Ustaadhi Aoa Mke wa Mgoni Wake | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ustaadhi Aoa Mke wa Mgoni Wake

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MaxShimba, Sep 16, 2011.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Jiji letu la Bongo ni kubwa lisiloisha vituko kila kukicha, Ustadhi aliyefahamika kwa jina la Shaaban Rajabu, maarufu 'Kidevu' mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, hivi karibuni aliwashangaza majirani zake alipotangaza ndoa na mke wa mgoni wake muda mfupi baada ya kuwafumania, Tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Midizini Manzese, jijini Dar es Salaam, Kidevu ambaye ni mfanyabiashara maarufu, alifikia uamuzi huo baada ya kumfuma rafiki yake wa karibu aitwaye Majuto...
  [​IMG]


  Jiji letu la Bongo ni kubwa lisiloisha vituko kila kukicha, Ustadhi aliyefahamika kwa jina la Shaaban Rajabu, maarufu ‘Kidevu’ mkazi wa Manzese jijini Dar es Salaam, hivi karibuni aliwashangaza majirani zake alipotangaza ndoa na mke wa mgoni wake muda mfupi baada ya kuwafumania.
  Tukio hilo lilitokea katika Mtaa wa Midizini Manzese, jijini Dar es Salaam.
  Kidevu ambaye ni mfanyabiashara maarufu, alifikia uamuzi huo baada ya kumfuma rafiki yake wa karibu aitwaye Majuto maarufu Lunyungu akikandamiza raha na mkewe aliyejulikana kwa jina la Leila katika Baa ya Mississippi iliyopo Manzese.
  Akisimulia mkasa huo, Kidevu alisema kuwa yeye ni mpangaji katika nyumba ya familia ya Lunyungu, ingawa mwenye nyumba huyo alikuwa akiishi Mabibo lakini mara kwa mara alikuwa akifika nyumbani kwake (Kidevu) kumtembelea.
  Kidevu alisema, siku moja kabla ya tukio, Lunyungu alifika nyumbani kwake ambapo kuna grosari na kuagiza kinywaji kisha baada ya muda yeye na mkewe wakatoweka.
  “Kitendo cha kutoweka kwa mke wangu katika mazingira ya kutatanisha kukanifanya niingiwe na wasiwasi, hata hivyo, nikavuta subira nikiamini kuwa angerudi lakini hadi usiku hakurejea. Nikachukua jukumu la kwenda kwa dada yake anayeitwa Jaka anayeishi Kigogo kumtaarifu juu ya suala hilo,” alieleza Kidevu
  Aliongeza kuwa siku hiyo mkewe hakurudi kabisa nyumbani hadi kesho yake alipopewa taarifa na mke wa Lunyungu aitwaye Pili kuwa alimuona Leila akiwa na Lunyungu katika Baa ya Mississippi wakiponda raha na kumuomba waende kuwafumania.
  “Taarifa hiyo ilinishtua, hivyo tulifuatana pamoja na wapambe hadi kwenye baa hiyo na kufanikiwa kuwafumania wagoni hao wakiwa katika mahaba mazito, lakini walipotuona walikimbia,” alisema Kidevu.
  Aliongeza kuwa baada ya wagoni wao kukimbia, yeye na Pili waliumia sana moyoni hivyo, waliamua kurudi nyumbani ili kuwasubiri lakini kilichowashangaza ni kuwa watu hao hawakurudi.
  Aidha, Kidevu alisema baada ya kuona wawili hao hawatokei walikubaliana kuwa nao wafunge ndoa kwa vile mkewe na Lunyungu walikuwa wamesaliti ndoa zao.
  “Tulifikia uamuzi wa kuoana, baada ya kuona Lunyungu amekimbia na mke wangu nami ikabidi nimchukue mkewe, nikaandika talaka siku hiyo hiyo, saa kumi nikapeleka posa ya kumuoa mke wa Lunyungu na ikakubaliwa, hivyo tangu siku hiyo tunaishi pamoja,” alisema Kidevu.
  Naye aliyekuwa mke wa Lunyungu, Pili Said alisema kuwa amefurahishwa na uamuzi waliouchukua kwani alikuwa akifikiria ataishi vipi baada ya kukimbiwa na mumewe.
  “Leila amekimbia na mume wangu nami inabidi niishi na mume wake, nilikuwa nikifikiria wapi nitaenda lakini nimefurahishwa na uamuzi tuliouchukua, nina imani tutapendana na kuishi kwa amani katika ndoa yetu,” alisema Pili.
  Hata hivyo, habari zaidi zinasema kufuatia fumanizi hilo aliyekuwa mke wa Kidevu (Leila) amekuwa akimpigia simu mumewe na kuomba radhi ili warudiane lakini mumewe amekuwa akikataa.
  Imetoka dar411
   
 2. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2011
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  Wanafiki tu hao sema hii ni WIFE SWAP bongo edition.
   
