Bajeti hii inaonekana ni ya kwenye vitabu tu. Nafikiri waziri ame copy na ku paste tu bajeti za nyuma. Utagundua kwamba vyanzo vya pato la taifa ni vilevile vya kila mwaka, nafikiri ingekuwa ni hekima waziri aeleze kwanza taifa lina hazina ya pato la taifa kiasi gani, na ili kutathmini vema bajeti kuna haja ya kila mtu kutambua kwanza utekelezaji wa bajeti ya 2011/2012 ilifanikiwa kwa kiasi gani. Bajeti hii inaonekana wazi si 'people centred' kwani bajeti inapozungumzia kilimo mara nyingi wanalengwa wale akina mfuko mkubwa, ni bajeti ya kundi dogo. Hai ainishi ni namna gnai malengo yatafikiwa na kwa vigezo vipi, hai ainishi hazina ina kiasi gani mpaka sasa. Imejikita katika utegemezi zaidi. Hakika tumejiendekeza sana. Kuomba omba hakutatuweka huru