Maisha ni ushindani jamani, kila kitu hapa duniani ni kushindana anayeshinda anapewa taji, ukitaka kuwa na nguvu lazima ushindane na ili ushinde lazima uwe na technique za kushinda iwe kiroho au kimwili.
Mwanamke kuolewa ni mashindano angalia mnapokuwa kwenye uchumba ni wangapi wanamtaka huyo mwanaume? na kuwa kwenye ndoa ni mashindano sio kwamba ukipata ndoa ndio umemaliza no unahitaji technique za kuhakikisha unaulinda ushindi wako, ukizubaa unanyang'anywa kombe na hapo unakuwa umeshinda, kwenye biashara kuna mashindano, ukifirisika umeshindwa mashindano, usichukie mwenzio anaposhinda ila ikupe hasira za ndani kutafuta mbinu na bidii ili upate kushinda mchezo wako
Ambacho hakitakiwi ni mashindano ya maneno hayo hayana faida
2 Timotheo 2:14
[14]Uwakumbushe mambo hayo, ukiwaonya machoni pa Mungu, wasiwe na mashindano ya maneno, ambayo hayana faida, bali huwaharibu wasikiao.
Lakini kushindana kuliko halali kunaruhusiwa
1 Wakorintho 9:24-26
[24]Je! Hamjui, ya kuwa wale washindanao kwa kupiga mbio, hupiga mbio wote, lakini apokeaye tuzo ni mmoja? Pigeni mbio namna hiyo, ili mpate.
[25]Na kila ashindanaye katika michezo hujizuia katika yote; basi hao hufanya hivyo kusudi wapokee taji iharibikayo; bali sisi tupokee taji isiyoharibika.
[26]Hata mimi napiga mbio vivyo hivyo, si kama asitaye; napigana ngumi vivyo hivyo, si kama apigaye hewa;