Usimnyime mwanao haki ya kumjua babaye | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usimnyime mwanao haki ya kumjua babaye

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Ozzie, Jan 4, 2011.

 1. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Wana JF,
  Mimi kwa fani ni daktari bingwa wa magonjwa ya binadamu Internal Medicine; nimeona nitumie wasaa huu kuwakumbusha au kuwashauri baadhi ya watu hususani dada zetu kwamba ni haki ya watoto waliowazaa kuwajua baba zao pindi wanapohitaji na hata kama hawahitaji bila kujali kama hamna mahusiano tena na baba huyo kwa sababu zozote zilizopo duniani; hii ni baada ya jana kukutana na dada asiyetaka mwanae amjue baba yake.
  Mwaka 2005/2006 nilikuwa nafanya internship katika hospitali ya Taifa nyumbani Tanzania. Kwa kawaida ukiwa wafanya internship utapangiwa ratiba ya kuzunguka katika idara mbalimbali ikiwamo ya magonjwa ya akili, Psychiatry.
  Nikiwa psychiatry nakumbuka kuna mtoto wa kiume wa miaka kama kumi na nne aliletwa toka Hospitali ya mkoa wa Morogoro akiwa na tatizo la kuchanganyikiwa. Kwa ufupi yeye binafsi alikuwa hajui jina lake na hata mahala alipotoka. Mtoto alikuwa haongei na mtu na hata akiongea anachagua baadhi ya watu na akichagua hataongea maneno yanayoeleweka.
  Bahati nzuri idara ya Psychiatry ya hospitali husika huwa inatoa huduma nzuri sana, kiasi cha kuwa baada ya wiki tatu za kulazwa huyu mtoto akawa anaanza kurudiwa ufahamu na kuweka kulikumbuka jina lake. Taarifa kuhusu huyu mtoto zikatangazwa na muda si mrefu mama mzazi (alikuwa akiishi Tanga) wa mtoto huyu akapatikana. Baadaye tukaweza kuongea vizuri na mama pamoja na mtoto.
  Kumbe mama aliwahi wekwa unyumba na mwanajeshi fulani aliyekuwa amehamia karibu na kijiji chao huko Tanga; lakini mama angali mjamzito kukatokea kutokuelewana kwa hawa wapenzi wawili kulikosababisha kutengana!!! Baba akachukua hamsini zake na mama akachukua hamsini zake pamoja na mimba.
  Mtoto alipozaliwa tu, baba akahamishwa na kupelekwa kambi isiyofahamika na mzazi mwenzake, kwa kuwa mama hakutaka kujua.Hata mtoto alipozidi kukua na kuuliza baba aliko hakuwa anapata jibu sahihi zaidi ya kujua jina na kazi ya baba yake.
  Ikafika kipindi mtoto kahitimu darasa la saba na kachaguliwa kwenda boarding school nje ya mkoa wa Tanga. Mama akamwandalia mwanae kila kitu ikiwamo pesa za ada na za matumizi ya kila siku. Kama kawaida ya watoto wengi wa kiume wanaotoka katika familia za kigumu au kimaskini, mtoto alisindikizwa mpaka kituo cha basi tu ingawa alikuwa anaenda nje ya mkoa tena asioufahamu!
  Masikini kumbe mtoto ndio kapata mission ya kumtafuta baba yake akitumia pesa alizonazo. Moja kwa moja akaenda Makao makuu ya jeshi Lugalo, Upanga Dar es Salaam; ambapo kwa bahati aliambiwa kuwa baba yao alikuwapo kwenye ile kambi miaka kama miwili iliyopita lakini akawa amehamishiwa tena kwenda kwenye kambi nyingine iliyopo Morogoro (Nimesahau Wilaya). Mtoto akafunga safari mpaka kwenye kambi husika huko Morogoro. Bahati mbaya alipofika akaambiwa mzee anayemtafuta kafariki wiki moja kabla!!! Hapo ndipo mtoto alipopata tatizo la akili. Akalazwa katika hospitali ya wilaya husika kwa wiki mbili baadaye waliposhindwa wakampeleka Hospitali ya mkoa wa Morogoro ambao nao waliposhindwa wakamleta kwenye hospitali niliyokuwa nafanya kazi.
  Si kila mtu akipitia jambo kama hilo lazima atapata mtindio wa akili, lakini bila shaka mtoto alikuwa ana genetic predisposition ambazo zikawa triggered na mazingira aliyokuwa akiyapitia. Nashukuru kwamba mwisho wa siku yule mtoto alirudi kuwa na akili nzuri, japo sijui maendeleo yake kwa sasa.
  Ujumbe uliopo hapa ni kwamba haijalishi umekosana vipi na mzazi mwenzio, mwanao ana haki ya kumjua baba au mama yake. Tena tuwe na tabia ya kufanya migongano kati ya wazazi inaishia kwa wazazi na hakika tuepuke kupandikiza chuki za bifu zetu kwa watoto. Hata kama mzazi mwenza ni jambazi, kahaba, muuaji; mtoto hastahili kujua mambo hayo; ila anastahili kujua kwamba hawa wawili ndio wazazi pekeee nilionao hapa duniani.
  Shukrani,
  Ozzanne.
   
 2. Fab

  Fab JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2011
  Joined: Apr 16, 2010
  Messages: 763
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mnh ina maana mama alimwambia mwanaye kuhusu baba???mtoto alijuaje pa kuanzia ni lugalo??

  kama ni mazingira hata huko shule pia yangeweza kutrigger huo mtindio...

  mind ni kitu complex,huwezi ukasema for definite kuwa ishu ya babayake ndio actually iliyocause huo mtindio.....

  na ishu za akili sio kama malaria,au typhoid kuwa kuna kipimo maalumu unapima then you know whtswrong with you!....
   
 3. LD

  LD JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Thanks.
   
 4. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Mh siku ingine ufupishe!

  Mtoto anahaki ya kuwa na baba na mama yeye hausiki katika ugonvi wenu... (yeye ni victm tu wa circumstance) mpe haki yake!
   
 5. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hapo kuna mawili..we lawama zote umemwaga kwa mama!Je kama huyo baba alikua hataki chochote kinachohusiana na huyo mtoto?Kama yeye hakufanya jitihada za kua na uhusiano na mwanae mama hawezi kulazimisha!Fikiria kama huyo baba alikua hamtaki huyo mtoto..mama akamtafuta mwenyewe akampeleka mtoto alafu huyo mzee akamkataa mtoto akishuhudia unadhani angeathirika kiasi gani?Kila mtu yuko kwenye situation tofauti kwahiyo huwezi tu kumwambia mtu mjuze mtoto baba yake bila kujua kilichopo nyuma ya pazia
   
 6. Riwa

  Riwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2011
  Joined: Oct 11, 2007
  Messages: 2,601
  Likes Received: 234
  Trophy Points: 160
  Ni kweli Ozzie, nimeshaona hili katika familia moja ambayo inanihusu. Mtoto sasa wa kiume ana umri zaidi ya miaka 20 sasa, alikuwa hamfahamu wala hakukutana na baba yake mpaka akiwa na miaka 18. Alipata 'msongo' wa mawazo, akadrop out toka shule (alikuwa kidato cha tano, na alikuwa anafanya vizuri sana shule), akaanza kuvuta bangi kupita kiasi, na hakuna mtu anayemwambia chochote...mama yake ndio kabisa, mtoto anatumia 'excuse' ya kutojuzwa baba yake! Ilibudi mama yake amtafute baba (ni mNigeria sijui hata alikuwa wapi), akaja Tz lakini haikusaidia na alitimuliwa mbio na matusi meengi kuwa siyo baba yake. Sasa hivi hakuna anayemuweza, ameshalazwa wodi 'psychiatry' Muhimbili mara kadhaa, counseling na madaktari bingwa wa magonjwa ya akili imeshindikana, na juhudi za kumpeleka Milembe hazijawahi kufanikiwa.

  Hivi vitu tunadharau...lakini tuna'understimate' ukuaji wa watotop wetu kiakili na uwezo wao wa kukubali/kukabili haya mambo.
   
Loading...