Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba

Discussion in 'JF Doctor' started by Saint Ivuga, Feb 8, 2012.

 1. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]Utafiti: Nusu ya wanaume nchini wagumba[/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"] Send to a friend[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]Tuesday, 07 February 2012 20:53[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]
  0digg
  [​IMG]Florence Majani
  UTAFTI mpya umebaini kuwa nusu ya wanaume nchini ni wagumba ukipingana madai ya wengi kuwa tatizo hilo linawaathiri zaidi wanawake.Kwa mujibu wa utafiti huo, uliofanywa na Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili kati ya mwaka 2009 na Septemba 2010 unaonyesha, asilimia 47.05 ya wanaume wanaokwenda kupima afya zao za uzazi, hawana uwezo wa kutungisha mimba.Malengo ya utafiti huo uliosimamiwa na Dk Henry Mwakyoma, yalikuwa ni kubaini ni kwa kiasi gani wanaume huweza kuathiriwa katika via vyao vya uzazi na hatimaye kushindwa kutungisha mimba.

  Utafiti huo ulionyesha kati ya wanaume 221 waliopimwa, asilimia 30.03 walikuwa na mbegu dhaifu na asilimia 17.02 walikuwa hawana kabisa mbegu zenye uwezo wa kutungisha mimba, zaidi ya maji tu.
  Akizungumza katika mahojiano maalumu na Mwananchi, Dk Mwakyoma alisema, ugumba kwa wanaume limekuwa tatizo sugu katika miaka ya hivi karibuni.

  "Nasisitiza kuwa, pengine mwanaume aliwahi kupata watoto hapo awali, lakini sasa hivi hapati, bado atakuwa mgumba," alisema Dk Mwakyoma.Alisema hapo awali ilikuwa vigumu kupata idadi kamili ya wanaume wenye ugumba kwa sababu walikuwa hawajitokezi kupima."Angalau sasa hivi wanakuja na tunawapima, ingawa ni kazi ngumu kuwapa majibu yao," alisema Mwakyoma.

  Sababu za ugumba
  Mwakyoma alitaja sababu za ugumba kwa wanaume kuwa ni uambukizo katika tezi inayozalisha manii.
  Alitaja sababu nyingine kuwa ni kemikali zinazoingia katika miili yetu, mionzi na wakati mwingine ajali inapoathiri tezi hiyo.

  Dk Mwakyoma aliongeza kuwa, wanaoathirika zaidi ni wanaofanya kazi migodini, jeshini au wanaozungukwa na kemikali kwa muda mrefu."Sababu nyingine ni joto kuzidi katika sehemu za siri za mwanaume, kubeba laptop, unene kupita kiasi na mazingira," alisema.

  Dk Mwakyoma akifafanua jinsi kitengo chake kinavyopima manii ili kujua kama zina matatizo au zipo salama, alisema, " rangi ya mbegu pamoja na umbile huangaliwa ili kutambua ubora wake. Hata kwa kuziangalia tu, mbegu zenye rangi aidha kijivu au nyeupe si salama."

  Kwa upande wake, Dk Innocent Mosha, ambaye ni daktari wa uchunguzi wa magonjwa katika Hospitali ya Muhimbili alisema, wamefanikiwa kupata takwimu hizo kutokana na wanandoa wengi kufika hospitalini hapo kwa ajili ya kujua sababu ya kutokuwa na watoto katika ndoa yao."Mara nyingi matokeo huonyesha tatizo liko kwa mwanaume. Lakini kuna tabu ya kuwaeleza ukweli, wengi hawataki kukubali," alisema Dk Mosha.

  Aliongeza, "Kesi kama hizo huleta migogoro ya kifamilia, kwani huenda mwanamke huyo amekwishamzalia mumewe watoto ambao kimantiki si wa kwake," alisema Dk Mosha.

  Dk Mosha alisema, kuna ugumba wa aina mbili; wa kuzawa nao na ugumba unaopatikana ukubwani.
  "Wapo wanaozaliwa na ugumba, yaani mbegu zao aidha ni dhaifu au hawana kabisa mbegu tangu kuzaliwa kwao," alisema Dk Mosha.

