FARARI (shairi)

FARARI (shairi)

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
1>upo mwingi usafiri,ila huu ni hatari.
Hatari si kama gari,lipasukapo tairi.
Nawaza naufikiri,sitopanda kwa hiyari.
Namwaza huyu farasi,siku nikija mpanda.
2>na ulimi ulikiri,kiri imani hariri.
Ninamuomba ghafari,ya ilahi ya qahari.
Afanye yangu safari,vyema mimi nisafiri.
Namwaza huyu farasi,siku nikija mpanda.
3>mwendo wake ni wa kasi,farasi huyu ajabu.
Wote wafanya maasi,watampanda kwa tabu.
Wakitokwa na kamasi,bora mapema kutubu.
Namwaza huyu farasi,siku nikija mpanda.
4>farasi hana kelele,ni mkimya wa sauti.
Hutompanda milele,hutompanda kwa suti.
Hata wako ukelele,utazimwa kwa manati.
Namwaza huyu farasi,siku nikija mpanda.
5>farasi siyo mzuri,japokuwa apendeza.
Atanukishwa uzuri,hakuna ataecheza.
Na tandiko lilo zuri,litafunikwa jeneza.
Namwaza huyu farasi,siku nikija mpanda.

Shairi=FARASI.
MTUNZI=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
0755519736 Au 0655519736.
 
Back
Top Bottom