NGAYANIMO
Member
- Feb 17, 2026
- 42
- 58
Afande sele.( Verse)..
"inshallah kama umenisamehe
Kama bado basi Ewallah
Yote namuachia Allah
Kwani tulipo , Tupo kwa vile ametaka Tuwepo/
Anatupenda Sawa sawa kabisa/
Wote anatupa Mvua,misikiti na makanisa/
Na wote anawapa jua masikini na Wenye pesa/
Kama kuvuta Pumzi kwa wote amesema Ruksa/
Sasa iweje wewe unichukie/
Na hata kama na kosa kwanini usiniambie/
Eeh..!!
Chuki ni dhambi Rafiki, na Dhambi ikitunga mimba mwishoni itazaa mauti/
Kumchukia mwenzako Tena bila sababu ni kumkera muumba wako/
Aliyekulinda Tangu ulipokuanga mimba/
Aliyekuumba binadamu wala sio Simba Au mamba/
Ni kwamba mimi ni Rastafari/
Eeh.!!
Hapa Duniani naimani mimi msafiri/
Sele..!!
Sitaki shari ukininyang'anya shati nitakupa mpaka suruali/
Narudi kwetu Moro/
Watu wakiniuliza nitajibu tuna mgogoro/
Kama mimi na solo/
Thank You hata mimi na majani..."
Kuna maneno hapa aliyoandika selemani msindi a.k.a afande sele katika verse hii katika wimbo huu "usinichukie" maneno ambayo mara nyingi hutumiwa na watu ambao wana Imani ya kiisilamu" ( Islamic)..
Neno.
1. Inshalla - maanake anamaanisha "Mungu akipenda "
2. Allah - ni jina la Mungu wao
3. Ewallah - " Wallah " tafsiri yake nina muamini Mungu
Sisi sote ni ndugu, tutaniane, tuelekezane kwa Upole Na TUSICHUKIANE. Tofauti zetu za Maisha Wala Zisitufanye TUCHUKIANE. Sisi ni NDUGU..
Tunatofautiana ki Imani Tu.
Ukwaju wa kitambo
0767 542 202