GAGL
JF-Expert Member
- Aug 5, 2010
- 392
- 400
Ilitamkwa waziwazi na viongozi akiwemo na mgombea urais ccm kuwa LAZIMA WASHINDE kwa zaidi ya asilimia 80, hili lilitiliwa mkazo na wasomi wasaliti kama prof. Mukandara kupitia taasisi zao dhalimu. Huu ni utabiri wa ajabu kwa kuwa umeweka neno LAZIMA, ambalo inatakiwa tulijengee hoja wazalendo wenzangu. Kwa maneno mengine ccm walikuwa wanasema kwa wapinzani wazalendo kama Rais wangu Dr.Slaa, kuishinda ccm, ni sawa na kuomba samaki kwa mmasai. Lakini kuna kitu cha kujadili hapa jamvini, ushindi huu uliotabiliwa kiajabu, ulitarajiwa kutoka wapi na nguvu ipi? Nguvu ya dola au Nguvu ya uma(peoples power) 'wakati tunajadili naomba msaada wa mawazo na hasa upande wa kisiasa, kwa sababu nataka kugombea ubunge 2015 sikonge kupitia chama cha watu, Chadema' nawasilisha.