Mwanamke mwanamke Mwanamke

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
5,984
7,753
Sira 9

1 Usimwonee wivu mke umpendaye; utakuwa umemfundisha namna ya kukudhuru.

2 Usimwachie mwanamke ukuu wako, la sivyo atakutawala kabisa.

3 Usifuatane na mwanamke wa tabia mbaya, la sivyo utanaswa katika mitego yake.

4 Usishirikiane na mwanamke mwanamuziki,
la sivyo, utanaswa kwa werevu wake.

5 Usimtazame kijana msichana mzuri; la sivyo, wewe na yeye mtapata adhabu ileile.

6 Usimpe malaya moyo wako, la sivyo utapoteza nchi yako yote.

7 Usipepesepepese macho mitaani mjini,
wala kuzururazurura kwenye maeneo yake ya pekee.

8 Usimtazame mwanamke mzuri,
usimkodolee macho mwanamke mrembo asiye wako. Maana wengi wameangushwa kwa uzuri wa mwanamke,
maana jambo hilo hufanya tamaa kuwaka kama moto.

9 Kamwe usiketi na mke wa mtu, wala kuketi naye kunywa pombe; la sivyo moyo wako utampenda
nawe utakosa kujizuia ukaangamia.
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom