Usimkopeshe ndugu au rafiki wa karibu fedha

Usimkopeshe ndugu au rafiki wa karibu fedha

yoelisahe

Member
Joined
Jul 23, 2013
Posts
72
Reaction score
21
Ndugu zanguni,

Nimeamini unapomkopesha ndugu au rafiki fedha, nikujiletea uadui,au chuki labda uamua kumpa.

Imenitokea mimi kuna ndugu yangu alinikopa fedha, na kuniambia atairudisha mwisho wa mwezi,nilimweleza sina fedha kwa kipindi hicho, ila kwakuwa alinieleza anashida muhimu nikaamua kutoa fedha za mchango wa harusi ya watu kwa sababu nilikuwa nazihifadhi.

Nilimweleza kabisa fedha niliyompa haikuwa yangu bali ni michango ya harusi,hivyo mwisho wa mwezi ukifika airejeshe.
 
Kila mtu anatabia yake na malezi yanatofautiana jinsi mlivyo kuzwa familia yenu na ya wengine ni tofauti.
 
wakati mwingine mtu hukopa pesa huku mooni ameshapanga halipi wewe utahangaika kudai mwisho unaamua kusamehe, kuna rafiki yangu nilimkopesha pesa na hivi huwa sipendi kumkumbusha mtu kila mara basi alikaa kimya miezi sita nikaona ujinganikaanza kumkumbusha mtu akawa hapokei simu nilikoma.
 
Nimekiona Cha Moto hata mie yamenikuta ila huwa nashindwa kujizuia kukopesha watu kwasababu hata mimi huwa nikibanwa nakopa na ninalipa sasa sidhani kama idea ya kuacha kabisa kukopesha watu ni nzuri cause sometimes mtu anakuwa na shida ya dhati na wewe unakuwa kwenye nafasi ya kumsaidia sasa sijui tufanyaje tukiwasaidia wanaingia mitini ila na sisi sometimes tunabanwa na tunasaidiwa
 
Inaumiza sana mi ndugu aliniomba nikamkopesha akala kimya kuona simfuatilii akaomba tena zaidi ya ya mwanzo loooh
 
Nimekiona Cha Moto hata mie yamenikuta ila huwa nashindwa kujizuia kukopesha watu kwasababu hata mimi huwa nikibanwa nakopa na ninalipa sasa sidhani kama idea ya kuacha kabisa kukopesha watu ni nzuri cause sometimes mtu anakuwa na shida ya dhati na wewe unakuwa kwenye nafasi ya kumsaidia sasa sijui tufanyaje tukiwasaidia wanaingia mitini ila na sisi sometimes tunabanwa na tunasaidiwa

kukopa harusi kulipa ni matanga.......... mpo hapo ????
 
ni ushauri tuu....
1. usikopeshe mtu fedha ukiwa bado ujajitosheleza kifedha wewe mwenyewe, maana utapata chuki bure.
2. usikopeshe mtu pasipo makubaliano, maandishi au kuweka dhamana kitu.
3. usikopeshe ki holela hata kama ni ndugu yako wawepo mashaidi au shahidi mmoja tu.

japo yapo yale ya kuazima fedha kimazoea lakini nayo inabidi ujue tabia ya mkopaji pia na uwezo wake wa kulipa.
 
Nimekiona Cha Moto hata mie yamenikuta ila huwa nashindwa kujizuia kukopesha watu kwasababu hata mimi huwa nikibanwa nakopa na ninalipa sasa sidhani kama idea ya kuacha kabisa kukopesha watu ni nzuri cause sometimes mtu anakuwa na shida ya dhati na wewe unakuwa kwenye nafasi ya kumsaidia sasa sijui tufanyaje tukiwasaidia wanaingia mitini ila na sisi sometimes tunabanwa na tunasaidiwa

Kama umeamua kugawa gawa tu, hakuna kukopeshana sikuizi. Na kwa hao ndugu na rafiki wa karibu ndo kabsaaa kutafutiana uhasama tu.
Mi sikopeshi hata nikiwa nayo.
 
Hakuna kitu ambacho huwa kinanitia huruma kama ndugu yangu au rafiki akihangaika wakati ninao uwezo wa kumkopesha..!

Sasa na nilivyokuwa nina bahati mbaya, yaani wakinikopa hawarudishi kabisaaa..!

Huwa najiapiza kwamba sitawapa tena, lakini matatizo yakiwapata najikuta nawaonea huruma nawakopesha huku nikiwasema, lakini kulipwa silipwi..!

Saiv itanibidi nijifunze ukauzu tuu..!
 
Ila wakopaji wasiorudisha wanakera sana, huwa wanaona wao ndio wenye shida mkopeshaji hana shida na hiyo hela yake. Nina rafiki kaingia mtini mpaka urafiki umekufa kisa hela ndogo tu. Siku hizi nimejifunza kusema "sina" au kutoa kiasi kidogo cha "potelea mbali" ingawa unaoana kabisa mtu haamini kama huna
 
Hii Mada ni Darasa kwani ni janga la kitaifa. Kila Mtu lazima atAkuwa ashaonja hii Shubiri, na kama bado basi utarajie kukutana na hii shubiri.

Mambo ya Ndugu na Marafiki katika PESA hupoteza Uaminifu na hata kupelekea Undugu/Urafiki kufa kabisa.

Skiza kisa hiki changu kidogo na utajua kuwa Binadamu sio watu.
"Niliwahi kumkopesha rafiki yangu kiasi cha 1.5Ml aongezee ili akanunue Gari,akaniahidi kuwa kila Mwezi atakuwa anapunguza kiasi fulan cha pesa. Siku zikaenda huku akiomba nimpe Grace Period kwani aliingia Damage kubwa Mfukoni kununua Gari.Ikaenda hadi Miez saba kabla hajaanza kunilipa kiasi tulichokubaliana kila Mwezi.
Nlipoanza kufuatilitia, siku nyingingine anakupa 20,000 out of 250,000 mliyokubaliana.
Ikaenda hadi ikawa uhasama:kibaya zaidi akatunga Maneno ya uongo kuwa Mm ninamsema vibaya Boss wangu. Lakini kwa Vile Boss alikwisha Mtambua na Matatizo yake alokuwa nayo pale ofisin wala hakumsikiliza.
Mwishowe kabisa ilibakia 320,0000 akajifanya kula Kobisi kabisa tokea 2008 hadi Leo hii.

Kwa nanamna hii siku nyingine unaweza kukopesha kweli!????"

Kwa sasa akija Mtu ndugu mwenye shida ya kukopa nnamwelekeza aende Sakosi au kama ana Security Item basi najifanya kuwa rafiki anakopesha kwa Riba Ndogo na Lakini lazima uwe Na security Item.
Binadam tumepoteza Utu siku hizi.

Naomba mlete visa vya kutufunza ili tuepukane na Huu usumbufu.
Na kama huna uwezo wa Kulipaaaa,kwa nn ukakope Malaki kwa Mamilioni!!? Aliyenikopa hiyo 1.5Ml angekuwa na nia ya kulipa angeweza kunilipa kwa Miezi 3 kutokana na kiwango cha Mshahara wake.
 
Aisee huu uzi unanihusu kabisa, tena usiseme kukopa tu, hata kufanya nao dili / biashara ndugu au 'rafiki' nako ni kujipalia mkaa tu.
 
Back
Top Bottom