Abari za siku wana jamvi? Nimekuwa kimya mUda mrefu hii ni kwa sababu ya majukumu yalokuwa yamenibana.Tumukuwa tukishudia au watu kuleta mada hapa juu ya kuumizwa au kutotimiziwa mambo muhimu ktk ndoa au dharau ktk ndoa au kuumizwa kwa vigezo vya fedha au mafanikio ya mtu kifedha aliyeko kwenye ndoa na hii kupelekea ndoa nyingi za watu kuwa ktk hali mizozo mikubwa.Nakuja na ombi kwenu nina mchakato wa kuanza utafiti juu ya kwa nini wasomi wengi kwa sasa hawaoni uthamani wa kuoa au kuolewa. kama itaungwa mkono ifanyike, maswali dodoso yatawekwa hapa na taarifa zote zitakusanywa kwa umakini kwa ajili ya kufanyia utafiti. Idadi ya njia zote za kupata takwimu zitakuwa mbili maojiano pamoja na maswli dodoso yatakayowekwa apa na kisha kutumwa kwa IMELI itakayotumika kwa kazi hii.Tafadhali hii itafanyika tu kama idadi ya waunga mkono itakuwa kubwa.PIA REPOTI YA UTAFITI ITAWEKWA HAPA KUWEZA KUISAIDIA JAMII KUIPITIA KWA LENGO LA KUSAIDIA JAMMII YETU KTK KUISHI NA KULEA FAMILIA ZAO KWA AMANI NA KUWA MFANO BORA KWA JAMII YA KITANZANIA.MUNGU AWABARIKI.