USIWE NA TAMAA YA VITU VYA WATU

USIWE NA TAMAA YA VITU VYA WATU

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,599
Nimeona sehemu


UKUMBUSHO



Amekuomba urafiki facebook.

Umeangalia picha zake

Anaendesha Range

Anaonekana ni jamaa mwenye uwezo

Umemkubalia urafiki

Amekutumia text inbox

Umemjibu

Amekuomba out

Mkapanga kuonana

Ukajikwatua mwenyewe

Ukajipulizia na marashi ya kunukia vyema

Ukaweka na make-up na weave mpya.

Akakuchukua kwa ajili ya lunch Serena hotel

Akakuagizia na soft drinks

Mkawa na muda mzuri pamoja

Akakushika mkono

Akakufanya uwe unacheka muda wote kwa vituko vyake

Ukampenda

Ikawa kama umemjua kwa miaka
Akakuchukua kwenda kwake

Akaweka mazingira ya wewe kujisikia upo kwako kwa kukuruhusu ulale kitandani kwake

Akakubusu kimahaba

Ukapenda jinsi alivyo romantic, nguvu na ujasiri

Ukajisikia secure ukiwa nae

Ukajua kuwa unachoenda kufanya sio sahihi lakini ukajisikia poa tu

Ukamwambia atumie kinga, akakuambia it's too late.

Ukamkubalia na hukutaka kumsumbua.

Akakuambia anakupenda na hukusita kumwambia unampenda pia.

Baada ya kumaliza akafungua friji na kukunywesha maji ya kunywa.

Ukajihisi hapa mume nimepata

Ukajihisi ni mwanamke special

Atakuwa ndio yeye uliyekuwa ukimuota siku zote.

Ukavaa nguo.

Akakuchukua mpaka sehemu zinakopaki taxi

Akakubusu katika shavu.

Nimekuwa na muda mzuri na wewe akakueleza.

Akakupa Tsh 100,000.

Ukatabasamu na kumwambia nitakuona kesho.

Akabaki kimya.

Taxi uliyopanda ikaondoka

Ndani ya taxi hukuacha kutabasamu

Ukafika nyumbani kwenu na kumwandikia text watsapp kwamba umefika salama.

Yupo online lakini hakujibu text yako

Ukaamua kumtext tena, hakujibu!

Dakika chache baadae humuoni watsapp unaona kivuli tu.

AMEKUBLOCK!!

Siku, wiki, miezi ikapita ukaanza kujisikia homa homa, mchovu, uzito umepungua na utando mdomoni

Ukaenda kituo cha afya

Ukapima

Nusu saa baadae daktari anaingia.

Pole sana dada yangu daktari anakuambia.

Una maambukizi ya virusi vya UKIMWI na ni mjamzito vile vile.

Mimba, HIV+???? HOW??

Hauelewi

Inakuumiza sana, hauamini.

Unaenda nyumbani.

Ukiwa na hofu kubwa.

Unaona kifo hichi hapa

Unatazama angani, na unauona mwisho wako huu hapa.

Unajuta kumuamini mtu kirahisi hivyo

MWANAMKE ACHA KUTAMANI MATERIAL THINGS.

ISHI MAISHA YANAYOMPENDEZA MWENYEZI MUNGU PEKEE NA SIO BINADAMU.

*MWISHO*

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kutishia jamii, UKIMWI ni ugonjwa mgumu sana kuupata, sio kirahisi kama ulivoandika shenzi wewe
 
Nmetembea na wanawake wengi Sana....

Ila Mara zote
Linapokuja suala la matumizi ya CONDOM, Mimi ndo huwa muanzilishi.

Unatomasa jitu linaguna TU, hata haliulizi condom Iko wapi.

HUU UJINGA WA kumuamini kila mwanamme sijui wataachaga lini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom