UTAFITI: 'Message' ni adui wa Elimu pia... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UTAFITI: 'Message' ni adui wa Elimu pia...

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by VUTA-NKUVUTE, Oct 5, 2012.

 1. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #1
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ni utafiti wangu binafsi.Hapa ni sehemu ya kwanza kuuwakilisha.Ni hivi:ujumbe mfupi wa maneno wa simu za viganjani almaarufu kama 'sms' kwa kiasi kikubwa unachangia kudumaza elimu Tanzania. Hii ni kwasababu,wanafunzi wa Shule na Vyuo ambao hutumia simu za vikanjani kwa kutuma ujumbe,hulemazwa na uandishi wa kifupikifupi katika ujumbe na kujikuta wakiandika kifupi hata kwenye mitihani yao.

  Katika utafiti huu,nilifanya mahojiano na maafisa mbalimbali wa Baraza la Taifa la Mitihani,Walimu na Wahadhiri pamoja na Wanafunzi wenyewe. Hoja ya msingi ni juu ya jinsi majibu ya mitihani yanavyoathiriwa na uandishi wa sms. Wengi wa Maafisa,Walimu na Wahadhiri wamekiri kuwepo na kukua kwa tatizo hilo na kudai kuwa majibu ya wanafunzi na wanavyuo hayaeleweki kwa kuwa yanaandikwa 'kihuni'. Wakatoa mfano wa sentensi kama 'Tanzania is a democratic country' ambapo wanafunzi huandika 'Tz z a dmcrtic cntry'.

  Wanafunzi nao wamekiri kwa wingi wao kuwa sms hulemaza na kuwaharibia majibu katika mitihani waifanyayo. Wanafunzi hao wakawaasa wenzao na wengine kujenga utaratibu wa kuandika kwa kirefu sms zao ili wasije kulemaa katika uandishi hata wa mambo muhimu ya kimtihani.

  Katika utafiti huo,nimewahoji Maafisa 11,Walimu 20,Wahadhiri 20 na Wanafunzi wa Shule na Vyuo 45. Niliuanza 2011 na kuukamilisha 2012. Nitauweka katika mtindo wa ripoti hivi karibuni. Asanteni Wakuu...
   
 2. Root

  Root JF-Expert Member

  #2
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,136
  Likes Received: 12,844
  Trophy Points: 280
  Hahhaa binafsi huwa naandika kwa urefu

  Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
   
 3. Nazjaz

  Nazjaz JF-Expert Member

  #3
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 5,345
  Likes Received: 1,131
  Trophy Points: 280
  hao wanafunzi ndio waleeeeeeeeee...... Walio maliza darasa wakiwa hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu
   
 4. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #4
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Huyo Mwanafunzi atakayejibu kifupi kwenye mtihani basi atakuwa zumburkuku na anajitakia mwenyewe kufeli
   
 5. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #5
  Oct 5, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,507
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  Hilo ni tatizo kweli,huwa uandishi wa namna ile unanikera sana
   
 6. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #6
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  yani ni ukweli ulio uchi!yani namaanisha a naked truth!tuulizeni sie.
   
 7. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #7
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Tena nilisahau kukuuliza.Kwani wewe mwalimu? Najua Mwalimu humu JF ni gfsowin...
   
 8. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #8
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,174
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  mimi pia ni mwalimu mkuu!
   
 9. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #9
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Usengwile!
   
 10. Ziltan

  Ziltan JF-Expert Member

  #10
  Oct 5, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 1,345
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  Ngoja nisubiri hiyo ripoti yako ya utafiti ndio ntapata pa kuanza kuchangia
   
 11. waza_makubwa

  waza_makubwa Senior Member

  #11
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  hlo tatzo la walimu. Kam tulikuwa tunafundishwa usiandke kfup cha katika 'ktk' sembuse madudu ya kujitungia ya is 'z'. Namuunga mkono mdau hapo juu.
   
 12. b

  bdo JF-Expert Member

  #12
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,711
  Likes Received: 1,611
  Trophy Points: 280
  Ni adui mkubwa sana katika elimu, maana kushindwa mitihani ni sawa na umbali wa nusu nukta
   
 13. waza_makubwa

  waza_makubwa Senior Member

  #13
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 192
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  afadhal asiitoe, kama anatafuta ulaj sion kam ni rpot nzur badala yake aseme Tanzania hatuna walimu
   
 14. unknown animal

  unknown animal JF-Expert Member

  #14
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  na ndo maana wanafeli
   
 15. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #15
  Oct 5, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Ni kweli...
   
 16. nipeukweli

  nipeukweli JF-Expert Member

  #16
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 16, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  ...hii yote ilianza na suala zima la kuandika kifupi ili kukwepa "multiple in one" msg maana yakizidi na hela inazidi kukatwa. mpk makampuni ya simu yalipokuja na mapromotion ya extreme sijui cheka na jiachie it was already too late, watu wako addicted na cutting words short. dah safari ya elimu bora, tunaenda mbele tunarudi nyuma

  on the other hand, mbona hata sisi katika uandishi wetu huwa tunafupisha kama tunaandika kitu casual mfano sms, fb au tunapopost kitu hapa JF, ila tunapokuwa tunaandika vitu formal huku makazini kwetu huwa tunajisahau? I hope no. mara nyingine ni hawa vijana kujiendekeza tu!
   
 17. Mr Penal Code

  Mr Penal Code JF-Expert Member

  #17
  Oct 5, 2012
  Joined: Jul 9, 2012
  Messages: 777
  Likes Received: 117
  Trophy Points: 60
  halafu ww mbya.....WW upo sawa Kabisa!!!!!!!!!!!
   
 18. Kimbori

  Kimbori JF-Expert Member

  #18
  Oct 5, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 2,724
  Likes Received: 346
  Trophy Points: 180
  Hata mimi naamini kabisa! Hata huku JF kuna wanafunzi na wahitimu wa Vyuo Vikuu wengi wanaandika kihuni kabisa. Wakikumbushwa kurekebisha lugha wanakuwa wakali ile mbaya.
   
 19. idawa

  idawa JF-Expert Member

  #19
  Oct 5, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 18,519
  Likes Received: 10,437
  Trophy Points: 280
  walewale sasa hapo umemaanisha nini.?
   
Loading...