BADILI TABIA
JF-Expert Member
- Jun 13, 2011
- 32,766
- 23,230
usikopeshe mtu ndo mwanzo wa kuharibu undugu au urafiki
Mimi nimeshawah kumweka mjomba wangu wa dam kabisa polisi kwa siku 4,mbna alilipa!
kweli we kauzu zaidi ya dagaa................... ni msemo tu.
na ukampa tenaInaumiza sana mi ndugu aliniomba nikamkopesha akala kimya kuona simfuatilii akaomba tena zaidi ya ya mwanzo loooh
Nilishawahi kumkopesha kaka yangu hela ndefu nilivyoona nikienda kumdai anakuwa mkali..nikamchunia kama mwezi hivi..ila nilichomfanyia kamwe hatakaa anisahau..kwani nilimkomba tv na sofa..mpaka leo hatuongei..
duu mimi nina mdogo wangu nimemkopesha 1m tokea mwaka jana nov mpaka leo yeye na mumewe ,naona kimya tuu,mdogo wangu kama upo humu na unasoma hii msg please nilipe mwaka mzima bandari haijatema tu
Hii kitu ya uaminifu ni ngumu kwa watu wengi sana sijui kwanini! Mie nilimkopa binamu yangu kiasi fulani, alikuja akinambia biashara yangu imekwama nataka nichukue mzigo, nikisha uchukua nakuuza nakurudishia pesa yako J3 week ijayo. Nikamwambia mama kuhusu hii kitu akanambia hiyo haitorudi, nikasema kama haitorudi ndo utakuwa mwisho wa kumkopesha maana kiasi hakikuwa kikubwa sana kiasi hicho... siku hiyo hiyo nikamtumia Tigo pesa, wiki ikakatika, mwezi hadi mwaka mtu kimyaaaaaa! Basi ikatokea mdogo mtu anaolewa aliponiomba mchango nikamrefer kwa dada yake, naye hakumpa hadi leo! Nilichojifunza now, mtu akitaka mkopo ni maandishi tu na kuweka kitu chake cha thamani la sivyo ni kulizwa tu na watu wetu wa karibu