Usipige kura kwa ushabiki

Usipige kura kwa ushabiki

Baba Mtu

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2008
Posts
870
Reaction score
170
Bahati nzuri niliyonayo ni kwamba nimeshiriki chaguzi zote zilizopita, yaani nimepiga kura tangu uchaguzi wa kwanza mwaka 1995. Tatizo liko kwa wanaoanza kupiga kura mwaka huu.

Kwa hawa wanaonza kupiga kura mwaka huu naomba niwasaidie kitu, uamuzi wa kuelewa ama kutoelewa ni juu yao. Kuwarahisishia kuelewa ama kutoelewa, ninapanga chaguzi hizo katika AWAMU TATU kama ifuatavyo:

1. AWAMU YA KWANZA

Hii ilikuwa ni kipindi cha Mrema na chama chake. Mrema alitingisha kipindi chake. Kampeni zilipamba moto sana, nakumbuka gari yake ilikuwa ikisukumwa na wafuasi wake.

Lakini chama cha Mrema hakikushinda. Kabla ya kuhamia upinzani Mrema alikuwa Waziri wa Mambo ya ndani na baadae Waziri asiyekuwa na wizara maalum katika Serikali ya CCM. Mrema alifanya kazi nzuri sana alipokuwa waziri, moja ya kazi zake ni hivi vituo vya polisi mnavyoviona mitaani, maarufu kama POLISI POST. Lengo la kuvianzisha ilikuwa kudhibiti uhalifu. Chama cha Mrema hakikushinda katika uchaguzi kwa kuwa wananchi tuliaminishwa kuwa wapinzani walikuwa bado ni wachanga, hawakustahili kupewa nchi kuongoza.

2. AWAMU YA PILI

Hii ilikuwa ni kipindi cha chama cha CUF kuwa cha kikuu cha upinzani. Chama hiki kilikuja kwa kishindo kikuu sana, kilifanikiwa kuweka wagombea Tanzania Bara na Zenji. Kilichoikosesha ushindi chama cha CUF ni nini? Cuf ilipoonekana kuwa ni tishio, wananchi tuliaminishwa kuwa CUF ni chama cha kidini, hakifai kupewa nchi kitaleta udini ambao ni uislam.

Wengine wakafikia hatua ya kusema kuwa hata matamshi ya neno CUF ni herufu katika kitabu cha Quran. Kwa upande wa Tanzania Bara CUF ilikuwa na mgombea mahiri, Profesa Lipumba ambaye ni mtaalam wa uchumi duniani. Inasemekana wataalam wa uchumi kama Lipumba kipindi kile walikuwa hawazidi 10 duniani, wazungu walikuwa wakimtumia kufanya tafiti mbalimbali za kurekebisha uchumi katika nchi zao.

Pamoja ubora wa Lipumba lakini hakushinda kwa kuwa wananchi tuliaminishwa kuwa CUF ni chama cha kiislam, kitaleta udini. Kwa upande wa Zenji mgombea alikuwa ni Maalim Seif ambaye aliwahi kuwa kiongoz katika serikali ya smz kabla ya kuhamia upinzani. Kule Zenj nako wananchi waliaminishwa kuwa cuf ilikuwa ni cha cha kidini, na kuwa Seif atarejesha waarabu Zenj. Basi cuf ikawa inanyimwa ushindi kwa kauli kama "HATUWEZI KUBADILI NCHI KWA VIKARATASI". VIKARATASI=KURA.
Basi Wazenji wakaingia machafukoni, wakaanza kuchukiana wenyewe kwa wenyewe. Ile kauli ya ZANZIBAR NJEMA ATAKAE NA AJE, ikabadilika na kuwa ZANZIBAR SI NJEMA.

3. AWAMU YA TATU.

Hiki ni kipindi cha chadema kushika hatamu. Na ndio kipindi tulicho nacho sasa. Miaka ya nyuma wananchi walihitaji sana muunganiko wa vyama vya upinzani ili kupata chama kimoja chenye nguvu za kuing'oa ccm. Mungu amesikia kilio hicho, ameleta UKAWA, yaani baadhi ya vyama vimeungana kupata mgombea mmoja ambaye ni Lowassa, sifa zake zinajulikana.
Hofu yangu ni huku kuibuka kwa sababu kama zile zilizoinyima ushindi cuf. Sasa hivi ziko propaganda kwamba chadema ni chama cha kikabila, kitaleta ubaguzi wa kikabila. Enzi za cuf, tulipoambiwa kuwa cuf ni chama cha kidini, tulionyeshwa visu vyenye rangi ya bendera ya cuf. Tuliambiwa cuf imeingiza kontena la visu ili kuanzisha mapambano na jeshi la polisi. Na sisi wananchi bila hata ya kuhoji tukayaweka kichwani na kuacha kuichagua cuf, tulipishana na neema. Mwaka huu tunaambiwa chadema ni chama cha ukabila kwa kuwa viongozi wake wengi ni wachaga. Na sisi wananchi tunaelekea kuyaamini hayo, tunataka kupishana na neema nyingine.

USHAURI WANGU

Nenda kapige kura umchague rais unayemtaka, ila usipige kura kwa ushabiki. Una watu watu wa kuwapigia kura, ambao ni rais, mbunge na diwani. Si lazima kuwachagua wote kutoka chama kimoja. Angalia diwani aliyepita amefanya nini ktk miaka mitano iliyopita. Ukiona amefanya mema mpe kura bila kujari anatoka chama gani. Ukiona mbunge aliyepita amefanya mema mpe kura bila kujari anatoka chama gani. Bahati mbaya ama nzuri marais wote ni wapya na washawahi kufanya kazi pamoja. Ukiona Magufuri kupitia ccm iliyokaa madarakani zaid nusu karne inakufaa, ipe kura ya urais. Ukiona Lowassa kupitia cdm ambayo haijawahi kukaa madarakani anakufaa, mpe kura ya urais.
Ila mimi kama mimi, kura yangu ya urais ni kwa Lowasa. Mi simlazimishi mtu kumchagua fulani. Sina shaka na Magufuri. Tatizo ni mfumo unaomzunguka. Kikwete wakti anaingia madarakani alituahidi MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA. Alishindwa kutimiza kwa kuwa mfumo ulomzunguka ni mbovu. Tembeeni muone kama MAISHA NI BORA KWA KILA MTANZANIA ama MAISHA NI BALAA KWA KILA MTANZANIA. Msikae tu maofisini na majumbani mwenu, tokeni na tembeeni muone jinsi hali halisi ya maisha ya mtanzania yalivyo, piteni katika shule na hospitali za serikali muone hali ikoje.
Sikwambii mpigie fulani kura, akili yako changanya na za kuambiwa.

MUHIMU:

TENDA HAKI, SIMAMIA HAKI, JIEPUSHE NA DHULMA, kumbuka kutakuwa na siku ya hukumu, siku iliyo kuu kabisa, siku ambayo ujio wake hauna shaka. Siku hiyo kila mtu atalipwa haki yake na mola mlipaji mkuu.
MUNGU IBARIKI TANZANIA
 
Wamejaribu kutugawa mara mbili wamefanikiwa. Safari hii tumeungana sijui watasema UKAWA dini gani!

25 10 2015 ni mkesha wa mwaka mpya
 
Back
Top Bottom