Usitafute pesa kwaajili ya kujenga bali ongeza vyazo vya mapato kwanza

Umuhimu wa nyumba ni mkubwa lakini unaijengajengaje ikiwa fendha yenyewe haina uhakika?! Bora kuwa na kiwanja kisha kuanzisha mradi utakaokuwezesha kuijenga hiyo nyumba kwa awamu hata kama utaijenga kwa miaka mitatu na zaidi.
 
Haya mambo ni kama kubahatisha, unaweza kuchagua kufanya moja kati ya hayo na ukaona matunda yake, au ikawa kinyume chake.

Wangapi wanaanzisha biashara na zinaanguka?
Kila sehemu utakayo amua kuiendea lazima ukutane na changamoto zake. Ni vizuri kuwa na taarifa sahihi katika kila unachotaka kukifanya, huu utakuwa ni mwanzo tu katika safari ya kuyaendea mafanikio yako katika hilo utakalokuwa umelichagua
 
Wazo ni zuri japo kwa upande wangu naona kama limeegamia zaidi kwenye nidhamu ya woga. Umuhimu wa nyumba upo palepale lakini huwezi kula hiyo nyumba! Ni vyema zaidi ukatafuta namna ya kuzalisha ili iwezeshe kujenga hiyo nyumba. Watu hutofautiana namna ya kufikiri na mitazamo pia, kwa mtu asiyepata dira ya kuongeza kipato chake ni bora akajihami kwa kufanya huo ujenzi.
 
Mimi katika utafiti wangu nikipanda daladala vyanzo vya kupata mtonyo vinakata mbaya sana, ila nikisanuka na ndinga langu yaani mapene yanatiririka, wajuvi ndio kusema nikipanda gari naruka viunzi vingi vya nuksi au......mshana jr naomba unisaidie
 
binafsi sijawahi ona mtu akaanza nunua gari akashindwa jenga nyumba
anyway kila mtu na kipaumbele chake
Sure Mkuu, kabla sijanunua gari nilikuwa najua sitaweza kujenga, ila baada ya kuwa na gari nikaona kila jambo linawezekana, inategemea inaitumiaje nguvu yako ya akili
 
Ujenzi wa nyumba hauishagi.
Hili nalo naona lilisahaulika! Nina rafiki yangu tangu nafahamiana naye sasa ni miaka 14, mpaka sasa bado anajenga tu nyumba yake (anafanyia maboresho) hii imenifanya kichwa kisiniume sana kuhusu kujenga ila nitajenga tu kwa wakati niaouona unanifaa zaidi. Mwingine namjua tangu mwaka 1994, ndiyo sasa hivi amemalizia kujenga lakini uzio bado hajaufanyia finishing anayoitaka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…