Usiwe mwepesi wa kulaumu

Usiwe mwepesi wa kulaumu

Rich Woman

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2012
Posts
867
Reaction score
558
Wengi tumekua wepesi wa kulaumu hasa linapokuja swala la kutokuitwa kwenye usaili ilihali unaamini una vigezo vyote na wakati mwingine tumekua tukisema watu fulani wanapendelewa ila unapolaumu, je ni kweli ulifuata maelekezo yote uliyotakiwa kuyafuata kabla ya kutuma maombi ya kazi? au unalaumu tu ili uonekane umeeonewa.

Leo sekretariati ya ajira wamewatolea uvivu watu wasiokidhi vigezo na kulalamika hawaitwi kwenye usaili bahati nzuri walitoa kabisa na ushahidi ili kwamba kila mtu apate kujionea mambo ambayo huwa yanajitokeza huko.

Mfano mmojawapo: Zilitangazwa kazi za tutorial assistant na kuna mtu alikua anakidhi vigezo vyote ila alichokifanya sijui labda ungekeua wewe ungempa ajira

hii hapo chini ndiyo barua yake ya maombi ya kazi aliyoituma huko sekretariati

IMG_20140324_115131.jpg
IMG_20140324_115137.jpg alichokifanya ni kuhighlight sifa zote alizonazo hiyo ndiyo barua yake, na badala ya kuambatanisha passport size hapo chini kuna picha ambazo ndizo alizoambatanisha
IMG_20140324_115121.jpg
Mtu huyo ana shahada ya uzamili ila hicho ndicho alichotuma huko utumishi kweli mtu huyu asipoitwa kwenye usaili anamlaumu nani mimi nilifikiri labda mtu akiwa na shahada ya uzamili akili inakua inafikiri vizuri zaid ya yule mwenye shahada ya kwanza mtazamo wangu.

Kulingana na maelezo ya
sekretariati mtu huyo alipigiwa simu na kuulizwa kulikoni kutuma barua kama hiyo huyo mtu maelezo yake alisema kwamba barua yake ya maombi alimpa mpenzi wake amtumie na haakuituma yeye.

NB: Linapokuja swala la future yako usicheze nayo hata ukiwa una mambo mengi kiasi gani kwanini umuachie mtu akufanyie fanya mwenyewe sasa hapo hakuna ajuaye kama ni kweli alitumiwa na mpenzi wake au alituma mwenyewe.

Mifano iko mingi ila huo kwa leo unatosha

kabla hujalaumu hakikisha umefuata hatua zote ulizoagizwa kuzifuata sio unalaumu kumbe mambo uliyoyafanya sio basi jirekebishe maana mara nyingi watu wanaolaumu tu mara nyingi ukijaribu kufuatilia utagundua nyuma ya pazia kuna kitu japo wapo wanaolaumu na wana haki ya kufanya hivyo.

kila la heri katika michakato ya kutafuta kazi ila MAKE SURE YOUR HANDS ARE CLEAN BEFORE YOU POINT A FINGER.

hi barua ni kwamba alifanya kwa kutokujua au ndo makusudi mh kwa kweli inaonyesha tunalaumu ila wenyewe hatuwi makini huyo kavunja record what a shame
 
Baadhi ya watu hawapo makini hata chembe,kuna rafiki yangu nilimwambia aandike barua ya kuomba kujiunga na chuo kipitia pre entry programme, Fortunate nilimuomba anitumie then niiwasilishe kwa mkono,madudu aliyokuwa kaandika huwezi kuamini kuwa kamaliza kidato cha sita tena PCB,nilimuandikia upya,kahitimu 2yrs ago!
 
sasa hapo ndo najiuliza ina maana tatizo ni kiwango cha elimu yetu ya tanzania au tatizo ni mtu mwenyewe
 
hi barua ni kwamba alifanya kwa kutokujua au ndo makusudi mh kwa kweli inaonyesha tunalaumu ila wenyewe hatuwi makini huyo kavunja record what a shame

ndo hivyo kabla hujalaumu uwe na uhakika na ulichofanya mimi hata sijui alikua anawaza nini kutuma kitu kama hicho
 
