Utafiti: Simu zinachangia umaskini na migogoro katika mahusiano

Utafiti: Simu zinachangia umaskini na migogoro katika mahusiano

Dotto Mnzava

R I P
Joined
Mar 6, 2014
Posts
864
Reaction score
427
Wataalamu wa Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania na Chuo Kikuu cha vijana cha Bringman nchini Marekani wamebaini kuwa matumizi ya simu ni chanzo cha kutofurahia maisha na kuongeza msongo.

Utafiti uliofanywa na wataalamu hao chini ya usimamizi wa Brandon McDaniel,Mkufunzi kutoka Chuo Kikuu cha Pennsylvania,ulibainisha kuwa watu wengi wanaongeza umaskini wa kujitakia kwa kutumia muda mwingi kwenye simu.

Wanazungumzia maisha ya watu, mafanikio yao, kushindwa kwao badala ya kuangalia vitu vitakavyowaingia fedha zaidi, inaeleza sehemu ya utafiti huo.

Utafiti huo ulibainisha kuwa mbali na umaskini wa kujitakia,matumizi ya simu kupita kiasi huchangia kwa asilimia 75 ndoa kuvunjika pia hatari ya kupata msongo wa mawazo.

Utafiti huo uliohusisha watu wazima 867 wenye umri wa miaka 30 hadi 45,ulibainisha kuwa kama wasingekuwa na simu,robo tatu ya watu hao wangekuwa wamefanya mambo mengi kuboresha maisha yao ikiwemo utendaji bora wa kazi.

Majibu ya utafiti huo yalionesha kuwa wanandoa wengi wangepata muda wa kujadili namna ya kumaliza tofauti zao,kufikia mafanikio,kutimiza malengo hata kuboresha penzi kama wasingetumia simu.

Takwimu za Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania (TCRA) zinaonesha kuwa mwaka 2014 kulikuwa na laini za simu za mkononi zipatazo 31,862,656,ikilinganishwa na laini 2,963,737 mwaka 2005,watumiaji wa intaneti wameongezeka hadi kufikia 11,000,000 Desemba mwaka 2014 kutoka 3,563 waliokuwepo mwaka 2008.
 
Wala hakuna ubishi hapo. Just imagine FB, JF(na forums zingine), WHATSAPP(including all groups), TWITTER, Email addresses, bado sports sites kwa wao wapenzi wa sports, celebrities' forums kwa wapenzi wake,....and the list goes on and on....na mtu yupo busy 24/7. Kweli teknolojia inatuharibu na kuleta umaskini.
 
aisee huu utafiti ni kweli kabisa
inatokea watu wanakosa hata muda wa kusali wao ni mitandao tu
hata akiwa nyumba ya ibada utaona pembeni ana tablets, pads anafungua na
kushare vitu mbalimbali wala hayuko ndani ya ibada yaani simu izimeharibu kabisa watu

Na kwenye ndoa ndo kabisa watu hawako bize kujadiliana mambo ya msingi wala
wanandoa hawako karibu kuleta maushauriano ya mstakabali wa ndoa yao wao
wako bize kuchat mpaka masaa saba mfano upo ni jana tu nilikuwa nachat na
mmojawapo wa wanandoa mpaka usiku kenda yaani mpaka nikashangaa anapata
muda kweli wa kukaa na mwenizi wake na kuongea jamani simu ni kiboko ya
uduni na umaskini kwa watu na hasa sisi WAAFRIKA
 
Umesema kweli tupu. Na wanandoa ndio kundi la kwanza kuathirika, badala ya kutenga mda na familia zetu sisi ni kuchat plus magroup yasiyoisha kila siku. Tunasahau majukumu yetu na wenza wetu.
 
aisee huu utafiti ni kweli kabisa
inatokea watu wanakosa hata muda wa kusali wao ni mitandao tu
hata akiwa nyumba ya ibada utaona pembeni ana tablets, pads anafungua na
kushare vitu mbalimbali wala hayuko ndani ya ibada yaani simu izimeharibu kabisa watu

Na kwenye ndoa ndo kabisa watu hawako bize kujadiliana mambo ya msingi wala
wanandoa hawako karibu kuleta maushauriano ya mstakabali wa ndoa yao wao
wako bize kuchat mpaka masaa saba mfano upo ni jana tu nilikuwa nachat na
mmojawapo wa wanandoa mpaka usiku kenda yaani mpaka nikashangaa anapata
muda kweli wa kukaa na mwenizi wake na kuongea jamani simu ni kiboko ya
uduni na umaskini kwa watu na hasa sisi WAAFRIKA

Dear I agree with you ...Its very sad .Na tusipokuwa really serious this will effect even our next generation.. People are getting divorces because of the electronics and websites, etc. God help us .. My people are destroyed for the lack of knowledge ..Thanks..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom