Utafiti Usio rasmi: Watanzania wenye kipato cha Tsh. 20,000 kwa siku hawazidi milioni tano

Ndio maana watu wanatukana matusi kwenye social media, unakuta mtu njaa ni kali moja haikai mbili haikai, familia yake ni 'Mungu na Wanadamu' kifupi hana mbele wala nyuma. Hasira zote zinaishia kwenye matusi na lawama kwa wanasiasa. Hii bongo ni nyoso..


Ndio kawaida ya mtu fukara
 
Halina ubishi hili wala halihitaji Phd ndiomaana tunaitwa nchi masikini, ama nchi ya dunia ya tatu maana yake ni kwamba wengi wa watu wake wanaishi kwa kipato cha chini ya dola moja kwa siku dola moja nikama sh 2300 hivi sasa imagine kuanzia asubuhi , chai, kula mchana ,jioni , maji usafiri e.t.c , ndio mjue kwamba Tanzania ni nchi masikini sana


Alafu ujuaji walionao khaaa
 
Wakuu Kwema!

Kwa watembezi wa mikoa ya Tanzania na wachunguzi huru mtakubaliana na mimi katika utafiti huu usio rasmi.

Utafiti huu nimeufanya kwa miaka minne tangu 2016 mpaka 2020 nikiwa natembelea mikoa mbalimbali ya Tanzania. Mikoa niliyoifanyia utafiti ni mikoa ifuatayo; Dar es salaam, Pwani, Morogoro, Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Mbeya, Shinyanga, Dodoma, Kagera, Mwanza na Kigoma.

Utafiti wangu ulijikita katika mambo makuu yafuatayo;


Utafiti wangu pia ulijikita katika katika makundi yafuatayo ya watu;

i/ Watu wazima wanaume
ii/Watu wazima wanawake

i/ Vijana wa kike
ii/ Vijana wa kiume




Utafiti wangu usio rasmi baada ya kuchunguza nimebaini mambo yafuatayo

i/ Watu wazima wenye umri kuanzia miaka 45 mpaka wazee kabisa zaidi ya asilimia 90% hawajawahi kushika milioni tano kwa pamoja kama zao. Joka jeusi katika kufukunyua nikabaini kuwa walioshika pesa hizo 5M+ Wengi waao walikuwa wafanyakazi ambao pesa hizo wamezipata kwenye mafao baada ya kustaafu. Tena wafanyakazi wa serikalini na kwenye mashirika binafsi yanayolipa mishahara inayoanzia laki nne. Wengine waliopata pesaa hizo ni waliokuwa wafanyabiashara, wakulima na wafugaji. Lakini ajabu ni kuwa watu wazima wengi zaidi ya 90% hawaajawahi kushika milioni tano kwa pamoja. Utafiti wangu unaonyesha kuwa kuwa kwenye wazee/watu wazima(umri 45+) kumi, tisa hawajawahi kushika milion tano kwa pamoja. Hata hivyo wapo wachache walioshika pesa hizo kwa kuuza mali za urithi kama vile nyumba, mashamba au magari ambao wapo kwenye hizo asilimia 10% zilizobakia.

ii/ Utafiti wangu unaonyesha kuwa watu wazima wanawake wenye umri kuanzia 45 - 100, zaidi ya asilimia 95% hawajawahi kushika milioni tano za kwao kwa pamoja . Wengi walioshika ni wafanyakazi baada ya kupewa mafao yao ya kustaafu, walioachiwa mirathi baada ya waume zao kufariki waliokuwa wakifanya kazi zenye maslahi kuanzia laki tano. Waliouza nyumba, wafanyabiashara, wakulima na wafugaji.

iii/ Utafiti wangu unaonyesha watu wazima wenye miaka kuanzia 45 -100 asilimia 90% walijenga makazi yao(wengi huita nyumba lakini sio nyumba bali vibanda) kwa zaidi ya miaka kumi, yaani kidogo kidogo kwa kuunga unga. Nimegundua kuwa kundi hilo lilianza ujenzi wa makazi yao wakiwa na umri wa miaka thelasini mpaka miaka 50. Na wengi makazi yao hawakumaliza wao bali walipewa msaada na watoto wao. Asilimia 10% iliyosalia ndio walijenga nyumba zao ndani ya muda mchache usiozidi miaka miwili mpaka kukamilika. Kundi hili ni tabaka la juu, wafanyabiashara, wafugaji, watu wa madini, viongozi wa serikali na watumishi wa Umma kwenye kada zinazolipa vizuri. Aidha wazee wachache walijenga baada ya kufanya dili haramu kama kuuza madawa ya kulevya, na shughuli zingine haramu.

