STUNTER
JF-Expert Member
- Dec 15, 2015
- 13,077
- 17,260
UNAFIKI tabia mbaya sana, walio makazini wanajua maudhi ya kuwa na mfanyakazi mwenzao mnafiki anaetaka kujipendekeza kwa Bosi. Huyu atakuwa kazi kumsifu Bosi na kudidimiza wenzake wanaotaka haki. Mnafiki husifia hata ujinga au hata ambacho hakiko.
Atamsifia bosi kuwa ana kohoa kistaarabu, au hata kama bosi ni mfupi atamsifia bosi kwa urefu, au hata kwa kumsifia Bosi kuwa anajali wafanyakazi wake japo bosi ni dhulumati mkubwa. Huyo ndie mnafiki. Kwa kawaida bosi yoyote anamjua mnafiki, na pamoja na kuwa atamchekea mara nyingi atamtumia mnafiki kuendeleza kugandamiza wafanyakazi wake.
Japo kuna mabosi wengine huwa wanafikia kuanza kuamini sifa za mnafiki. Mnafiki anapomsifu Bosi mfupi kuwa mrefu kisha bosi akaanza kujiona kweli mrefu ni tatizo kubwa, mnafiki hana maendeleo kwani ana imani unafiki wake utamfanya bosi amtupie chochote, badala ya kufanya kazi kwa bidii daima hutegemea fadhila za bosi.
Mara nyingi mabosi huwatupia wanafiki makombo, na wanafiki huamini kuwa huo ni mwanzo wa kupata mambo makubwa. Ndugu zangu wanafiki, maendeleo hayategemei fadhila zinazotokana na unafiki, juhudi na kudai haki stahili na kazi iliyofanywa huleta maendeleo.
NAWASILISHA HOJA