Usiseme Hujaonywa!!

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Kwenye familia nyingi (mimi nazifahamu tano) watoto wasipoangaliwa kwa ukaribu wanaweza kuwa na Mahusiano ya kingono bila wazazi wao kufahamu au kuja kufahamu wakati yule wa kike atakapopata ujauzito. Mfano mmoja ni Professa Mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambaye alipokuwa kwenye umri wa kubalehe (teen age) alingonoka na dada yake kwa bahati mbaya dada yake akapata ujauzito. Mtoto aliyezaliwa yuko hai mpaka sasa naye ana familia yake.

Kama tukichukulia kwamba mambo ni salama kwa sababu wazazi tunataka yawe salama, basi tunajidanganya sana na ukweli uko mbali nasi. Watoto wanatakiwa waangaliwe kwa karibu sana na wafunzwe nini halali na si halali kwenye mahusiano ya kingono. Mafunzo haya zamani yaliyotolewa kwenye Unyago na Jando lakini kwa sasa ni wajibu wetu wazazi kuwafunza wanetu nini cha kufanya wanapokutana na changamoto hizi za mabadiliko ya miili yao.

Jambo la pili ni mahusiano kati ya mashemeji kwenye majumba yetu. Ni kweli kwamba ni vizuri ukakaa na mdogo wako wa kiume au wa kike nyumbani kwako. Lakini imethibitika kwamba ukaaji wao usipodhibitwa wana madhara makubwa sana kwenye ndoa za ndugu zao.

Tofauti kati ya ndugu wa kike na wa kiume inakuja pale ndugu wa kiume anapotembea na mkeo ni vigumu sana kuonyesha na atajitahidi kuficha matendo yake ya kungonoka na shemejie. Lakini ndugu wa kike akitembea na mumeo basi inawezekana kabisa ukajua (kama jamaa naye kalewa kwa penzi la shemejie) kutokana na matendo ya mdogo wako au ya mumeo.

Haya mambo ya wana ndugu kungonoka yanatokea sana na hili la mashemeji kuingilia ndoa za ndugu zao lipo kwa sana tu. Kinachotakiwa sisi kama binadamu tuukubali ukweli huu na kujitahidi kuishi nao bila ya kuleta madhara kwetu.

USISEME HUJAONYWA!!
 
asante kwa ushauri....

Kingine hata ndugu tunaoishi naotuwe nao makini kwa watoto wetu, ndo hao hao wanaobaka na kuabuse watoto......
 
Tafiti zinaonyesha kwamba wasichana wengi kubikiriwa kwao au kunajisiwa kwa watoto wa kiume kunafanywa na ndugu wa karibu au na marafiki wanaoaminiwa na wazazi wa watoto husika!!
 
Hili halina Ubishi.

Ninafahamu watu waliozaliwa baba na mama mmoja na sasa wanaishi kama mume na mke na wana watoto watatu

Hawa ilikua ni Geti kali, Dada ni mkubwa kuliko kaka

( Kigarama umenena )
 
Kwenye familia nyingi (mimi nazifahamu tano) watoto wasipoangaliwa kwa ukaribu wanaweza kuwa na Mahusiano ya kingono bila wazazi wao kufahamu au kuja kufahamu wakati yule wa kike atakapopata ujauzito. Mfano mmoja ni Professa Mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam ambaye alipokuwa kwenye umri wa kubalehe (teen age) alingonoka na dada yake kwa bahati mbaya dada yake akapata ujauzito. Mtoto aliyezaliwa yuko hai mpaka sasa naye ana familia yake.

Kama tukichukulia kwamba mambo ni salama kwa sababu wazazi tunataka yawe salama, basi tunajidanganya sana na ukweli uko mbali nasi. Watoto wanatakiwa waangaliwe kwa karibu sana na wafunzwe nini halali na si halali kwenye mahusiano ya kingono. Mafunzo haya zamani yaliyotolewa kwenye Unyago na Jando lakini kwa sasa ni wajibu wetu wazazi kuwafunza wanetu nini cha kufanya wanapokutana na changamoto hizi za mabadiliko ya miili yao.

Jambo la pili ni mahusiano kati ya mashemeji kwenye majumba yetu. Ni kweli kwamba ni vizuri ukakaa na mdogo wako wa kiume au wa kike nyumbani kwako. Lakini imethibitika kwamba ukaaji wao usipodhibitwa wana madhara makubwa sana kwenye ndoa za ndugu zao.

Tofauti kati ya ndugu wa kike na wa kiume inakuja pale ndugu wa kiume anapotembea na mkeo ni vigumu sana kuonyesha na atajitahidi kuficha matendo yake ya kungonoka na shemejie. Lakini ndugu wa kike akitembea na mumeo basi inawezekana kabisa ukajua (kama jamaa naye kalewa kwa penzi la shemejie) kutokana na matendo ya mdogo wako au ya mumeo.

Haya mambo ya wana ndugu kungonoka yanatokea sana na hili la mashemeji kuingilia ndoa za ndugu zao lipo kwa sana tu. Kinachotakiwa sisi kama binadamu tuukubali ukweli huu na kujitahidi kuishi nao bila ya kuleta madhara kwetu.

USISEME HUJAONYWA!!
Maharibiko!
 
mtu ni shemeji yako tena mke wa Kaka yako, unangoja nikitoka ahumbani unaingia kama kwako paaa!-John Walker
 
mh! baada ya mwaka mmoja na nusu bila kuliona jamvi, sasa mida hii naingia tu unanipa kubwa hivo? kwa heri mpendwa
 
Pole, ningejua kama unapita huku ningekuzuia usiingie humu. Hata hivyo karibu sana Jamvini!!
 
Back
Top Bottom