Trump huenda akaanguka Urais Marekani, Macho yote majimbo(state) matatu Nevada, Wisconsin na Michigan

Elvis Legacy

JF-Expert Member
Aug 10, 2017
3,385
4,711
Habari wakuu.

Kulingana na ukweli kuwa Demokrasia ya Marekani ni tofauti sana na yetu ambapo matokeo ya Urais yanaamuliwa na Electoral college votes, kwenye majimbo 50 kila jimbo linakuwa na namba ya Electoral collage votes kulingana na idadi ya raia katika jimbo(state) husika.

Ili uwe mshindi ni sharti upate Electoral college votes 270. Endapo mtalingana basi maamuzi yatafanywa na House of Representatives kwa Rais na Senate kwa makamu wa Rais.

Mpaka sasa Joe Biden wa Democrat ana Electoral college votes 238 wakati Donald Trump wa Republican ana Electoral college votes 214.

Joe Biden anahitaji Electoral college votes 32 ili aweze kuwa Rais mpya wa marekani ambapo anategemea majimbo hayo matatu, Nevada, Wisconsin na Michigan ambayo yana jumla ya Electoral college votes 32. Mpaka sasa anaongoza kwenye kura za wananchi kwenye majimbo hayo japo Trump anamfukuzia kwa ukaribu sana.

Kura za wananchi hazina maamuzi ya nani atakuwa Rais maana hata Hillary Clinton alishinda kwa kura zaidi ya milioni tatu lakini Trump alishinda hizo za Electoral college votes na kuwa Rais.

Lolote linaweza kutokea Marekani. Japo Trump ameshaanza kulalamika kuibiwa kura.
 
Jimbo la Wisconsin tayari Joe Biden ameshinda kura zote 10 za Electoral college votes. Sasa ana jumla ya kura 248

Yamebaki majimbo mawili, Nevada na Michigan kufanya maamuzi. Endapo atashinda hayo majimbo basi utawala wa Donald Trump utakuwa umefika mwisho.
 
Trump ameanza kulalamika kuwa kura za jimbo la Wisconsin zihesabiwe upya.

Pia kura za Michigan zisitishwe kuhesabiwa.

Sababu zisizoeleweka zimesitisha kuendelea kuhesabiwa kwa kura za Nevada.

Mpaka kesho Trump atakuwa amefanikiwa kufanya hujuma. Sio kwa harakati hizi. Vinginevyo Joe Biden ameshamkalia pabaya.
 
Michigan inaenda kuhitimishwa na hakuna dalili zozote za Trump kupindua meza. Maana 99% ya kura zimeshahesabiwa na Joe Biden anaongoza kwa kura zaidi ya elfu 30.
 
Nevada, where Biden leads according to the @AP, will not announce any new updates on election results until 9 a.m. Pacific time on Thursday, state election officials said.

C&P from USA TODAY
 
Hali ilivuo sasa
Screenshot_2020-11-05-02-59-11.png
 
Back
Top Bottom