eden kimario
JF-Expert Member
- Jun 13, 2015
- 10,356
- 16,400
Baadhi ya makatibu wa wilaya mbalimbali nchini wamekerwa na ugumu wanaoupata katika Ukusanyaji wa wawatu sehemu mbalimbali ikiwemo na ya urais makatibu hao wamesema jukumu walilopewa ni gumu kwa kua pesa wanazopewa ni kidogo na hazitoshi kuwashawishi watu kuhudhuria mikutano yao kwani inatakiwa uwanja uonekane umejaa kwani sh/5000-10000 wanazotoa wengine wanazikataa
Makatibu hao ambao hawakutaka majina yao yawekwe hadharani wala wilaya wanazosimamia walisema wilaya zote nchini zimepewa pesa ili kuratibu mikutano hiyo na hata kuwasafirisha watu kutoka sehemu mbalimbali ili uwanja uonekane umejaa.
Wakati mwingine hua tunapata tabu sana kwa kuwakusanya na kuwasafirisha kutoka katika maeneo husika hadi katika eneo la mkutano na kuwalipa shida ni kubwa sana wakati wa kuwapa nauli sisi tunakua hatujakabidhiwa fedha hivyo kuanza kusumbuana na viongozi wa misafara ya wagombea. Mikutano yote hasa ile ya urais inatubidi tukusanye watu wa kutosha ili uwanja uonekane umejaa na hivyo inatubidi kuwalipa pesa nyingi watu hao wanaohudhuria mkutano huo.
Makatibu hao walisema wamekua na wakati mgumu kuliko mwaka wowote walizowahi kufanya kampeni kutokana na watu wengi kutokua na mwamko na chama hicho na badala yake bila kulipwa wamekua hawafiki kwenye mikutano yao.
Naibu katibu mkuu CCM bara rajabu luwavi alipoulizwa juu ya shutuma hizo kutoka kwa makatibu hao wa wilaya wa CCM alisema hazina ukweli wowote na zina lengo la kukichafua chama huku akimsifu magufuli kua ana kipaji cha kipekee kinachovutia watu kuja wenyewe kumwangalia na kusikiliza Sera
Lakini luwavi alikiri kuna watu wana safiri umbali mrefu kwa ajili ya kumuona magufuli hivyo wao hawawezi kuwazuia kwa kua ni mapenzi yao lakini sio wanawapa pesa kama makatibu hao wanavyosema.
Chanzo: Tanzania daima