Huyo alikuwa hana shida ya kazi na ndo maana alimpa mpenzi wake,kuna watu wanashida ya kazi na linapokuja suala la kupeleka barua wako makini lakini mwisho wa siku hawapati ili hali na vigezo wanavyo katika hili utumishi hawawezi kujivua eti kwa sababu ya huyo mmoja, hao hawakosekani katika jamiii na isiwe kigezo cha kuwaonea wengine kwa mgongo wa huyo mmoja wawe makini na kazi yao,na sisi waomba kazi tuhakikishe basi Cv zetu na barua za maombi zimeambatanishwa na vile vitu vinavyohitajika kuepusha sababu kama hizi tuwe makini,ni kweli wengine wanakosa kizembe kabisa lakini kuna wengine wako serious,wito wangu kwa utumishi watende haki ili watu wajilaumu wenyewe kwa uzembe
 
Hata wao wana mapungufu yao wala wasikatae ila wameona lawama zinakua nyingi kwao zaidi na wengine wamekua wanawafuata kulalamika kwanini hawaitwi kwenye usaili kwahiyo wakaona watoe baadhi ya sababu barua ziko nyingi nisingeweza kuweka zote hapa huo ni mfano mmoja tu.
 
Mastaz kweli? hata wa cheti anakuwa na nidhamu katika kutuma maombi aiseee,huwezi ukampa mpenzi wako kwanye issue sirias kama hizo huyo namsahuri arudie darasa tu!
 
Mastaz kweli? hata wa cheti anakuwa na nidhamu katika kutuma maombi aiseee,huwezi ukampa mpenzi wako kwanye issue sirias kama hizo huyo namsahuri arudie darasa tu!

Hapo aanza shahada ya kwanza au maana si mchezo kurudia darasa
 
Hapo aanza shahada ya kwanza au maana si mchezo kurudia darasa
Ikiwezekana aanze diploma kabisa maana huo ni ujinga wa hali ya juuu,Na hapo naamini elimu ya siku hizi ni ya kukalili mtu anakuwa na gpa kubwa lakini ujinga wenyewe ndo huuu sasa huyu ametofautiana na nini na wale 4m4 wanaochora mazombi kwenye mtihani? yaani picha anaambatanisha ya ngono? lol
 
kituko cha mwaka....
kwa mtin huu kazi kupata kwa kweli
 
siyo kweli huu ni mchezo tu, wameamua kuutunga na wala haiwezi kutokea hivi.
 
Sikuiona hii Rich Woman, pamoja na changamoto zingine za ajira lakini watu hawako makini kabisa wakati wanaandaa hivi vifurushi vya maombi ya kazi.

Nimebahatika kupitia barua za maombi za watu kadhaa, inachekesha kuamini kama hawa ndio wahitimu wa shahada... Hata ungekuwa wewe huwezi kumuita!
 
Last edited by a moderator:
hivi kwa nini watanzania hatuwi wakweli?

tungekuwa wakweli hapa tukaanza kupiga kura tukaulizana ni wangapi wako kwenye ajira walizojitafutia kwa kutumia vigezo vya elimu mngeona hali halisi.

inasikitisha mtu mwenyewe anakuwa kwenye ajira ambayo alibebwa na mtu fulani alimtafutia na yeye anatamani kupata ajira nzuri zaidi lakini yeye mwenyewe hawezi lafu anasimama kulaumu wanajamii wengine wasio na watu wa kubeba kwa maana ya kuwa na watu wanaowajua au kuwa na mvuto wa kimaumbile.

hapa tusidanyane ukweli ni kuwa hakuna sheria au mifumo inayowabana waajiri kuwa fare katika ajira na matokeo yake wanatumia nafasi hizo kupeana na matokeo yake hakuna nafasi yenye maslahi mazuri inayotolewa kwa uwezo wa mtu katika usaili.ila hilo haliwezi kumkatisha mtu akaacha kuomba.

wanatumia mifano kama hii kujiosha lakini ukweli unajulikana labda haya ukawaambie wa vijijini ambao hawako kwenye soko la ajira na kujua kinachoendelea

Hapo aanza shahada ya kwanza au maana si mchezo kurudia darasa
 
jokes! uyo jamaa alifanya makusudi ni sawa na mwanafunz aliyeandika verse badala ya kujibu mtihani, mbona uozo wenu amuwek hapa.... na tutaaminije kama ni kwel au imetengenezwa ili kujisafisha! tUKUBALI UKWEL UONEVU NDO MANA MTU AD ANAAMUA KUTUMA MAOMBI AKIWA HANA IMAN KUWA ANAWEZA PATA NDO MAANA KAMA NI KWEL ANAFANYA UKICHAA WA NAMNA HIYO... sina hakika kwamba elimu yetu ya tz ni poor kwawba watu hawajui namna ya kuandika cover letter,! bali wamechoka na manyanyaso ya ajira! ni wakat wa kubadirika watz turud ya mwaka 1980's hali ya urushwa haikuwepo ndugu zangu saiz had kupata msaada pccb unatoa rushwa sasa nani mkomboz wa raia?
 
