
Hizi kasumba kuwa labda CUF wana ngome yao kubwa huko Pemba
Nadahani hivi sasa zinapaswa kuachwa kwanza kwa sababu mimi nimetoka hivi karibuni huko Pemba na hali ilivyo sasa sivyo hivyo ilivyo kabisa amesema Masauni.
Masauni hakutaka kuongelea utafiti uliofanywa na Kampuni ya Synovate ambao umempa nafasi ya pili katika kinyanyanyiro cha uchaguzi wa 2010 Dk. Bilali kwa madai kwamba bado hajafanya utafiti katika chama chake kuona nani anafaa katika kinyanganyiro hicho cha urais wa 2010.
Amesema kwamba chama chake hakiwezi kumteuwa mtu asiyekuwa safi
hivyo kwa vyovyote vile lazima mgombea atakayeteuliwa atakuwa na vigezo na sifa zinazokubalika kuwa ni mgombea urais na hakuna sababu ya kuwepo utafiti wa sasa kwani CCM haijawahi kumsimamisha mgombea ambaye sio safi.
Mimi sijafanya research ndani ya CCM kwa sababu najua chama changu hakifanyi makosa sisi tunachagua mgombea safi wakati ukifika mie nipo na kura yangu na nitampa kura mgombea atakayeteuliwa na chama changu kwa mujibu wa vigezo vilivyowekwa na chama changu amesema Masauni.
Hata hivyo amesema amekuwa akifanya na tathimini ya kukipima Chama Cha Wananchi (CUF) na amegundua kwamba kuna udhaifu mkubwa na huenda udhaifu huo ukawakosesha nafasi na uongozi viongozi kadhaa wakiwemo wabunge, wawakilishi na madiwani kwa kuwa CUF haina muelekeo.
Mie sijafanya research katika CCM lakini research yangu nimefanya kwa CUF ni nimeona hawana nafasi katika uchaguzi mkuu ujao amesisitiza Kiongozi huyo wa vijana ambaye anasema CCM ina nafasi kubwa ya kushinda bara na Zanzibar katika ngazi zote za uongozi.
Kwa upande wake Waziri Mmoja wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ambaye anatajwa sana katika kinyanyanyiro cha urais wa 2010 amesema hana sababu ya kujilabu wala kuwatuma watu wamfanyie utafiti kwa kuwa anaamini nafasi ya kuwa mgombea anayo na anatarajia kupata nafasi ya kwanza kuliko aliyoipata Dk. Bilali katika utafiti huo uliofanywa ambapo kimsingi alisema hakubaliani nao.
Mie pia nina nafasi kubwa ya kushinda katika kinyanganyiro cha uraia wa 2010 lakini naona kama ni mambo ya kitoto kufnaywa utafiti hivi sasa kwani tuna haraka ya nini mimi nakwambia chaguzi zetu wewe ngoja utaona maajabu hapa yule mtu aliyekuwa anasemwa ni maarufu basi ataangushwa kichwa chini miguu juu amesema mjumbe huyo.
Aliyekuwa Afisa katika balozi la Tanzania nchini Geneva, Mohammed Yussuf amesema tafiti zinazofanywa katika nchi za Afrika huwa zinatumia vigezo vya nchi za magharibi (Europe) jambo mbalo halileti picha halisi ya nchi za kiafrika kwa kuwa wazungu wanapojiandikisha aktika daftari la kupiga kura tayari huwa wanajulikana watapigia chama gani kitendo ambacho ni tofauti katika nchi za kiafrika.
Wanapofanya hizi tafiti wasitumie vigezo vya Europe kwa sababu kule wenzetu wao wanapofanya registrations wanaweka details zao kabisa na wanajulikana kabisa kwamba fulani atakipigia chama fulani kama ni republican au chama chengine lakini sisi utamjuane kama mtu huyu atyakipigia chama hiki au kile? alihoji.
Kwa upande wa wananchi wengi wamefurahishwa na utafiti uliofanywa na wamesema tafiti kama hizo zinaonesha hali halisi ya ukweli ambapo wananchi wengi wamesema wakizitarajia kufaywa na wasomi lakini kinachosikitisha katika matokeo huwa hayaendani kabisa na tafiti hizo kwa kuwa kuna uibaji wa kura katika chaguzi zinazofanyika nchini.
Tatizo kubwa hapa hizi tafiti zinakwenda sawa sawa na matokeo ya uchaguzi kwa kuwa walitemtaja kashinda ndio huyo kipenzi cha umma unamjua? Ni maalim Seif lakini anayeshinda hapewi hiyo haki yake hapa kuna uporaji wa kura uibaji wa maboxi ya kura na hivi sasa kuna hili la kuwakatalia watu kuwaandika katika daftari hilo pia ni lengo la kuiba kura tu amesema Mmoja wa vijana Ali Hamad Mohammed ambaye alizongewa na vijana wenzake katika eneo la darajani alipokuwa akisoma gazeti la Mwananchi huku umma mkubwa wa vijana ukiwa nyuma yake wakimshangiria, amesema mjumbe mmoja kwa ghadhabu kubwa huku akimsukuma mwandishi wa habari hizi.
SOURCE: Gazeti la Mwananchi

Last edited: