Usitoe huduma kwa upendeleo

Usitoe huduma kwa upendeleo

Mangwea1900

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2025
Posts
2,485
Reaction score
3,224
Hali ya ubaguzi na upendeleo katika kila ofisi kuanzia zile za dini, binafsi hata serikali ni kubwa sana.
Bila kujulikana au rushwa hupewi huduma Bora zaidi utatoka ukiwa una huzuni na wakati mwingine machozi.
Jana nilimwona Mzee mmoja akifurahia alivyopewa huduma nzuri katika banda la RITA katika uwanja wa maonyesho ya sabasaba. Mzee huyu uso wake ulionyesha furaha isiyo kifani.
RAI YANGU; Watoa huduma mahala popote, viongozi mahala popote mlipo katika ngazi zozote toeni huduma pasipo upendeleo wala kwa nguvu ya rushwa. Sisi ni watoto wa baba mmoja na siku mmoja tutarudi kwake kutoa hesabu ya kila tulichofanya kwa kadiri ya ukubwa wa dhamana uliyopewa. Ni kweli machozi ya samaki huenda na maji lakini kumbuka yupo mmiliki wa maji atayaona machozi hayo. Tupendane, tujaliane na tusitiriane ni kitambo kidogo tutarudi kwa baba yetu.
 
Natamani wangekusikia ,ishakuwa kero kubwa.
Watu hawana tena hofu na Mungu.
 
Hali ni mbaya sana.

Rushwa imekuwa sio jambo la aibu tena kwa wafanyakazi wengi.
 
Back
Top Bottom