UTABIRI: Katika michezo 4 ijayo ya Ligi, Simba SC itaambulia alama 5 au pungufu kati ya alama 12

THE FIRST BORN

JF-Expert Member
Apr 24, 2019
1,729
3,288
Habari wanajukwaa

Nimeangalia michezo ijayo ya Simba katika michezo 4 jayo kwenye ligi. Aiseeee 😁😁

Niseme tu kwa hii Fixture Simba itapata ushindi mmoja na itasare michezo 2 na itapoteza mchezo moja. Sitaki kuwambia kwanini nimetabiri hivyo ila subirini.

Na ikifanya mzaha huenda ikapata points 4 tu.

Toa Maoni yako unaonaje wewe?

#Mnaruhusiwa Kutukana

Screenshot_20231224-165524_Flashscore.jpg
 
Kinachonichekesha kwa upande wangu ni kuahirishwa tu kwa mechi kati ya Azam na Simba!!! Sijajua shida iko wapi eti kiasi cha kusababisha hiyo mechi kuahirishwa kwa nyakati mbili tofauti.
Azam FC hawajitambui huu ulikua wakati wao wa kujihakikishia nasafi ya pili kwanza hio mechi wao ndio wenyeji wangegomea kucheza mechi zingine mpka wacheze hio mechi ajabu wapo kimya
 
Hii imekaaje, kwenye mechi nne timu inacheza mechi tatu ugenini.
Jografia ya nchi yetu ndio inafanya mtu acheze game 3 mfululizo ugenini au nyumbani. Mfano una game na Prisons Mbeya unataka urudi Dar badala umalizane na Ihefu kabisa ?? Au una game na Kagera Sugar lazima umalizane na Mashujaha kabisa. Huwezi kwenda Kagera then urudi dar halafu uende tena Kigoma
 
Ratiba za ligi kwa kiasi kikubwa zinanufaisha timu kubwa. Fikiria mpaka sasa katika mechi 11 Yanga ilizocheza, wametoka nje ya Dar mara mbili 2 tu. Simba hivyo hivyo. Matokeo yake ni rahisi sana kutengeneza mazingira ya ushindani wa ubingwa kuzifeva timu hizo.

Nilichogundua timu za mikoani zimeimarika sana na zina uwezo wa kutoa ushindani mkubwa kama mizania ya ushindani itawekwa sawa kuanzia kwenye ratiba hadi waamuzi.

Binafsi ningependa ligi ingekuwa na ushindani zaidi kiasi kwamba Simba au Yanga kufungwa au kutoa sare na timu ya mkoani isionekane kama ni jambo la kushangaza sana.
 
Habari wanajukwaa
Nimeanglia Fixture ya Simba Katika Michezo 4 Ijayo kwenye Ligi,
Aiseeee😁😁

Niseme tu kwa hii Fixture Simba Itapata Ushindi Mmoja na itasare Michezo 2 na itapoteza Mchezo Mmoja..
Sitaki kuwambia Why nimetabiri hivo ila subirien.

Na ikifanya Mzaha huenda ikapata points 4 tu.

Toa Maoni yako unaonaje wewe?


#Mnaruhusiwa Kutukana

View attachment 2851645
Tutarudi tena hapa inshaAllah, tushuhudie ukiumbuka wewe sheikh Yahya wa mchongo.
 
Back
Top Bottom