Usiri wa Maalim Seif, Karume Jr. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usiri wa Maalim Seif, Karume Jr.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by The Prophet, Apr 28, 2011.

 1. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  "......kama baadhi ya watu wanavyohoji chimbuko la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kati ya Julius Nyerere na Abeid Karume ndivyo leo watu wanavyotaka kujua ni makubaliano gani yaliyofikiwa kati ya Rais Karume na Katibu Mkuu wa CUF Maalim Seif Sharif Hamad walipokutana Ikulu. Ukiacha mbali wawili hao hakuna mwingine anayejua kile hasa kilichozungumzwa na kusababisha kuanza kwa mchakato wa kuisaka Serikali ya Umoja wa Kitaifa...."

  Tayari Mwakilishi wa Jimbo la Mkwajuni, Mbarouk Wadi Mtando(CCM) ametaka apewe ufafanuzi na SMZ kupitia Baraza la Wawakilishi kilichopita, pale alipotaka kujua iwapo maridhiano hayo yameandikwa katika kabrasha maalumu kama kumbukumbu au la.  ....akijibu swali hilo, Waziri wa Katiba na Sheria, Aboubakary Khamis Bakari(CUF) alisema makubaliano hayo hayakuandikwa katika kabrasha na kwamba yalikuwa yamelenga kutanguliza mbele maslahi ya Zanzibar kama taifa.

  my take:
  Jibu la Waziri ni la kushangaza. Karne ya 21 bado kuna watu, tena executives, wanafanya mambo makubwa kama haya bila maandishi? Bila kumbukumbu?

  source: RAI
   
 2. jouneGwalu

  jouneGwalu JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 2,680
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  Bado tunasiasa za mazoea, unafiki, kuogopana na kulindana.
  Tuna siasa nyepesi sana.
  suala la nchi kufanyiwa chumbani!
   
 3. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Alishasema Mwalimu, ukidhani Muungano ni mbaya, jaribu kujitenga. Ukitadhani elimu ni aghali jaribu ujinga.

  Watanganyika ni watu wa ajabu sana. Wanaridhika na kuendelea mbele kiulaini sana, bora tu wapuuze kinachotokea. Lakini siku wakijaamua hapo ndipo ya chuya yatakapojulikana. Simba mwenda kimya sio gonjwa siku zote. Ngoja tuendelee kujichubua magamba tukidhani tutamaliza matatizo bila kugusa maini.
   
 4. n

  ngwendu JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Jun 7, 2010
  Messages: 1,967
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Tunajua yamewauma sana kuona sasa hivi zanzibar kuko shwari na kinyume chake (mlifurahi sana kuona zanzibar wakiishi kwa kuuana wenyewe) sasa wanajua mchawi wao. yawe yameandikwa au yasiwe haijalishi what we want is peace for our people. Period.
   
 5. m

  mkulimamwema Senior Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 14, 2011
  Messages: 153
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naye Maalim mroho wa madaraka watu wangapi waliumia au kupoteza maisha kwa kumuunga mkono leo hii anakaribia kuingia ikulu anadanganywa kirahisi hebu tutumie elimu vizuri wanafanya mambo pasipo kuandika ukitapeliwa kisa makamu wa kwanza wa Rais
   
 6. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Langu jicho tu. Mie napita njia.
   
 7. Pepombili

  Pepombili JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Dec 20, 2010
  Messages: 439
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Usipate shida kwa hilo sio kila mkitu kuandikiana lazima ufike wakati watu wawe wanaaminiana bila ya maandishi, kwani kuna maandishi mamngapi yameandikwa na watu hawayafuati maana damu wameminiana yatosha wacha tuvuke hili kwanza maandishi baadae
   
 8. M

  Mkulima1 New Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu zanguni tunatakiwa tuwe na upeo wa kufikiria. yale mazungumzo yaliokuwa kati ya Maalim Seif na Amani Karume. yalikuwa sio mazungumzo ya maandishi kwa sababu yalikuwa yanalenga kuleta amani Zanzibar na kuachana na Siasa za chuki.

  Mazungumzo yale yalikuwa ni mzungumzo pia ya kuunda serikali ya kitaifa. so kama serikali ya kitaifa imeundwa hapa ndio wajibu wetu sisi kupigania kuwa katiba yetu lazima ikubaliane na suala hili. na chengine lazima tukubali kuwa Tume ya chaguzi iwe tume huru na iundwe nyingine. hapa sasa ndio kalamu ya maandishi inafanya kazi. ila kwa pale mwanzi maalim seif asingeweza kufanya vile kwa kuwa anawapenda ndugu zake na njia ya kufanikiwa iko pale pale....la muhimu sasa ni kumsaporrt mara mbili ya hapo ili kuweza kuleta mapinduzi zaidi.....!
   
Loading...