Utabiri wa hali ya umeme siku ya leo

Utabiri wa hali ya umeme siku ya leo

Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Joined
Dec 6, 2006
Posts
3,019
Reaction score
580
Source: Yahoo friends

KUMBE WATABIRI WAPO!!!
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TD]Habari za saa hizi mabibi na mabwana.

Na ufuatao ni utabiri wa hali ya Umeme kwa siku ya leo!

Pepo za umeme zitavuma taratibu kutoka upande wa kusini mwa Dar es Salaam kuelekea upande wa Kaskazini hivyo kutakuwa na umeme mchache maeneo yote ya Jiji na ngurumo nyingi za Jenereta pande za Kariakoo,Boko, Mwenge, Posta na maeneo yote ya katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Na kwa wakati wa usiku watu wa Mbagala, Kigamboni, Kimara, Mtoni na maeneo yote ya jirani wilaya ya Temeke na Kinondoni kutakuwa na Kiza kisichojulikana mwisho wake ........ Maeneo ya Sinza, Mbezi na Tegeta kutakuwa na miunguromo ya jenereta hapa na pale nyakati za usiku , hii ni kutokana na familia chache zinazotumia jenereta nyakati za usiku

Ni kutoka mamlaka ya utabiri wa nguvu za umeme Ubungo Tanesco ghorofa ya Pili ....... Nawatakia siku njema. Ahsanteni.


Regards,


[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Tuwe na moyo wa subira. Suala la mgao wa umeme litakuwa HISTORIA hivi karibuni!
 
kiuhalisia tayari swala la mgawo wa umeme limeshakuwa historia sasa sijui tunataka historia ipi tena? Nimefurahi kama tunaweza kuhama kutoka katika utabiri wa hali ya hewa na kutabiri mgawo wa umeme kwa ufasaha mkubwa.
 
Tuwe na moyo wa subira. Suala la mgao wa umeme litakuwa HISTORIA hivi karibuni!

Hahahahaaaaaaaaaaa!!!!!!!!! Limeanza kuwa historia pale Uwanja wa Taifa...
Teh teh teh teheeeeeeeeeeeeeeee, efyuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!
 
Tuwe na moyo wa subira. Suala la mgao wa umeme litakuwa HISTORIA hivi karibuni!
unafanya kazi tanesco ama? we want proof na cyo maneno tu bila vitendo, if ur, am telling u, i hate tanesco
 
Back
Top Bottom