  Shirika la Afya duniani (WHO) linathibitisha kuwa, ujazo wa manii anaopaswa kuwa nao mwanaume ili aweze kutungisha mimba ni milligram moja na nusu hadi nne na nusu na kuongeza, "Ujazo wa manii ukipungua au ukizidi basi mbegu hizo zina matatizo" alisema Dk Mwakyoma.

  Naye Dk Joshua Noreh wa kituo cha upandikizaji cha jijini Nairobi (IVF centre) alisema, tatizo la ugumba alianza kuliona tangu mwaka 2006 baada ya kupokea wanandoa wengi kutoka Afrika Mashariki ikiwemo Tanzania waliofika kutafuta huduma ya upandikizaji wa mbegu ili kupata watoto.

  Utafiti uliofanywa na WHO mwaka 2009 duniani, ulibainisha kuwa, mwanaume mmoja kati ya saba wanaofika kupima afya ya uzazi hugundulika na matatizo ya ugumba.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 2. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Nadhani ni vyema kwa wanaume kwenda kupima maana mara nyingi hawakubaliani na tatizo!
   
 3. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  wakapime tu
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,103
  Likes Received: 22,142
  Trophy Points: 280
  Kwa takwimu hizo itakuwa ni wengi wanao bambikiwa.
   
 5. Tosha

  Tosha Member

  #5
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  kweli hilo ni tatizo kubwa sana na watu wengi katika jamii yetu hawana elimu juu ya UGUMBA,wengi wanafikiri mwanamke siku zote ndio tatizo na pengine wengi wanshindwa kutofautisha uwezo na ubora wa mbegu za kiume na uwezo kujamiiana,utakuta mtu anadhani km anweza kufika zaidi ya mara moja basi ana nguvu za kiume na hivyo an uwzo wa kuababisha mimba kumbe ubora wa mbegu zake ni hafifu au muuondo wa mbegu una kasoro au hata idadi ya mbegu ni chache hazikidhi viwango akiwa

  hili ni tatizo kubwa sana,ndoa nyingi zinasambaratishwa hasa na ndugu wakimtumuu mwanamke ooh hakuzalii huyo,kazi ni kujaza choo tu!maskini kumbe wakati mwingine tatizo ni mwanaume!

  Kutoka na uelewa finyu ni wanaume wachache sana wanakubali kufanyiwa sperm analysis!
   
 6. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,322
  Likes Received: 19,494
  Trophy Points: 280
  sitaki kuamini hizi takwimu..laazima kuna tatizo hizi chanjo hizi watu walizopigwa sijui ndui zina kitu ..wazungu wana roho mbaya sana kama hamwajui
   
 7. Tosha

  Tosha Member

  #7
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 18, 2011
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  mimi nakubaliana na utafiti isipokuwa naona hiyo title ndio inakasoro lakini cha msingi ni kubwa tatizo lipo na linakuwa kwa kasi ndicho nacho pata katika utafiti na siyo nusu ya wanaume ni wagumba ila tatizo lipo na linakuwa so watch out!take care! watu waamuke hasa wanandoa maan baada ya mwaka mmoja wa ndoa huku ndoa inakuwa consumed the hakuna mtoto ni vyema taratibu za mazungumzo ya wanandoa yafanyike na wakubaliane kupima haijarishi nani naanza lakini lengo liwe ni kutafuta suluhisho na sio kumsaka nani mchawi
   
 8. Michael Paul

  Michael Paul Verified User

  #8
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
 9. Michael Paul

  Michael Paul Verified User

  #9
  Feb 8, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 379
  Likes Received: 237
  Trophy Points: 60
 10. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2012
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Hii inatisha
   
 11. SOBY

  SOBY JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2012
  Joined: Sep 19, 2011
  Messages: 1,265
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Uzuri ni kwamba bao moja linaweza kuzalisha watoto milioni moja. Kwa hiyo tusaidiane.
   
 12. measkron

  measkron JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 3,713
  Likes Received: 365
  Trophy Points: 180
  Inawezekana kabisa FF hata ukikumbuka wakati Dr Mwakyusa akiwa Waziri Wa Afya walipokuwa wanazungumzia bungeni kuhusu vina Saba, DNA pia alisema Tanzania 60% ya wanaume wanatunza watoto
  wasio wao
   
Loading...