Kuna somo kubwa sana ambalo kila mfanyabiashara anapaswa kujifunza.
Kuna mtu aliwahi kuwa na biashara iliyokuwa inafanya vizuri sana. Wateja walikuwa wanaingia dukani kila siku, bidhaa zilikuwepo, huduma ilikuwa nzuri na biashara ilikuwa inampa kipato cha kutosha.
Lakini kadiri muda ulivyoenda, alianza kupoteza mwelekeo. Pombe ikawa sehemu kubwa ya maisha yake yeye muda wote kalewa anatoa huduma huku kalewa kinywa na macho maziyo sauti ya pombe kwa wateja hana weekend muda wote analewa tena maeneo ya ofisi kuna pub, akatumia muda mwingi kufanya starehe na mahusiano ya kimapenzi na kila mwanamke anaepita mbele yake na hata baadhi ya wafanya biashara wenzake alikuwa anwatongoza wengine anawagongea nyuma ya frame, milimani n.k hii nolipata kwa sababu pia mimi nilikuwa mtu wake wa karibu kwakuwa na mimi nilikuwa nafanya biashara hiyo hiyo maeneo hayo na tulikuwa tunapiga story sana mida ambayo hakuna wateja. Nilimwambia acha pombe mida ya kazi atleast kunywa werkend au ukienda kwako alinitusi kwa mara ya kwanza ushikaji ukafa.
Sasa akapata demu mwingine Mbaye amemfanya mke mahusiano yao mpaka dukani wanakaa hovyo kama wako chumbani unakuta mchizi kalewa na mkewe huyo ni mkevi ni aina ya wanawake wanao adapt tabia za waume wao yaani anamuhudumia pombe kama ndo barmaid, anafata vidungura, mara bia mara pombe kupima n k, hali ya biashara ikawa mbaya. Bidhaa ambazo wateja walikuwa wanazipata kwa urahisi zikaanza kukosekana. Duka likawa linafunguliwa bila mpangilio, wakati mwingine mwenye biashara analiacha wateja wakija yete hayupo kamwacha demu wake hapo hata hajui kuhudumia kila anaeenda anaamviwa hiyo haipo au subiri nimpigie mshikaji, sasa hivi wateja hawapo ni kama walianza kuondoka taratibu.
Wale waliokuwa wanamtegemea kwa oda wakaanza kutafuta huduma sehemu nyingine na wengine kwangu. Biashara iliyokuwa na wateja wengi ikaanza kupoteza mvuto, mapato yakashuka na hatimaye mwenye biashara akaanza kukabiliwa na msongo wa mawazo kutokana na hali aliyojikuta nayo sikuhizi kawa mnyonge analewa zaidi ikifika saa 1. ameanzavkuuza tuvitu tudogo tudogo tusitokuwa na faida ni kama mfanya biashara mkubwa alieyefirisika ila hataki kuamini kafurisika.
Biashara nyingi hazifi kwa sababu ya kukosa mtaji pekee. Nyingine hufa kwa sababu ya kukosa nidhamu, usimamizi na uwajibikaji wa mwenyewe.
Kuwa na biashara inayopata faida hakumaanishi umefanikiwa milele. Mafanikio yanahitaji kulindwa kila siku.
Kama wewe ni mfanyabiashara, kumbuka mambo haya:
✅ Linda muda wako. Usiruhusu starehe zikufanye usahau majukumu yako.
✅ Simamia biashara yako. Jua bidhaa ulizonazo, zilizoisha, mapato, matumizi na mahitaji ya wateja wako.
✅ Wathamini wateja wako. Mteja akizoea kukosa huduma kwako, atatafuta huduma hiyo sehemu nyingine.
✅ Tenganisha biashara na maisha binafsi. Mahusiano yako yasiharibu maamuzi yako, muda wako au mtaji wa biashara yako.
✅ Epuka tabia zinazoharibu maisha yako. Pombe ikizidi na kuanza kuathiri kazi, fedha na majukumu yako, kubali tatizo na tafuta msaada.
✅ Usisubiri mpaka biashara ife ndipo uamke. Ukiona mauzo yanashuka, bidhaa hazipatikani na wateja wanapungua, tafuta chanzo cha tatizo na chukua hatua mapema.
Kumbuka, biashara haijengwi kwa mtaji pekee. Inajengwa kwa nidhamu, uvumilivu, uaminifu, huduma bora na maamuzi sahihi.