Magoya2000
JF-Expert Member
- May 7, 2017
- 641
- 1,267
Habari wadau. Biblia inasema usimuache Mwanamke wa ujanani. Hii inamaanisha wewe kama Mwanaume jitahidi Sana usiwe chanzo au wa kwanza kutaka kuachana. Maisha ya Mungu yeye ndo anatupangia utaishi vipi... Hivyo nashauri kama unataka kuishi Maisha ya furaha na amani ni bora Mwanamke akuache wewe. Mwanamke akikuacha utaishi kwa amani Sana. Wanawake wengi Wana visasi na roho za revenge. Hivyo mpe nafasi yeye akuache wewe. Usiumie Mwanamke akikuacha, ni muda tu utapona maumivu hayo. Haya Maisha wanawake wazuri wapo Sana. Population ya wanawake na wanaume wametuzidi. Kikubwa cha kufanya tuliza akili yako Muombe Sana Mungu akuepushe na revenge za wanawake maana Mwanamke akikuacha atafurahi akikuona umechoka hutamaniki kama wewe mlevi Basi uwe mbwa wa kuokotwa mtaloni.... Ndugu zangu Mwanamke akikuacha wewe furahi jisogeze kwa Mungu omba Sana. Mungu ndo anajua destiny yako..Mungu atakuinua utaona mafanikio yako Sana. Ukipata pesa utajua jinsi ya kuishi na wanawake... Wengine utawakimbia wewe mwenyewe.. Pesa ndo Kila kitu... Tafuta pesa utaona raha ya dunia.