iv/ Utafiti wangu unaonyesha kuwa zaidi ya 70% ya wanaume wenye umri wa miaka 45-100 walizaa na zaidi ya mwanamke mmoja. Yaani kwenye wanaume kumi, basi wanaume saba walizaa na mwanamke zaidi ya mmoja. Wakati upande wa wanawake zaidi ya 50% wenye umri kati ya 45 -100 wamezaa na wanaume zaidi ya mmoja. Kumaanisha kwenye wanawake kumi basi watano wamezaa na wanaume zaidi ya mmoja. Idadi ya wanawake waliozaa na mwanaume zaidi ya mmoja imezidishwa na wanawake waliozaliwa miaka ya 1960- 1979. Wanawake waliozaliwa chini ya 1960 yaani 1959 kurudi nyuma wengi walizaa na mwanaume mmoja kwa kulingana na utafiti wangu

v/ Utafiti wangu unaonyesha, vijana wenye umri kati ya 25 - 44 zaidi ya 90% hawajawahi kushika milioni 3 kwa pamoja au hata kwa kuzikusanya kidogo kidogo. Vijana wengi huishia kupata chini ya milioni moja kwa pamoja. Kwenye vijana kumi basi vijana tisa hawajawahi kushika milioni tatu kwa pamoja au kwa kukusanya kidogo kidogo. Vijana wachache yaani 10% ndio waliowahi kushika pesa hiyo kwa pamoja, hawa wengi ni wafanyakazi waliochukua mkopo, wafanyabiashara, na vijana wakulima na wafugaji wanaouza kwa mkupuo bidhaa zao. Vijana wachache waliopo kwenye hiyo 10% wamewahi kushika hiyo milion tatu kwa shughuli za vipaji vyao kama muziki, uchoraji, Ushehereshaji wa shughuli na wachache waliozaliwa kwenye familia tajiri au waliopokea urithi kwa wazazi wao.

vi/ Utafiti wangu unaonyesha kuwa vijana wa umri 25 - 44 asilimi 90% hawana sifa ya kukopeshwa na Mabenki milioni tatu kuendelea, wengi wana sifa za kukopeshwa chini ya milioni moja na bado kulipa inakuwa ni kwa mbinde.

vii/ Utafiti wangu umebaini, vijana wengi (umri 25 -44) zaidi ya asilimi 90% waliopanga vyumba hulipa chini ya elfu 40 kwa mwezi na kodi hutoa kwa miezi mitatu mitatu. Mikoa ya nje ya Dar es salaam hulipa kodi tsh 25,000 -30,000 kwa mwezi ndani ya miezi mitatu. 10% ya vijana waliosalia ndio hulipa kodi kuanzia tsh 50,000 kuendelea, na hawa wengi hawa wengi wao ni wafanyakazi na wafanyabiashara.

viii/ Utafiti wangu umebaini kuwa zaidi ya asilimia 90% ya vijana wa umri 25 - 44 vitu vyao vya ndani kama kitanda, godoro, friji n.k havina thamani inayofikia milioni tatu. Ukiingia kwenye makazi ya vijana wengi, ukithaminisha vitu vyao vya ndani havifiki thamani ya milioni tatu. Hata hivyo vijana wengi huchukua bidhaa za mtumba kwa bei rahisi zaidi kwa mfano Tv ya laki tano dukani, kijana atainunua iliyotumika kwa mtu kwa shilingi laki tatu au laki mbili na tisini. 10% Iliyobaki ni ya vijana wenye vitu vinavyozidi thamani ya milioni tatu na wengi wao ni wafanyakazi na wachache sana wafanyabiashara.

ix/ Utafiti wangu umebaini kuwa, vijana wengi zaidi ya 90% kama akifanya kosa akapelekwa mahakamani, kisha akapewa adhabu alipe faini ya milioni mbili au kifungo cha mwaka mmoja. Basi vijana wengi watashindwa kulipa faini hiyo na watafungwa hata ndugu wote wakisema wachange bado haitafika milioni mbili.

x/ Utafiti wangu umebaini kuwa, asilimia 90% ya vijana waliolipa mahari wamelipa chini ya milioni moja. Na hii ni ishara ya kuwa na kipato duni. Wengine wameshindwa kabisa kulipa hata hiyo mahari.

xi/ Utafiti wangu umeonyesha kuwa, hapa Tanzania watu wanaoingiza kwa siku kipato cha shilingi elfu ishirini kwa siku, sawa na laki sita kwa mwezi hawafiki milioni tano.

