Usimwonee wivu mke umpendaye, utakuwa umemfundisha namna ya kukudhuru

DeepPond

JF-Expert Member
Nov 18, 2017
40,494
99,260
SIRA 9

Wanawake

1Usimwonee wivu mke umpendaye;
utakuwa umemfundisha namna ya kukudhuru.

2Usimwachie mwanamke ukuu wako,
la sivyo atakutawala kabisa.

3Usifuatane na mwanamke wa tabia mbaya,
la sivyo utanaswa katika mitego yake.

4Usishirikiane na mwanamke mwanamuziki,
la sivyo, utanaswa kwa werevu wake.

5Usimtazame kijana msichana mzuri;
la sivyo, wewe na yeye mtapata adhabu ileile.

6Usimpe malaya moyo wako,
la sivyo utapoteza nchi yako yote.

7Usipepesepepese macho mitaani mjini,
wala kuzururazurura kwenye maeneo yake ya pekee.

8Usimtazame mwanamke mzuri,
usimkodolee macho mwanamke mrembo asiye wako.
Maana wengi wameangushwa kwa uzuri wa mwanamke,
maana jambo hilo hufanya tamaa kuwaka kama moto.

9Kamwe usiketi na mke wa mtu,
wala kuketi naye kunywa pombe
la sivyo moyo wako utampenda
nawe utakosa kujizuia ukaangamia.
6862c81bb56345488c431b0ddd95f742.jpg
 
Kipo kinaitwa Yoshua bin SIRA ,kitafute utakipata

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata ningekua mimi ndio shetani.
Lazima ningefanya jambo kama hilo.. alilolifanya.
(Mbinu ya uwongo)

Ningetafuta mwanadamu mmoja na kumwambia etengeneze sura kadhaa / kitabu na nimwambie nenda kawadanganye uma kuwa hivi navyo ni vitabu vya Mungu na vilifaa kuingia kwenye bible, sema walivipunguza tu.
😂😅😅
 
Hata ningekua mimi ndio shetani.
Lazima ningefanya jambo kama hilo.. alilolifanya.
(Mbinu ya uwongo)

Ningetafuta mwanadamu mmoja na kumwambia etengeneze sura kadhaa / kitabu na nimwambie nenda kawadanganye uma kuwa hivi navyo ni vitabu vya Mungu na vilifaa kuingia kwenye bible, sema walivipunguza tu.
Usisema kitu ambacho hata hukijui ,kumbuka mapadri ndo Huwa wanatumia hivi vitabu ,Vipo vitabu kama hiki, MAKABAYO, SIRA,N k.Usikalili pia kumbuka biblia original ipo na siyo hii unayoitumia wewe.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naona thread inaenda kubadirika na kuwa ya kutambulika au kutokutambulika kwa hicho kitabu katika biblia
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom