UTABIRI KUTIMIA (Shairi)

UTABIRI KUTIMIA (Shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
Hii ni sehemu ya shairi lililoandikwa na Idd Ninga ,shairi linaitwa UTABIRI KUTIMIA



1>picha imeshadhihiri,mwisho wao umefika.
Utatimu utabiri,ule niliouweka.
Yote niliobashiri,yaonekana yatoka.
Bora sasa tupumue,utabiri kutimia.
2>hata kama iwe shari,mwisho wao utafika.
Tutavipiga vidari,mikono tutaishika.
Tuziepuke hatari,na balaa la majoka.
Bora sasa tupumue,utabiri kutimia.
3>walizitupa khabari,wakasahau hakika.
Maovu yaliyojiri,wenyewe waliyapika.
Wakajifanya viburi,leo sumu watapika.
Bora sasa tupumue,utabiri kutimia.
4>pamoja majemedari,bendera twenda ishika.
Kwa miguu na kwa gari,kuta yao yapasuka.
Mashujaa ni hodari,ushindi tumeusuka.
Bora sasa tupumue,utabiri kutimia.
5>limepasuka tairi,jahazi limepinduka.
Wote sasa tu tayari,maarifa kuzinduka.
Bila hata ya hiyari,wenyewe mtang'atuka.
Bora sasa tupumue,utabiri kutimia.
Shairi=UTABIRI KUTIMIA.
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 Au 0655519736.
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom