Usomaji wa nyota yako kila siku

Usomaji wa nyota yako kila siku

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,455
Reaction score
6,465
USOMAJI NYOTA JUMAPILI 17/8/2025

MSHALE

Mtu unayemjali atapata habari njema ambazo pia zitakunufaisha wewe. Mtu wako wa zamani atakufikia kwa njia isiyokuwa ya fujo. Utapata wakati utakaoufanya useme "maisha ni mazuri kwa kweli".

MBUZI

Utakuwa mahali fulani kwa wakati unaofaa ili kupata fursa. Pongezi kutoka kwa mtu ambaye ni mgeni kwako zitabaki nawe wiki nzima. Utaweza kufanya jambo ambalo umekuwa ukilihairisha mara kwa mara.

NDOO

Kutokuelewana kutatokea na utagundua kwamba mtu huyo anakuheshimu sana kuliko vile ulivyojua. Kosa la bahati mbaya litakuokoa kutokana na tatizo kubwa zaidi. Ikiwa umekuwa ukiepuka kitu fulani kwa uwoga, utagundua kuwa ni kitu rahisi zaidi kujaribu.

SAMAKI

Mgogoro unaoweza kutokea utatoweka kabla hata hujaanza. Utapata uthibitisho kwamba ulifanya chaguo sahihi juu ya jambo fulani. Mtu atakusaidia bila kutarajia malipo yoyote. Utaachana na tabia ndogo ambayo imekuwa ikikuzuia kimya kimya.

PUNDA

Mtu atakusimamia bila hata wewe kumuomba. Barua pepe (email) au ujumbe wako utageuka kuwa fursa. Utasikia kitu ambacho kinahisi kama kilikusudiwa usikie. Utapewa kitu kitakchokuweka katika hali nzuri zaidi ya kifedha.

NG'OMBE

Fursa nzuri sana inakuja, unaweza hata kutia sahihi kwenye kitu rasmi. Subira yako itazaa matunda. Mtu anakaribia kufuta deni analodaiwa na wewe, hat hutolazimika kuongea sana atakulipa tu.

MAPACHA

Utajisikia vizuri zaidi kwenye ngozi yako kuliko vile ulivyokuwa nayo kwa muda. Utaepuka hali mbaya bila hata kujua ilikuwa karibu kutokea. Kupata nafasi ya pili katika jambo ulilofikiri limeisha.

KAA

Mtu unayemmiss atakufikia wakati hukutarajia. Mtu atataka kushirikiana nawe kwa njia ambayo itawanufaisha nyote wawili. Jina lako litatajwa kwa njia nzuri na mtu. Ununuzi wako unaofuata utaleta furaha zaidi kuliko kujutia.

SIMBA

Utakutana na mtu ambaye anahisi kama alitumwa mahususi kwa ajili ya sura hii ya maisha yako. Mtu atakupatia kitu bila malipo ambacho kwa kawaida huwa kinagharimu pesa. Ushindi mdogo utasababisha kitu kikubwa.

MASHUKE

Mtu atatiwa moyo na wewe. Utakishinda kitu ambacho kilikuwa kikikupa stress. Mtu atarudisha kitu ambacho alikuazima bila hata kumwambia. Utasikia habari zitakazokufanya ufurahie siku zako zijazo tena.

MIZANI

Kitendo kidogo cha wema utakachokifanya kutoka kwako kitakupa malipo mazuri mara kumi. Kitu kuhusu mwonekano wako kitavuma, pongezi zinakuja. Ratiba yako itafunguka kwa njia ambayo itakupa uhuru zaidi.

NG'E

Suala la kifamilia litajisuluhisha bila hata kugombana. Utaalikwa mahali ambapo utawasiliana na mtu sahihi kwa wakati unaofaa. Kama umekuwa ukijihisi huonekani kwa watu, hiyo inakaribia kubadilika, tarajia pongezi, umakini (attention) wa ziada.

Hizi ni jumbe za jumla hivyo haziwezi kumhusu kila mtu kwa kila kinachotabiriwa hapa! Chukua kitakachokuhusu na uache ambacho hakikuhusu! Usilazimishe ujumbe ambao sio wa kwako utashindwa kuelewa wakati mwingine!
 
USOMAJI NYOTA JUMATATU 18/8/2025



NDOO

Kuwa na wasiwasi na familia yako. Marafiki zako watakuwa msaada wako sana, kuwa mwangalifu kuhusu kuwasahau au kuwapotezea kutokana na kuzama kimapenzi na mtu fulani. Malaika namba 333 au 777 kama njia ya kukuhakikishia kuwa kila kitu kitakuwa sawa.

MBUZI

Siri ya familia ambayo tayari unaishuku itafichuliwa. Simu isiyotarajiwa. Habari njema zinakuja. Kufikiria kitu kupita kiasi. Mambo kukuendea vizuri. Kusaidia mtu. Kila kitu kilichokusudiwa kukuvunja kimeshindwa. Una nguvu kuliko vile watu wanavyotaka uwe. Endelea kufanya mambo yako bila kujiona na hatia.

MSHALE

Mtu wa zamani ataangalia story yako unayopost mtandaoni au atawatuma baadhi ya marafiki zake kuangalia kwa ajili yake. Samaki anaanza ku move on, haoni sababu ya kuendelea kubaki. Kusikiliza podcast. 444.

NG'E

Kuona jina la mtu itakuwa ni ishara ya kuonekana kwake tena. Kufanya ununuzi wa mtandaoni kwa siku zijazo, hakikisha unaomba punguzo (discount) ili kuokoa pesa. Usijumuike na rafiki yako wa zamani karibu, hafai. 111.

MIZANI

Kubadilishana namba na mwanaume handsome. Mtu anavutiwa nawe na atakuambia. Samaki au Simba sio wa kwako huyo. Unahitaji kuwa na maamuzi zaidi juu ya hatua unayotaka kuchukua.

MASHUKE

Mtu atarudi kwa kukushanga, au kuku surprise. Mtu atakuomba utoke naye out, itakuwa nzuri sana isiyosahaulika. Kununua gel ya kuogea au serum. Mwanzo mpya kwenye mapenzi, uponyaji na furaha. 444.

SIMBA

Hujawahi kuwa na watu wenye bahati. Umekuwa na washiriki wa familia wenye sumu na wanyanyasaji, marafiki ambao wamekusaliti, urafiki au mahusiano ambayo huisha tu bila mpangilio, kuachika (kutodumu) kwenye mahusiano bila sababu. Mapenzi yamekuwa yakuzugwa tu kwako. Pata tiba kutoka mtaalam, kuna laana (nuksi).

KAA

Kuna uwezekano wa kuzama kimapenzi na Mshale. Unahitaji uachane na huyo Ndoo, Mapacha, au Mizani hafanyi bidii yoyote. Kutumia muda na marafiki zako. Watu wataomba msamaha kupitia ndoto.

MAPACHA

Mtu bado anahisi kuvunjwa moyo (heartbreaking) na wewe. Kupokea mawasiliano kabla ya siku yako ya kuzaliwa. Simba au Mizani atakuomba mtoke out kwenda kwenye date. Huyo Punda, Simba, au Mshale sio soulmate wako, ameshikwa sana na mambo mengine. 911.

NG'OMBE

Je, hayo yanatosha? ukiangalia maisha yako unafurahishwa na ulichofanikiwa? Kuna mengi zaidi. Umejikuna kadiri ya mkono wako ulipofikia, kuna mengi bado unataka kufanya lakini unahisi kukwama. Hali hii ya kukwama imeteketeza maisha yako kwa muda sasa na unaishiwa matumaini. Mambo hayajakuwa mazuri kwa muda mrefu na ukiangalia umekuwa ukipambana sana.

PUNDA

Katika miezi 3 ijayo utakuwa unavutia pesa nyingi sana. Utabukiwa (booking) na kuwa bize sana. Utakutana na mambo sahihi bila kutarajia. Kudhihirisha mwanzo mpya katika mapenzi, iwe na mtu mpya au wa zamani.

SAMAKI

Malengo mapya kuhusu kazi yako, ushindani, kuona nafasi ya kupanda na kupata vyeo. Kuwa mwangalifu kuhusu hali ya unywaji wa pombe. Kupata pesa bila mpangilio mtaani. Baraka za kifedha.

Kumbuka hizi ni jumbe za jumla hivyo haziwezi kumhusu kila mtu kwa kila kinachotabiriwa hapa! Chukua kitakachokuhusu na uache ambacho hakikuhusu+ Usilazimishe ujumbe ambao sio wa kwako utashindwa kuelewa wakati mwingine!
 
TAREHE YAKO YA KUZALIWA NA MAANA YAKE.

Hizi ni tabia za kilamtu kulingana na tarehe aliyo zaliwa kuanzia tarehe moja hadi 30. Terehe 31 tunaihesabu sawa na tarehe moja.

01. Mtu alie zaliwa tarehe 1 atakua ni mtu wa bahati sana na maisha yake ni marefu.

02. Mtu alie zaliwa tarehe 2 atakua na bahati ya kupata vitu kwa ulahisi pasipo kuhangaika.

3. Mtu alie zaliwa tarehe 3 atakua mtu wa kupendwa sana nawatu wenye uwezo.

4. Mtu alie zaliwa tarehe 4 atakua ni mtu wa kuugua ugua kila wakati na vifovyao ni vya gafla.

5. Mtu alie zaliwa tarehe 5 ndoto zake zitakua ni za ukweli lakini atakua muongo muongo.

6. Mtu alie zaliwa tarehe 6 atakua na maisha marefu na ni mwenye afya.

7. Mtu alie zaliwa tarehe 7 atakua na maisha marefu lakini atakua ni mtu wa misukosuko ya kila mara.

8. Mtu alie zaliwa tarehe 8 atakua ni mtu wa kubri yani kila atakacho kifanya anafanikiwa.

9. Mtu alie zaliwa tarehe 9 atakua na mafanikio na umri mrefu.

10. Mtu alie zaliwa tarehe 10 atakua na maisha marefu na mafanikio yake yatakua ni sehemu za mbali au afanye biashara ya kusafili.

11. Mtu alie zaliwa tarehe 11 atakua mchamungu.

12. Mtu alie zaliwa tarehe 12 atakua na maisha marefu kwa uwezo wa alie muumba.

13. Mtu alie zaliwa tarehe 13 ndoto zake malanyingi hutimia.

14. Mtu alie zaliwa tarehe 14 atakua mtu wa kusikilizwa na watu.

15. Mtu alie zaliwa tarehe 15 atakua ni mtu wa kupata ajali za mala kwa mala.

16. Mtu alie zaliwa tarehe 16 atakua ni mtu wa kupata mikosi mara kwa mara.

17. Mtu alie zaliwa tarehe 17 atakua mjinga mjinga au mpole kupita kiasi.

18. Mtu alie zaliwa tarehe 18 atakua na tabia ya udokozi au wizi.

19. Mtu alie zaliwa tarehe 19 atakua dhaifu dhaifu.

20. Mtu alie zaliwa tarehe 20 atakua muongo muongo na mfitinishaji wa watu na ukiwa na rafiki wa tarehe hii usimwambie silizako maana hataweza kuvumilia nayo ataisematuu hatakama utamkataza.

21. Mtu alie zaliwa tarehe 21 atakua na uwezo ki fedha na atakua na afya njema.

22. Mtu alie zaliwa tarehe 22 atakua ni mchamungu na atapendwa na watu na katika tarehe hii kama ni shekhe au ustadhi au mtu yeyote wa kuombea watu basi atakua na nguvu za uponyaji.

23. Mtu alie zaliwa tarehe 23 atakua na hasira sana na atasaliti familia, akitaka kuepukana na hilo ajitahidi kujizuia na hasira na atapenda kuishi mbali na familia yao au mikoa ya mbali au nchi za mbali.

24. Mtu alie zaliwa tarehe 24 atakua mkalimu sana na nimtu mwenye kupenda amani na asie penda kuonewa nayeye hapendi kuonea.

25. Mtu alie zaliwa tarehe 25 atakua na roho mbaya sana na hata akianzisha ugonvi nilazima atumie siraha na kujeruhi haoni kama ni vibaya.

26. Mtu alie zaliwa tarehe 26 atakua ni mtu wa kupendwa sana na watu na atafanikiwa katika maisha yake.

27. Mtu alie zaliwa tarehe 27 atapendwa sana na wanawake awe mwanaume au mwanamke na marafikizake watakua ni wanawake.

28. Mtu alie zaliwa tarehe 28 atapendwa sana na wazazi na watamtegemea kwa asilimia kubwa na atawasaidia.

29. Mtu alie zaliwa tarehe 29 ataishi katika maisha ya dhiki katika muda mfupi na atafanikiwa hadi kifo chake.

30. Mtu alie zaliwa tarehe 30 atakua ni mvumbuzi wa kuvumbua vitu kama vile sayansi, biashara, ufundi nk, na pia atakua na mafanikio makubwa.

Ukitaka kujua ukweli wa tarehe hizi angalia katika watoto ulio wazaa kwa tarehe zao na uangalie matendo wanayo yafanya utaamini na utamjua kila mtoto atakua na hulkagani katika maisha yake.
IMG-20250817-WA0140(2).jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom