Ulimwengu wa leo tunao waumini waliopitiliza. Wamepitiliza kwa kuwa hawasomi neno (wamwemwachia Mchungaji/Padre). Wanaamini kila wanachoambiwa masikini. Wachungaji nao ni watu. kuna wa kweli na wa uwongo pia. Mtu anaweza kuwadanganya kadiri awezavyo (nina visa vingi kwenye hili)
Hakuna miujiza kwenye uhalisia. Mungu anakupa mtu wa kufanana na wewe na anakupa kitu unachoweza kukibeba. Tatizo injili inaelekea kufurahisha watu, wewe utoke from know where ukakae na wafalme kabla hujaandaliwa /hujafinyangwa? Kwenye maandiko sijawahi kuona hiko.. Wote waliokuwa wakubwa kuna hatua walipitishwa kabla. Injili ni uhalisia na sio miujiza.
Pili: Waumini wameaminishwa kuwa ni mchungaji pekee anayeweza kuwaombea ikasikiwa, Hio ilikua zamani. Pazia la hekalu lilipasuka kutoa ACCESS ya mimi na wewe kupaendea patakatifu. Unaendaje hio ni habari nyingine.
Tatu: Mungu ana njia nyingi ''Njia zangu sio njia zenu na mawazo yangu sio mawazo yenu '' na kwenye maandiko tumeona namna mbali mbali alivyojifunua kwa matukio mbali mbali, basi katika hayo tujifunzeni ufanyaji kazi wake..
Tujazwe NENO kwa wingi, vinginevyo tutahangaishwa hadi tukome.. mara njooni mchukue waume, mashamba, safari za ulaya, sijui magari, sijui nyumba.... n.k. ''Mungu si mwanadamu hata aseme uwongo na Anafuatilia NENO lake aweze kulitimiza''... anything out of His WORD ni ya kwetu.
Wachungaji tuwasikilize lakini tuyafanyie reference maneno yao kwenye NENO. vinginevyo ni hatari kwa nyakati hizi kuwa wasikivu WASIOFIKIRI.

No usiseme hivyo...Endelea kumuomba Mungu tu...Usitegemee kwa mchungaji mana mchungaji ni mtu kama mimi au wewe...Mtegemee Mungu wako,Sina hamu nao hao nilitabiriwa kujifungua mtoto mpaka jina la mtoto nikapewa.nikapangiwa hadi atakaomshika badala yake mtoto alikufa hata hakuiona dunia.Kiasi kikubwa imani yangu imeshuka saaana.
unataka tukurupuke tu?
Wewe ndo unapotosha watu ukimuabudu Mungu katika roho na kweli lazima atakupa haja ya moyo wako haijalishi ni kitu gani inaweza kuwa mme au mke, shamba, kazi, afya njema, Na kama usipomwamini kiongozi wako whether ni Shekhe, Nabii, Mchungaji, Padre actually huwezi kumuamini Mungu pia,
Ushuhuda mimi hapa Mungu kaniinua from zero to hero
LIKE,LIKE LIKE. Mkuu Tized umemaliza,ni kweli kabisa wakristo wa leo tumekuwa wavivu sana kusoma neno na kuomba tunategemea watu wengne watufanyie matokeo yake tunapewa matango pori.
Neno la Mungu linatuagiza kwamba tumtafute Bwana maadam anapatikana tumuite yu karibu.,lakin ajabu wanadamu wa leo hatuishi kubun njia zetu kinyume na mapenzi yake.
Matokeo ya kutopenda kuomba sisi wenyewe ni kupewa unabii wa uongo,kupewa maji,mafuta,vitambaa,chumvi n.k mwisho wa siku ni kugeuka na kumkejel Mungu kwamba hatendi kumbe tatizo ni sisi wenyewe kutopenda ushirika na Mungu moja kwa moja.