Usioe sababu ya mimba na usiolewe sababu ya mimba

Usioe sababu ya mimba na usiolewe sababu ya mimba

G55-MGODI

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2016
Posts
1,353
Reaction score
1,827
Mwanamke aliyempenda mpenzi wake kwa mapenzi ya dhati na kumpa heshima na unyenyekevu mwanaume wake akiwa na tumaini la kuwa amepata mume wa maisha yake na baba wa watoto wake, aliposhika mimba mwanaume alibadili tabia na mwanendo kitu kilichomfanya mwanamke kuwa mkiwa na mpweke kwa kupoteza mtu aliyempenda na kumuheshimu na kuwa na ndoto za pamoja kama mume na mke.

Moja ya kitu kibaya ambacho wanaume tunawafanyia wanawake ni kuwapa uja uzito na kuwakimbia pasipo kutoa gharama zozote wala kuwajulia hali ya mtoto anaendeleaje na kwenda kuoa mwanamke mwingine huku ukiwa umeacha mwanamke na uja zito wako.

Unaweza kumkimbia mwanamke hakuna shaka ila unawezaje sahau damu yako ambaye ni mtoto wako? Unashindwa japo salamu na visitation kwa mama watoto wako? Jua kama mwanamke uliyempa mimba alikuwa ni mwenye mapenzi ya dhati na muadilifu jua kiboko chako kipo na daima watoto wa nje huwa ni wenye akili na nidhamu kuliko watoto wako wa ndani ya ndoa.

Huzuni huja pale unapo upload picture za birthday za mtoto wako wa ndoa kwenye social media ilhali mtoto uliyezaa nje hujui hata birthday yake ni lini.Damu nzito kuliko maji ila yatakiwa tuwe wakweli ili tuwe huru wazazi.Kama umezaa nje ni wakati muafaka wa kuwafundisha watoto upendo wa pamoja na kuwa familia moja bila kuwabagua watoto.

Mungu amekupa pumzi na afya ili uwe mtu wa kutatua matatizo na sio kuongeza matatizo.Je unajua mzazi mwenzio uliyemkimbia toka uja uzito mpaka pindi amejifungua unajua amebeba simanzi kwa muda gani juu yako?
Ulikataa mimba na kumuacha mwanamke akiwa mpweke na mwenye simanzi,mwanamke anapoamua kutafuta mwanaume bora zaidi yako, mwenye mapenzi ya dhati na anayejali zaidi yako.

Mwanaume aliyekimbia mimba huona wivu kuona mwanamke aliyemkimbia ameanza kunawili kwa furaha na mapenzi ya dhati na kuwa na mvuto. Mwanaume mwenye mtoto huja kwa njia ya kutaka kumaliza tatizo ili washirikiane kulea mtoto ila dhamira huwa ni kuvuruga furaha na amani ya mwanamke mlengwa, kwa kuwa wanawake ni dhaifu hukubali na mwisho anapoteza mwanaume bora na kumrudia mzazi mwenzie aliyempa mateso na simanzi na kuendelea na maisha ya ukiwa na upweke.

Zingatia: Usiolewe sababu ya mimba wala usioe kwa sababu ya mimba, mtoto asiwe kigezo cha kuingia kwenye ndoa, ndoa yenye mapenzi ya dhati na yenye chemistry nzuri ndio kitu muhimu zaidi, mkiunganishwa na mtoto na hakuna chemistry kati yenu, jua unaingia kwenye ndoa ngumu sana omba Mungu akupe hekima na busara kufanya maamuzi sahihi. When your ex says “you’ll never find anyone like me” Just smile and reply “that’s the point”.
 
Dada'ngu Nifah ile avatar yako imeenda wapi? Usijaribu kuibadili inakutambulisha sana. Hasa ile lipstick [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Sijabadili na sitokaa niibadili mkuu.
Ile ndio Avatar ya maisha yangu huku JF.
Leo sijui kuna tatizo gani...kuna wakati Avatar zinabadilika.
 
unazijua shida za mtoto kulelewa na baba/mama wa kambo?
 
Back
Top Bottom