Mphamvu
JF-Expert Member
- Jan 28, 2011
- 10,702
- 3,345
Hiyo barua ni very extreme mpaka najiuliza kama ndo sample halisi ya maombi mengi yanayokataliwa.
Pia na hao Sekretariati wasijikoshe maana na tangazo lao la kazi ni shida tupu.
Sekretarieti wasijikoshe, lakini uongo ukisemwa sana unakuwa ukweli na wana haki ya kujisafisha.
Mkuu makosa ya kufuata maelekezo ni mengi sana kwenye barua za maombi, kuanzia uambatanishaji wa nyaraka, muundo wa barua yenyewe, na wakati mwingine hata anuani.
Jamaa wanaoajiri wanazingatia kigezo kuwa kushindwa kufuata maelekezo madogo ya ukurasa mmoja ni udhaifu mkubwa kwa muombaji wa kazi na zaidi unaonesha kuwa hukuwa makini/ulipuuzia mchakato wao, kwanini wakuamini na kukupa kazi?
NB: Wametoa mfano extreme ili na sisi tuone ukubwa wa shida yenyewe, wangetoa kigezo cha kukosea anuani au kuambatanisha nyaraka ungesema wanakompliketi, mbona tatizo lenyewe dogo hilo?