 3. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  duh hii kali....
   
 4. K

  Kilembwe JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2011
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 1,132
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Hahahah ukisikia ukimwaga mboga nami namwaga ugali basi ndo hii!
   
 5. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #5
  Sep 16, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Na hadithi yangu ikaishia hapohapo! Hadithi hii kakufundisha nani mjomba, kanifundisha shangazi! Kakwambia ina maana gani? Hakuniambia!
   
 6. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  [h=3]USTAADH ANAPOFUMANIWA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI![/h]

  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [​IMG]
  [TABLE]
  [TR]
  [TD="align: left"][/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Mkazi mmoja wa Karakata jijini Dar es Salaam, aliyefahamika kwa jina la Ustaadhi Hemed Mlawa, ameanza sikukuu ya Idd vibaya baada ya kufumaniwa akiwa gesti na mke wa jirani yake.


  Tukio hilo lilitokea Jumatano saa 3.30 usiku katika nyumba ya kulala wageni (gesti) iitwayo Maridadi Bar & Guest House, iliyopo Kiwalani jijini Dar es Salaam.

  Kwa mujibu wa mtoa habari, Mlawa licha ya kuwa ni muumini ya dini ya kiislamu katika eneo analoishi na kupewa pia cheo cha kuwa ustaadhi ana mke na mtoto mmoja.

  Habari zilisema kuwa Mlawa ambaye ni muuza mkaa wa Karakata alikuwa akimsubua kwa kumtongoza mke wa jirani yake huyo aliyefahamka kwa jina moja la Rashid, kila mwanamke huyo alipokwenda kununua mkaa.

  Mtoa habari huyo alisema kuwa, baada ya kuona anasumbuliwa kila mara, mwanamke huyo aliamua kumfahamisha mumewe (Rashid), ambaye alikasirishwa na kitendo hicho.

  Kutokana na hali hiyo, Rashid aliwafahamisha ndugu zake kuhusu tabia ya muuza mkaa huyo na ndipo walimshauri wamshikishe adabu, ili iwe fundisho kwa watu wengine wenye tabia ya ‘kuzengea' wake za watu.

  Mnyetishaji wetu alisema, kilichowatibua zaidi ni kwamba, licha ya Mlawa kuwa muislamu anayefunga Ramadhani pia ana mke na mtoto, aliendelea kumsumbua kumtaka kimapenzi mke wa mtu.

  Habari zilisema, siku ya tukio Mlawa alimpigia simu mwanamke huyo na kumwambia kuwa afanye kila njia wakutane Buguruni baada ya futru.

  "Mwanamke huyo alimfahamisha mumewe kuhusu ombi hilo, ambapo walishauriana kumwekea mtego na mipango ikaandaliwa,"
  alisema mtoa habari wetu.

  Mara baada ya kumaliza kufuturu, mwanamke huyo aliondoka kuelekea Buguruni, huku mumewe akitangulia eneo hilo la tukio kwa usafiri wake.

  Habari zilisema kuwa muda mfupi baada ya mwanamke huyo kufika katika Kituo cha Mabasi cha Rozana Buguruni, Mlawa alimpigia simu na kumtaka amfuate Umoja Gest House, karibu na kituo cha mabasi cha Chama, anamsubiri.

  Mwanamke huyo alipofika walichukuwa chumba namba 16B, na kuagiza soda, ambapo walianza kunywa huku wakipiga stori ndogondogo, bila kujua kuwa Rashid akiwa na vijana sita wakiwemo wapiga picha wetu walikuwa wakifuatilia zoezi hilo.

  Wakati Rashid akiwa anasubiri mawasiliano ya mkewe ili wavamie chumbani humo, Mlawa alishtuka na kumtaka mke wa jamaa waondoke eneo hilo haraka, baada ya machale kumcheza.

