Usitamani mali ya mtu mwingine au kitu chochote

Usitamani mali ya mtu mwingine au kitu chochote

Kingsharon92

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2015
Posts
8,588
Reaction score
12,359
Nawasalimu kwa jina la aliye juu Natumai mu wazima buheri wa afya
Nianze kwa kusema binadamu tumekuwa na matamanio ya mafanikio
Au ya wengine bila kujua hapo walipo
Wamefikaje

1. Marekani ni taifa kubwa sana duniani likiwa na ukwasi wa kutosha kila nyanja sasa imekuwa ni kama. Kasumba kwa watanzania tulio wengi tunatamani kufikia rank ya USA bila kujua yeye kafikaje hapo utatukuta tuko vijiwen tunadanganyana eti democracy ya Marekani hivi kweli

Unajua historia ya USA? Wako hapo kwa gharama kubwa sana wamemwaga Damu wa me dhulma roho za watu wameiba mali za mataifa mengine na wanalinda maslahi yao kwa gharama yoyote ile mpaka leo hii wanalinda taifa lao kwa jasho na Damu halafu wewe mtanzania unataka ulingane na usa kwa kupiga porojo tu ili hali hauko tayari kumwaga hata Damu acha tamaa

2. utakuta mtu anatamani kuwa kama mkuu wa mkoa wa dar wewe unajua mwenzio kapitia mangapi kufika hapo katukanwa kadhalilishwa kavumilia mengi halafu wewe na vyeti vyako unataka short cut acha tamaa kuna watu wana pesa halafu wewe unatamani kuwa kama wao wewe kuna wenzio wameua wamedhulumu wanalala chini walishinda kwa waganga usiku na mchana halafu wewe kiwepesi wepesi tu unataka ulingane nao acha tamaa maana hujui namna ya kufika hapo na usiiige njia aliyotumia fulani kufika rank fulani na wewe ukataka upite huko utashindwa tengeneza mfumo wako na wewe wa kutokea
 
Kikubwa hapa ni Kuwa duniani hamna short cut lazima u struggle kwa jasho hata na damu ndo mana inashauriwa tusione mtu kafika sehemu alipo Ila tukiuliza historia yake alipitia mengi na magumu sana. Bora kutamani Kuwa version yako mwenyewe na mapito yako Ili ufike sehemu. Hata matajiri wakubwa wa USA ukisoma historia yao walianzia chini wakakua step by step, hata ukimsoma Dr Benson Carson hakika historia yake inafunza mengi. Only in Africa tunaamini kwenye short cut kufikia malengo
 
Mkuu unakuta mtu anatamani mambo ya watu bila kujua nyuma ya mafanikio alipo katumia gharama kubwa sana
 
Mkuu unakuta mtu anatamani mambo ya watu bila kujua nyuma ya mafanikio alipo katumia gharama kubwa sana
Ni kweli aisee watu hutaka Kuwa ka flani ukiwauliza unawaza ku pay price ya huyo mtu aliyotumia kufika alipo jibu inakuwa hamna. Na sema huku kwetu watu hawasomi vtabu wangejifunza. In my life napenda nifanikiwe in my own ways na sio kumuiga flani, kila mtu na mapito yake
 
Wewe umegeneralize hii term tamaa.

Kuna tamaa njema ns tamaa ovu. Kutamani cha mtu ni sunna.
Bila kutamani basi tusingekuwa tunazaliana na kuongezeka.

Pia bila kutamani vya wengine hauwezi kuendelea.

Tamaa isiyofaa ni ile tamaa ovu, kama vile wizi na husda.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom