Usipopigwa Kofi Na Malaika Utapigwa Konzi Na Shetan

Ambiele Kiviele

JF-Expert Member
Dec 29, 2014
15,267
29,906
Manzi anakupenda balaa.. Anasubiri wewe tu umwambie ili muanze maisha matamu. Tatizo moja linajitokeza, we ni domo zege‍♂‍♂‍♂‍♂

Unajikakamua usiku huo, unamtumia meseji kuwa unakitu kitamu sana cha kumwambia. Demu anakujibu kwa bashasha, niambie. Unakaa kimya dakika 10. Anatuma txt ingine kuomba umwambie.

Unaamua kughairi kumwambia kwa madai ni jambo la kipuuzi sana hasa kwa umri wenu. Ila demu anakusisitizia umwambie. Anakopa hadi salio na kukupigia akiomba umwambie hivyohivyo. Unaamua kumwambia kuwa utamwambia kesho Manzi hana jinsi, anaamua kutry to sleep with broken heart.

Kesho yake mtoto anajipara balaa. Tena anachagua saa 2 usiku ambapo tayari wazee wake wamelala. Mnakutana maeneo fulani ambapo watu si rahisi kuwaona. Unaanza porojo zako. Mara leo tumekula nyanya chungu, mara ukila dengu ukijamba ushuzi unanuka balaa. Hujakaa vizuri unaanza kuhadithia Stori Za Kivita Mwishowe manzi anakuuliza jana ulitaka kuniambia nini? Tena huku kalegeza macho nadhani hata ubongo pia utakuwa umelegea. Chance pekee ambayo kamanda kama mimi nadokoa tu! Nafunga goli la kunyanyulia kombe

Unakaa kimya dakika kadhaa. Manzi pumzi zinapishana huku akili yake inawaza maneno matamu utakayoyamwaga. Na kweli, kimya kingi kina mshindo. Domo zege unaamua kufunguka uliyotaka kumwambia.

Unaanza kwa kumtaja. Naye anaitika kwa heshima. Unamwambia hili jambo ni la kipuuzi sababu ya umri wenu kutoruhusiwa na wazazi wenu na hata dini. Demu anakurekebisha, anakwambia hamna kitu cha kipuuzi kama tutaridhiana. Unafurahi kwa kukupa ahueni ya kuzidi kutiririka. Basi unaendelea kwa kumuita tena jina lake.

Unamwambia jambo nililotaka kukwambia.
Hapo unatulia kwa sekunde kadhaa kama vile MaMC wanavotaka kumtangaza Miss World. Binti Kimoyo kinaenda paa paa paa mpaka kitisheti kinafunuka

Unamalizia kwa kusema, naomba uniibie peni kwenye duka lenu

Kiukweli usipopigwa kofi na Malaika, utapigwa konzi na Shetani

 
habari hii umeiandika wewe domo zege ukikumbushia enzi zako ulivyojikanyaga kwa bint'flani na sasa unajuta jinsi ulivyompoteza kijinga.

Ama waweza kuwa ni binti uliyehangaishwa na hilo domo zege.
Hakuna kofi la shetani wala ubawa wa malaika kwenye masuala ya sanaa ya mapenzi.
 
habari hii umeiandika wewe domo zege ukikumbushia enzi zako ulivyojikanyaga kwa bint'flani na sasa unajuta jinsi ulivyompoteza kijinga.

Ama waweza kuwa ni binti uliyehangaishwa na hilo domo zege.
Hakuna kofi la shetani wala ubawa wa malaika kwenye masuala ya sanaa ya mapenzi.
Mbona Umetokwa Na Mapovu Sana Ndugu Yangu Kana Kwamba Aliyekuwa Anazungumziwa Ni Dada Ako

Ok Saww
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom