Usitafute pesa kwaajili ya kujenga bali ongeza vyazo vya mapato kwanza

Haya mambo ni magumu kuyashauri jamani inategemea na interest za mtu na maisha aliyomo pia, mleta uzi unaweza kuwa sahihi kwa upande mwingine usiwe sahii ila inategemea na mtu, kwani hata historia zetu ziko tofauti, ila nyumba ni muhimu hata kabla sijawa na chochote kile.
Umuhimu wa nyumba ni mkubwa lakini unaijengajengaje ikiwa fendha yenyewe haina uhakika?! Bora kuwa na kiwanja kisha kuanzisha mradi utakaokuwezesha kuijenga hiyo nyumba kwa awamu hata kama utaijenga kwa miaka mitatu na zaidi.
 
Haya mambo ni kama kubahatisha, unaweza kuchagua kufanya moja kati ya hayo na ukaona matunda yake, au ikawa kinyume chake.

Wangapi wanaanzisha biashara na zinaanguka?
Kila sehemu utakayo amua kuiendea lazima ukutane na changamoto zake. Ni vizuri kuwa na taarifa sahihi katika kila unachotaka kukifanya, huu utakuwa ni mwanzo tu katika safari ya kuyaendea mafanikio yako katika hilo utakalokuwa umelichagua
 
Acha kupotosha umma...... Kama unauwezo wa kujenga ni bora ukajenga kwanza sababu
1. Nyumba ni asset ambayo value yake inaongezeka kadiri muda unavyokwenda.

2.Nyumba unaweza kuitumia kama dhamana ili upate pesa ya kuweza kukuza mtaji au kuongeza vyanzo vya kipato chako.

3. Kwa hali ya kichumi ya sasa unapoanzisha chanzo kipya cha kipato ni kama kutake risk, mazingira si mazuri na nirahisi kupoteza kuliko kuongeza, hivyo kama hela yako si endelevu basi ni bora ukawekeza kwenye kitu chenye uhakika ambacho kitaonekana kuliko kucheza pata potea.

4.Ukiwa na nyumba unakuwa na aman, hata Ukitoka kutafuta umepata au hujapata ila unajua jioni unarudi kwako ambapo hakuna atakaekubuguzi.

5.Ukiwa na nyumba inakuongezea confidence, unakuwa unajiamini, unaweza kufanya unachotaka kwenye eneo lako, tofauti ukiwa nyumba ya kupanga lazima uombe ridhaa ya mwenye nyumba, hata hitilafu ya umeme huwez ita fundi bila kuwasiliana na mwenye nyumba .

6. Nyumba ni security ya maisha yako, hata mambo yakiyumba inaweza kukusitiri badae, tofauti na biashara ambayo haitabiriki... Mda wowote inaweza kufa.

Points zipo nyingi.... Ila kwa hizo chache mkuu natumai nimekuonesha kuwa kujenga ni muhimu sana kuliko kuongeza chanzo cha mapato... Hasa kama hela yako si endelevu..
Wazo ni zuri japo kwa upande wangu naona kama limeegamia zaidi kwenye nidhamu ya woga. Umuhimu wa nyumba upo palepale lakini huwezi kula hiyo nyumba! Ni vyema zaidi ukatafuta namna ya kuzalisha ili iwezeshe kujenga hiyo nyumba. Watu hutofautiana namna ya kufikiri na mitazamo pia, kwa mtu asiyepata dira ya kuongeza kipato chake ni bora akajihami kwa kufanya huo ujenzi.
 
Mimi katika utafiti wangu nikipanda daladala vyanzo vya kupata mtonyo vinakata mbaya sana, ila nikisanuka na ndinga langu yaani mapene yanatiririka, wajuvi ndio kusema nikipanda gari naruka viunzi vingi vya nuksi au......mshana jr naomba unisaidie
 
binafsi sijawahi ona mtu akaanza nunua gari akashindwa jenga nyumba
anyway kila mtu na kipaumbele chake
Sure Mkuu, kabla sijanunua gari nilikuwa najua sitaweza kujenga, ila baada ya kuwa na gari nikaona kila jambo linawezekana, inategemea inaitumiaje nguvu yako ya akili
 
Ujenzi wa nyumba hauishagi.
Hili nalo naona lilisahaulika! Nina rafiki yangu tangu nafahamiana naye sasa ni miaka 14, mpaka sasa bado anajenga tu nyumba yake (anafanyia maboresho) hii imenifanya kichwa kisiniume sana kuhusu kujenga ila nitajenga tu kwa wakati niaouona unanifaa zaidi. Mwingine namjua tangu mwaka 1994, ndiyo sasa hivi amemalizia kujenga lakini uzio bado hajaufanyia finishing anayoitaka.
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom