Utafiti: Kumbe tulidanganywa tatizo siyo mfumo ,tatizo ilikuwa ni usimamizi.

Etwege

JF-Expert Member
Jul 4, 2018
5,733
15,199
Habari .

Kutokana na kasi ya serikali ya awamu ya tano katika kutekeleza miradi ya maendeleo kwa wananchi ,sasa nashawishika kusema kuwa tulidanganywa kwamba matatizo ya watanzania kutopata maendeleo yanasababishwa na MFUMO!

Chadema walikuwa wanahubiria watanzania kuwa maendeleo hayatawezekana mpaka mfumo mzima wa ccm uondolewe madarakani na kuingia chama kingine.

Lakini baada ya ccm kurudi madarakani mwaka 2015 wakiwa na rais Magufuli mambo yamebadilika kabisa.
Ccm hiyo hiyo iliyokuwa imeoza kabisa ,sasa wanatoa elimu bure, wananunua ndege, wanajenga flyovers na hata maofisini utendaji kazi umeimarika kabisa tofauti na zamani!

Swali ni nini kimeibadirisha ccm?

Jibu ni usimamizi na ufuatiliaji imara wa rais Magufuli na siyo mfumo kama tulivyokuwa tunaaminishwa na wasaka madaraka.
 
Back
Top Bottom