  "Walitoka nje ya gesti na kukodi taxi, Rashid pamoja na vijana wake wakiwemo wapigapicha wetu nao wakiwa na magari mawili na pikipiki moja, walianza safari ya kuwafuata," alisema mtoa habari huyo.

  Safari ya Mlawa na mwanamke huyo iliishia katika nyumba ya kulala wageni ya Malidadi Bar & Guest House, ambapo walichukuwa chumba namba 202.

  Mtoa habari huyo aliongeza kuwa baada ya kuelekezwa chumba walichokuwemo, Rashid na wenzake walifika gesti hiyo ambapo mmoja alitinga mapokezi kama mteja, huku wengine wakipitiliza moja kwa moja hadi chumba husika na kugonga mlango.

  Aidha baada ya kugonga, mlango ulifunguliwa ambapo Rashid na wapiga picha wake walitinga chumbani jambo lililomfanya Mlawa anyanyuke haraka kutoka kitandani na kukimbila bukta yake ili avae.

  Hata hivyo, Rashid alimrukia na kuanza kumtandika makonde, hatua iliyokifanya chumba hicho kugeuka uwanja wa masumbwi kwani ustaadhi huyo naye alikuwa akirusha ngumi kama bingwa wa zamani wa ndondi duniani Michael Tyson.

  Wapiga picha wakiwemo wa gazeti la Risasi walifanikiwa kumpiga picha kadhaa.

  Meneja msaidizi wa gesti hiyo aliyefahamika kwa jina moja la Alex alipofika chumbani humo, vurugu ilitulia na Mlawa alipohojiwa kwanini aliingia chumbani na mke wa mtu, alidai kuwa hakujua kama mwanamke huyo ameolewa.

  Hata hivyo, kauli hiyo ilipingwa na Rashid ambaye alidai kuwa Mlawa anafahamu kuwa mwanamke huyo ni mkewe na kwamba ni majirani.

  Aidha meneja wa gesti hiyo aliita polisi wa kituo kidogo cha Kiwalani ambao walifika na kuwachukuwa Mlawa, Rashid na mwanamke huyo hadi kituoni kwa ajili ya kutoa maelezo.
  Katika maelezo yake, Mlawa alikiri kufumaniwa na kuomba msamaha kwa maandishi
   
 7. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Is this clergical?
   
 8. only83

  only83 JF-Expert Member

  #8
  Sep 16, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 5,252
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  .............Mahakama ya kadhi inahitajika wakuu teh teh teh...
   
 9. Mulhat Mpunga

  Mulhat Mpunga JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 25,538
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Hahaha mahakama ya kadhia,hii style ni jino kwa meno mwana fa aliimba mtu akimmega dem wako na wewe unatafta dem unamduu haleti heshma ila inapunguza maumiv
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Sep 16, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  mnh...................eti apiugwe mawe hadi kufa,huh
   
 11. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #11
  Sep 16, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
 12. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #12
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,822
  Likes Received: 22,467
  Trophy Points: 280
  hili neno ustaadhi hapa limekuja vipi????????
   
 13. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #13
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,971
  Likes Received: 2,967
  Trophy Points: 280
  Hapa wamefanya swaping. Good, ukimwaga mboga namwaga ugali. Ila je hapo kuna mapenzi ya kwel au usanii mtupu? Kama wana watoto nao watawafanyia swaping au?
   
 14. fabinyo

  fabinyo JF-Expert Member

  #14
  Sep 17, 2011
  Joined: Aug 5, 2011
  Messages: 2,084
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  eehh,hiyo ni remix ya ukweli
   
 15. STREET SMART

  STREET SMART JF-Expert Member

  #15
  Sep 17, 2011
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 668
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  NOW DAYS KILA MTU NI USTADHI. USTADH MREMA,USTADHI MBOWE.....
  [h=2]Re: Ustaadhi Aoa Mke wa Mgoni Wake, USTAADH ANAPOFUMANIWA NDANI YA MWEZI WA RAMADHANI!
  - NENO USTADH LIMETUMIKA KISHABIKI ILI KUUZA GAZETI, WANAOPATWA KWENYE HILI NI WALE WENYE CHUKI NA ISLAM TU..MAUSTADHI WENGINE HAWA USTADH ZITTO, USTADH INVISIBLE[/h]
   
 16. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #16
  Sep 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,807
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  mbona umekuwa sooo defensive?hajatajwa mtu wala dini tayari unataharuki.....??
   
 17. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #17
  Sep 18, 2011
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  Yale yale
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...