Daah! mbona inasikitisha sana embu watanzania tubadilike mtu kama uyo ilibidi kwanza achukuliwe atua za kinidhamu tena kali maana analeta mchezo wa madangi kwenye mambo seriously kwanza ukute mtu kama uyo wala hana nia ya kazi ukute mtu kama uyo ndugu zake wana mikampuni kibao wala haitaji kaz, kama unaona auna shida ya kazi basi acha kuwazibia riziki wengine kuna watanzania kibao wana njaa ya kazi si vzur kabisa kuleta masiala kwenye maali ambapo si maali pake, kingine watu wengi sana wanapoomba kazi utumishi wanashindwa kutekeleza jambo moja ambalo ni kujaza nafasi husika ya nafasi uliyoomba pale juu ya baasha ni muimu kufanya au kutekeleza mambo madogo madogo kama hayo kinyume na hapo lawama nyingi ambazo hazina msingi tujitaidi tuwe makini jaman.
 
Hiyo barua ni very extreme mpaka najiuliza kama ndo sample halisi ya maombi mengi yanayokataliwa.

Pia na hao Sekretariati wasijikoshe maana na tangazo lao la kazi ni shida tupu.
 
Hiyo barua ni very extreme mpaka najiuliza kama ndo sample halisi ya maombi mengi yanayokataliwa.

Pia na hao Sekretariati wasijikoshe maana na tangazo lao la kazi ni shida tupu.

Kwakweli secretariat nao wana mapungufu yao na wengi tunayafahamu ila hizo ni harakati za kutaka kueleimisha hiyo jamii ya waomba kazi, mimi na wewe hatujui ni kwanini maombi mengi yanakataliwa
 
jokes! uyo jamaa alifanya makusudi ni sawa na mwanafunz aliyeandika verse badala ya kujibu mtihani, mbona uozo wenu amuwek hapa.... na tutaaminije kama ni kwel au imetengenezwa ili kujisafisha! tUKUBALI UKWEL UONEVU NDO MANA MTU AD ANAAMUA KUTUMA MAOMBI AKIWA HANA IMAN KUWA ANAWEZA PATA NDO MAANA KAMA NI KWEL ANAFANYA UKICHAA WA NAMNA HIYO... sina hakika kwamba elimu yetu ya tz ni poor kwawba watu hawajui namna ya kuandika cover letter,! bali wamechoka na manyanyaso ya ajira! ni wakat wa kubadirika watz turud ya mwaka 1980's hali ya urushwa haikuwepo ndugu zangu saiz had kupata msaada pccb unatoa rushwa sasa nani mkomboz wa raia?

Boi unajua hesabu za makadirio?

Wimbi la wataka kazi ni kubwa sana kuliko ajira ambazo Serikali inaweza kutoa kwa hiyo usishangae ukaomba kila siku, kila mwaka na bado ukakosa.

Huwezi kutetea ukichaa kwa kigezo cha uonevu aisee, maana yake ni kuwa huyu mtu akiajiriwa wakimtibua tu kidogo kazi hazifanyiki, sio?

Sijui hasa ubora wa elimu yetu, lakini ukweli ni kuwa watu hawajui kuandika 'kava leta' bila kujali elimu yao, ushahidi mdogo ni hata uandishi wao wa mtandaoni na SMS, chunguza vema.

Kingine ni uvivu wa kusaka fursa mkuu, fikiria CV mtu anaomba template afanye kuhariri tu, barua za kazi hivyo hivyo na kadhalika. Inakuwaje kama huyu unaemuomba akutumie mfano wa barua wewe ujaze taarifa zako tu anakuwa amekosea, na wewe unakosea automatikale...

Kingine kinachoonesha uvivu ni kale kamtindo ka nisaidie kupost, kuna watu kadha niliwaonesha fursa, anakuambia ukiandika barua muandikie na yeye, si umburula huu kaka? Mtu ambae kazi ndio mkombozi wake anataka kijana mwenzake umfanyie harakati.

Ukishaona dalili kama hizi jiulize hao watu wana kiwango gani cha kujitoa na kufanya kweli harakati za kusaka kazi... Kumbuka harakati za kutafuta kibarua haziishi kwenye kuandika maombi ya kazi na kungoja kuitwa usaili pekee, ni jambo pana na mtambuka!
 
Back
Top Bottom