Usipunjwe tena nyama buchani

Mtaanza kugombana na Mangi kama zile lisiti za TRA,sasa ukute Mangi kapiga viloba duu kaz kwel
 
wacha waibe...
kama kuna watu wanalipwa hadi mshahara kwa kazi iyo wenyewe wanaishia kukaa ofisin tu
wacha watuibie hadi tunyooke
 
Yaani mdau umenena vyema siku hizi ukinunua nyama nusu utafikiria robo ukinunua kilo ndio kabisaa unapewa nusu na robo wala haifiki vizuri sana sana bucha za uswazi na baadhi ya mabucha ya mjini
 
Mie Enzi zangu nilikuwa nayapunguza Yale Mawe ya kupimia kwa kutumia 'Tupa' ya kunolea Visu, zile angle zote nazifanya zinakuwa round, kwny kg moja na punguza gram Kama Mia mbili hivi pia kwny Bakuli lile la kupimia natafuta lile zito la shaba.

Yale Mawe na Bakuli la Serikali nayahifadhi sehemu mpaka nikihamishwa ndo nayarudisha na kuhamia kwny Butcher jipya na kuendelea kutengeneza ngawira. Kweli Old is Gold

Kwny Kupima mbele ya Mteja najifanya niko fair.

It was 1970s Wakati huo Butcher zote zilikuwa Mali ya Serikali chini ya DDC Mwnykt akiwa Hayati Judge Lawrence Makame aliekuja kuwa Mwnykt wa Tume ya Uchaguzi kabla ya Mjamaa Lubuva
 
Hata hao mamlaka ya vipimo nao si wananunua nyama buchani au wao wanaenda na mizani zao?
Ndugu yetu mbona una kichwa kizito? Hapa unasaidiwa wewe maarifa ya kujiepusha na wizi mdogo mdogo, sasa ni juu yako kumhoji anayekuibia pindi ukiyaona mazingira hayo au uendelee kusubiri mamlaka.

Cha ajabu, mtu kama wewe wewe, akiona anapigwa mwizi mtaani hata husubiri mamlaka, unarusha mawe hata kama hujui ameiba nini.
 
Dar kwa uroho wa nyama ni tabu kila sehem huu mchezo upo,nilienda bar moja kula kitimoto na beshtee hapa tumeagiza kilo moja rost cha ajabu ilifika mezani ni chini ya nusu kilo imepungua ikabidi tumuite meneja mwisho wake mara hivi mara vile.
 
Nawakaribisha watu wa vipimo wilaya ya Ilemela, Mwanza wafike huku Kiseke A na Kiseke PPF waone maajabu. Hakuna mzani mzima, yote mibovu maana haijawahi kukaguliwa!!!
 
Ha ha ha msiogope akigizeni nyama bomba ya kongwa kutoka Dodoma kwa oda maalum,,,nyama nyama kwel,ukiichemsha unasikia harufu ya nyama sio nyama unachemsha unasikia km unachemsha dagaaa
 
Alafu kunamwingine anafunga uzi mwembabaaa katika vishikio vya bakuli la kuwekea nyama.
Alafu anafunga kwenye dolegumba kisha wakati anapima anavutavuta chini uleuzi na lolegumba kama anapiga drams ilikubalance uzito. Wahuni sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…