xii/ Utafiti wangu unaonyesha kuwa, kwa hapa Tanzania zaidi ya 90% ya vijana hukaa sehemu moja(mkoa mmoja) kwa zaidi ya miaka miwili kwa kukosa nauli na pesa ya kutalii sehemu zingine za Tanzania au dunia. Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu kuanzia miaka mitatu pia ni dalili ya umasikini. Mtu wa kipato cha kati au cha juu hawezi kukaa hata mwaka mmoja bila kutoka mkoa au nchi nyingine kwenda kutembea kwa biashara/kikazi au kustarehe.

xiii/ Utafiti wangu umebaini kuwa, zaid ya 90% ya vijana huona kuwa na Gari au simu nzuri ni moja ufahari na maendeleo makubwa jambo ambalo sio kweli, kwani gari na simu ni basic need kwa zama hizi kama chakula na nguo. Jambo hili bado linaonyesha vijana wengi wa kitanzania bado ni masikini.

xiv/ Utafiti wangu umeonyesha kuwa zaidi ya 90% huweza kukaa wiki nzima bila kuingiza hata vocha ya mia tano kwenye simu. Wengi hujiunga vifurushi vya sms vya mwezi na wengi hutumia Facebook ya free mode.

xv/ Utafiti wangu umebaini kuwa, zaidi ya 90% ya vijana wakiume wanajozi moja ya viatu ambavyo huweza kuvitumia kwa zaidi ya miaka miwili. Kidogo vijana wa kike wanajitahidi. Sio ajabu vijana wa kike kuona wakipagawa na vijana watanashati wanaobadilisha viatu, nguo na mafuta. Mtu hupagawa na kile asichokuwa nacho, ni dalili ya umasikini. Kama vijana wengi wangekuwa wanapesa za kubalisha viatu na nguo basi jambo hilo lisingekuwa agenda kwa wanawake.

xvi/ Utafiti wangu unaonyesha, zaidi ya 90% ya watanzania wanaogea sabuni za kufulia na kuoshea vyombo, huku wachache 10% wakiogea sabuni za kuogea. Pia utafiti wangu umebaini kuwa zaidi ya 90% hawatumii marashi, manukato au mafuta mazuri. Wengi hutumia mafuta yenye bei chini ya Tsh5000.

Naomba kuwasilisha, mwenye kunipinga anipinge kwa hoja.

Jokajeusi
Huu utafiti tukiuwekea research proposal yaani ni utafiti ambao kwa mwaka huu wote hakuna mtaaluma yeyote aliyefanya utafiti muhimu na mzito kama huu. Hata hawa waliopata PhD hakuna anaifika hapa. Hongera sana mkuu. Boresha huu utafiti ili uuchapishe rasmi kwasababu kwanza unajua kuandika research vizuri sana pili problem yako ni halisi
 
Huu utafiti tukiuwekea research proposal yaani ni utafiti ambao kwa mwaka huu wote hakuna mtaaluma yeyote aliyefanya utafiti muhimu na mzito kama huu. Hata hawa waliopata PhD hakuna anaifika hapa. Hongera sana mkuu. Boresha huu utafiti ili uuchapishe rasmi kwasababu kwanza unajua kuandika research vizuri sana pili problem yako ni halisi


Ngoja ntafute pesa Mkuu
 
Tufanye umeshinda mkuu


Hapana Mkuu hatushindani.

Ila najaribu Kueleza kuwa katika hili nimechunguza Kwa muda mrefu zaidi ya miaka minne hivyo kunishinda katika hili sio rahisi.

Labda mengine nipo tayari kusalimu amri😀😀😀
 
Hapana Mkuu hatushindani.

Ila najaribu Kueleza kuwa katika hili nimechunguza Kwa muda mrefu zaidi ya miaka minne hivyo kunishinda katika hili sio rahisi.

Labda mengine nipo tayari kusalimu amri
Wewe unachunguza lakini mimi ni idara yangu.
Hao unaowataja ndio mikono yangu.
So nina taarifa zao karibu mikoa yote...
Nasema mikoa sababu wanalipwa kutokana na mkoa au uwezo katika ubora wa kazi.
 
Mkuu umeandika vyema sana, wewe ni muandaaji na mwandishi mzuri wa tafiti, Umeitendea haki taaluma yako na nchi yako.

Nadhani kuna swali muhimu sana hapa
"Tufanyeje tutoke hapo kwenye ufukara huu uliotukuka?"

Tukianza na mtoa mada
Unapendekeza nini kifanyike?

Sent from my SM-M115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom