Utaadhimishaje kutokomea kwa magonjwa sugu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utaadhimishaje kutokomea kwa magonjwa sugu

Discussion in 'JF Doctor' started by Azimio Jipya, Mar 11, 2011.

 1. Azimio Jipya

  Azimio Jipya JF-Expert Member

  #1
  Mar 11, 2011
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 3,370
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135

  Kama ikitokea leo hii, magonjwa sugu mbalimbali yakapatiwa dawa, jamii ingefurahia na maadhimisho yangefanyika kwa mafanikio yaliyopatikana.

  Lakini hata kabla tiba za magonjwa yote sugu hazijapatikana, bado hatukati tamaa na tunatamani sana zisifikiwe. Hii inamfanya kila mmoja wetu kuwa na matarajio ya namna atakavyoadhimisha kupona ugonjwa fulani yeye au mwenzake.

  Kuna baadhi ya magonjwa yanaathiri kwa namna tofauti karibu familia zote. Na bado athari hizi zinaendelea hadi kufikia nyanja zote za ustawi na maendeleo ya jamii. Hivyo kutokomezwa kwa magonjwa haya ingekuwa ni tukio la kufanyiwa maadhimisho.

  Kila mmoja wetu ana ndoto za kupatikana kwa tiba ya magonjwa ambayo bado tiba haijapatikana. Pia kila mmoja wetu ana ndoto ya maadhimisho atakayofanya punde mafanikio hayo yatakapofikiwa na kuwa rasmi. Hii inaifanya jamii nzima kuwa na matarajio mbalimbali ya jinsi ya kufanya maadhimisho hayo hasa pale kisukari, kansa , ukimwi nk vitakapotoweka.

  Tunataka tutoe muda wetu kuzifuatilia ndoto hizi za maadhimisho, tuzitizame kwa karibu. Tunataka tuzielewe na kuona kama zinaweza kutupa mafundisho yeyote yenye maana, sasa au hata baada ya ufumbuzi kupatikana.

  Utafanya sherehe gani???????
   
Loading...