Usiombee kukosa hela

Usiombee kukosa hela

The Initiator huru

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2017
Posts
2,326
Reaction score
3,202
Hivi umewahi kukosa hela na huku unanuka madeni mpaka ukatamani hata mtu akosee kutuma mpesa, au tigo pesa, ili hela ije kwako? Au ukatembeatembea ukiamini unaweza hata okota hela mtu aliyedondosha? Kweli wanaume tumeumbwa matesooooo, matessooo kuhangaika.

Nina salio la buku (1000) kwenye wallet ndio kwanza jumatatu. Ee Mola ninusuru. Wangapi tunapitia haya? kama unaamini ni mapito tuu na sisi sikumoja tutakuwa na fedha za kutosheleza mahitaji yetu type Amen.
 
Afadhali yako huna familia

Mimi dogo amerudishwa school kisa nimeshidwa kulipa 8000 ya uji

Na mvua ndio zinanyesha hatari, dogo viatu vimechanika maji yanaingia mpaka ndani
,
Nikaenda kukopa vibuti vya kavaa dogo awe anavaa aende navyo shule, yule mama ananidai utazan amenikopesha moyo daily hodi haziishi
 
Afadhali yako huna familia

Mm dogo amerudushwa school kisa nimeshidwa kulipa 8000 ya uji

Na mvua ndio zinanyesha hatar,dogo viatu vimechanika maji yanaingia mpaka ndan
,
Nkaenda kukopa vibuti vya kavaa dogo awe anavaa aende navyo shule,yule mama ananidai utazan amenikopesha moyo daily hodi haziishi
That which doesn't kill us makes us stronger. Mkuu huwa ni motivational morale ya kufight, mkuu ipo siku utaangalia nyuma alafu utasema imebaki stori. Litapita mkuu trust me.!
 
...Kuna siku nilienda kwa wakala,kutuma pesa kwa a/c yangu,maana ilikuwa wikend niliogopa nitaila,maana nilikuwa jumatatu nipunguze ada ya dogo,nikampa yule wakala laki 2,na nikampa na kadi yangu ya benki,akanipa risiti, nilikuwa na haraka nikaondoka zangu nikijua nitapata sms ya simbanking, maana siku hiyo mtandao ulikuwa unasumbu,jumatatu nacheki mpunga holaa,ikabidi nipitie ile risiti,nakuta yule dada alikosea namber.jioni wakati narudi mihangaikoni nikapita pale yule dada wacha awakee,pembeni alikuwa mumewe mualewa,nikampa risiti akaikaguaa,akampigia jamaa yake wa tawi la benk afuatilie niwapitie kesho,kesho nikapita jamaa akanambia pesa mkewe aliituma kimakosa kwa mtu mwingine na ashakomba laki 1 moja,huyo jamaa wa benki alimpigia huyo jamaa na kukili akaihidi kurudisha mwisho wa mwezi.....Mwisho wa mwezi wakanipa hela yangu jamaa aliirudisha
😀😀
 
haya maisha haya, kuna wakati mate yalinidondoka kwa kutamani chakula alichokuwa anakula mtoto wa jirani yangu, baada ya kushinda njaa takribani siku nne,yaani sikuwa na hata mia mbovu.

namwomba Mungu nisirudi nilipotoka.
Siku nne hujala chochote mkuu..i mean yaani hata punje moja ya karanga?..
 
Back
Top Bottom