Utabiri wa T B Joshua uko sahihi, Clinton kashinda ila hajachaguliwa

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,798
71,218
Wakuu nimetafakari maneno yanayo zagaa kumkashifu TB Joshua kuwa utabiri wake kuwa mshindi wa kura za urais Marekani ni mwanamke ila kwa kura chache na kushangaa kuwa mbona alichosema ni kweli.

Hillary Clinton; 59,938,290. sawa na 47.7%.
D. Trump; 59,704,886. sawa na 47.5%

Hiyo maana yake ni kuwa kwa kutumia kigezo cha kura Hillary Clinton ndiye mshindi kwa kuchaguliwa na raia wengi wa Marekani.

Lakini kwa mfumo ule wa kura maalum 270 ambao haupo pengine popote duniani hapo ndipo walipo mteua D.Trump kwa kupata 290 dhidi ya Clinton aliyepata 232.

Utabiri wa Joshua sio wa kubezwa na kukashifiwa maana kwa idadi ya kura zaidi ya laki mbili Clinton kashinda na ndio maana hata raia wa US wanaandamana kwa Mara ya kwanza kupinga mfumo huo wa kura maalum 270.

Utabiri wa TB Joshua ulikuwa sawa
 
AROON
Hayo ya kusema atachaguliwa kasema wapi? Yeye kasema atashinda kwa kura na imekuwa hivyo basi.

Hizo habari za kuwa tapeli mie sijui nazungumzia nilichokisoma kwa kauli yake na kilichotokea. Kwangu mimi mtu yeyote anaye taja majina ya Yesu na Mungu siwezi mwita tapeli au muongo mpaka nifunuliwe hivyo na bahati mbaya haijawahi kunitokea kufunuliwa hivyo nanyamaza hata kama nitaamua kutokumfuata.
 
Yaani kunawatu wanapoteza muda kutetea vitu ambavyo vipo dhahiri. yaani hata ukifanyaje neno lilishatoka na yule bwana amekosa kweny ramli zake. usiumize kichwa. Mungu muumbaji alitaka kutuonesha kitu. lakini unafumba macho hulazimishwi kuona, endelea kusiinzia.
 
Lakini kwako wewe kwa maana ya kura nani kashinda? Haina umuhimu kwa sasa, lakini nimeweka hapa kwa vile naona upotoshaji kuwa kasema uongo, uongo uko wapi kama alimaanisha ya kura za raia? Na why huko kwao kwa mara ya kwanza watu wanalalamikia aina hiyo ya ushindi?
Twaweza kumchukia Joshua lakini alichosema alikuwa sahihi.
 
Hayo ya kusema atachaguliwa kasema wapi? Yeye kasema atashinda kwa kura na imekuwa hivyo basi.
Hizo habari za kuwa tapeli mie sijui nazungumzia nilichokisoma kwa kauli yake na kilichotokea. Kwangu mimi mtu yeyote anaye taja majina ya Yesu na Mungu siwezi mwita tapeli au muongo mpaka nifunuliwe hivyo na bahati mbaya haijawahi kunitokea kufunuliwa hivyo nanyamaza hata kama nitaamua kutokumfuata.
Mpaka ufunuliwe ndio uwajue matapeli

Basi utatapeliwa mpaka unaingia kaburin

Yeye mwenyewe TB Joshua kafuta post fb kwa aibu

Utabiri uliofanywa na muhubiri maarufu wa Nigeria, TB Joshua kwmba Hillary Clinton atashinda uchaguuzi wa urais nchini Marekani umeondolewa katika akaunti yake ya facebook.

Bwana Joshua aliwaambia wafuasi wake siku ya Ijumaa kwamba ameona mwanamke akishinda.

Baada ya Donald Trump kushinda kwa wingi wa kura katika uchaguzi wa Jumanne, wageni katika ukurasa wa facebook wa Muhubiri huyo walishangaa walipoona utabiri huo umeondolewa.

SOURCE:BBC
 
Lakini kwako wewe kwa maana ya kura nani kashinda? Haina umuhimu kwa sasa, lakini nimeweka hapa kwa vile naona upotoshaji kuwa kasema uongo, uongo uko wapi kama alimaanisha ya kura za raia? Na why huko kwao kwa mara ya kwanza watu wanalalamikia aina hiyo ya ushindi?
Twaweza kumchukia Joshua lakini alichosema alikuwa sahihi.
Ha ha ha

Huyo Mungu wake hakujua wanatumia VITUO miaka yote kuhesabu?

Kule fb amefuta ile post yake

Ha ha ha ha
 
Sijui kama watu tunaelewa vizuri utabiri na ubashiri. Labda mnatumia haya maneno interchangably
 
Back
Top Bottom