MSEZA MKULU
JF-Expert Member
- Jul 22, 2011
- 3,763
- 5,605

Picha hapo juu inaonyesha Sehemu za Ubongo zinazokuwa active mtu akipewa changamoto za kisiasa.

Watafiti wametoa Matokeo yao Kuhusu Jinsi ambavyo Ubongo wa Mtu aliyejikita kwenye siasa, Hii inajumuisha Taarifa za MPYA kisiasa, Habari FAKE au Za Uhakika za kisiasa, Mambo ya uchaguzi n.k. Kwa utafiti huu umeonyesha Imani za Kisiasa ni Sawa na Imani za kidini.
HIVI NI BAADHI YA VITU VILIVYOGUNDULIKA
1:Imani ya Siasa ya Mtu inapotiwa changamoto, Eneo la Ubongo wake linalokuwa ACTIVE ni lile linalohusika na Utambulisho wa mtu (Personal identity) na lile linalohusiha msisimko wa mtu kukabiliana na vitisho (Emotional responses to threat).
2:Imeonyesha ni Rahisi mtu kubadili msimamo wa kitu kisicho cha kisiasa kuliko Cha kisiasa kama vile kinachohusu chama hata akipewa Ushahidi.
Watu waliofanyiwa utafiti walikuwa tayari kukubali kuwa ALBERT EINSTEIN Hakuwa mwanasayansi Mkubwa alipopewa Ushahidi kuliko Kubadili misimamo yao ya Kisiasa hata walipopewa Ushahidi.
Source:Which brain networks respond when someone sticks to a belief?