Usiombe yakukute jamani, daah!!!

inasisimua
That is why nimekwambia usiombe yakakukuta haya mambo!
Sikuwahi kuitegemea hii hali,imekuwa mateso sana kwangu,na hata hamu ya wanawake sina kabisa!

Na nikitoka hapa salama,I swear to God,nitamheshimu mke wangu daima,sijafunga ndoa wala sijalipa mahari,ila baada ya kuchoropoka hapa,nitarasimisha ndoa na mama watoto wangu basi!!!
 
Ok au ni hizi safari ndogo napiga hapa 5N ndo zinafanya macho hayaoni vizuri
Ndugu usiombe haya mambo kabisa,bora ujinywee via nenda zako ukalale upumzike,lakini baadhi ya hawa wanawake wanatia hasira sana!
 


Kama unaweza mruhusu Rafiki wa kike alale chumbani kwako halafu wewe ukatoka unarudi saa 4 usiku bado yupo amelala kama kwake. Hapo ulikuwa na interest nae pia may be kwa sababu ya umbali na mama mtoto wako. Mazoea ya namna hiyo si mazuri katika desturi zetu.

Kuwa ana watoto wengine wawili kawaacha kwao na aliwapata katika mazingira kama hayo ingawaje hujafafanua hiyo inaonyesha huyo mtu ni matured na katika hali ya kawaida hakutakiwa kufanya alichokifanya cha kujidhuru ili wewe uogope - yaani uwe mateka?

The whole story sioni tatizo hapo wewe baki katika msingi wako wa mke mwenye watoto wawili maana huyu wa kujidhuru alikuja anajua. Kujidhuru ndio kukufanye iwe chachu ya kumpiga chini. Lakini huwezi kumpiga chini wakati mnakaa katika neighbourhood na manafanya kazi pamoja.

Dawa ni kuwa mbali nae ndio utaweza ku move on otherwise itakuwa ngumu. Hama kikazi la sivyo kisu kitakuja kwako au anaweza kukuua na kujiua maana mental stability yake iko fragile. Good luck.
 
Nakupa pole sana mkuu mana mwanaume rijali kupishana na haya maswaibu ni Mungu tu aingilie kati japo tunamkwaza lakini yeye ndo kila kitu wa kutuepusha na majanga.
Ndipo hapa kuna kauli inasema shetani ni mtaalam sana wa kutengeneza masufuria tena mazuri mno ila ameshindwa kutengeneza mifuniko that means ni mtaalam wa kutengeneza dhambi tena zilizo nzuri ila hana uwezo wa kutengeneza mfuniko wa kuficha dhambi.

Njia za kumpenda mwenza uliyekaribu naye zipo nyingi kuna njia nyepesi na njia ngumu ila hii ya kwako ni njia ngumu ambayo imekufanya kumpenda mke wako wa kwanza kama ulivyainisha hapo mwishoni.

Nakutakia mapito yaliyo mema, na Mungu akupe ujasiri na nguvu katika hilo sakata, ilianza saa, siku, wiki, mwezi, mwaka kufanya mambo yapite na kusahaulika.
 
Nipo njiani kuelekea huko ulipokuwa, na dalili naanza kuziona kwa mbaaali, ila tatizo linakuja kwenye kujitoa kwenye hii kitu, lazima mmoja apate maumivu, na anaweza kuchukua maamuzi magumu.
 
Nipo njiani kuelekea huko ulipokuwa, na dalili naanza kuziona kwa mbaaali, ila tatizo linakuja kwenye kujitoa kwenye hii kitu, lazima mmoja apate maumivu, na anaweza kuchukua maamuzi magumu.
Na inahitajika umakini mkubwa sana ndugu,kwa sababu ikitokea amekufa (kwa kuacha ujumbe kuwa wewe ni chanzo cha kifo chake) hakika utapoteza vyote,utapoteza familia yako ya sasa na utapoteza mwelekeo mzima wa maisha yako,muhimu ni kujitahidi kuyamaliza katika namna ambayo haiwezi kuacha madhara ya yeye kutoa uhai wake,ni hatari sanaaa!!

Mungu atusamehe,na atusaidie kuyavuka haya,baada ya hapa tusirudie tena makosa yafananayo na haya,hakika imenifunza sana!
 
Nimejifunza jambo hapa
Pole sana mkuu.
Nakushauri kama utaweza basi waoe wote wawili japo imani yako inaweza kukinzana ila hauna namna take risk tu
 
Nimejifunza jambo hapa
Pole sana mkuu.
Nakushauri kama utaweza basi waoe wote wawili japo imani yako inaweza kukinzana ila hauna namna take risk tu
Mkuu nadhani hiyo itaniumiza zaidi mimi,maana hata yule wa kwanza hawezi kuelewa,yaani mtu ambaye amekuwa rafiki yake na amekuwa akimpokea leo awe mke mwenzake!!!

Nadhani kuondoka kabisa mazingira haya ni bora zaidi,na nimeamua kuacha kila kilicho changu,nitaondoka kama nilivyo,vitu vitakavyobaki itakuwa kwa ajili ya mtoto wangu!
 
Kwahiyo unaacha kazi?
Unakimbia tatizo?
Una uhakika ukikimbia tatizo utakua umesaidia?

Relax tafuta akili ya kuweka mambo sawa wala huna haja ya kukimbia maana bado huna kesi ya kukupeleka jela, mwanaume unaanzaje kukimbia changamoto ya kimahusiano?
Kama vipi hama hiyo nyumba ili mkae mbali mbali na uendelee kumhudumia huyo mwanamke mpaka mtoto wako atakapozaliwa ndio ujue cha kufanya
 
we jamaa bana.........wanawake hawasogezwi karibu.....umevuruga kweli kweli.......pambana tuu....ila mkeo uliyeumbiwa ni yule wa Singidani.......huyo umpendae ni mgambo wa iblisi.....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…