Usimjaribu bwana mungu wako!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Usimjaribu bwana mungu wako!!!

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BRO EDDY, Mar 28, 2011.

 1. BRO EDDY

  BRO EDDY Member

  #1
  Mar 28, 2011
  Joined: Dec 6, 2010
  Messages: 22
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 3
  Ya kaisari mpe Kaisari na ya MUNGU mpe MUNGU! Huwezi kumjaribu BWANA MUNGU wako! MUNGU alimtoa YESU auwawe kwa ajili yetu, MUNGU pia alileta gharika na kuteketeza kizazi chote na kumuacha NUHU na wanyama aliowateua, Mungu pia anasema kila roho itaonja mauti ili ifike kwake.

  Haina maana kuwa ukinywa kikombe cha Babu hautakufa na kuwa utaishi milele! Babu haombei bali anakupa dawa unywe hivyo tusimbeze umati wote huu unaoenda kwake, unaonesha wazi yote ni ya kweli kama ni uongo ungejulikana mapema na watu wangesitisha!

  Kumbuka huwezi kumjaribu BWANA MUNGU wako na hatujui siku wala saa!!
   
 2. zaratustra

  zaratustra JF-Expert Member

  #2
  Mar 28, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 851
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  Katika UTOAJI TU (kumtolea sadaka na shukrani), tumeruhusiwa KUMJARIBU! Soma Malaki 3:8-10
   
 3. 4

  4 PRINCE Senior Member

  #3
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 27, 2011
  Messages: 144
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ni kweli,mimi nadhani badala ya kumbeza babu wa Loliondo na tiba yake,ni bora mtu akanyamaza kimya kama haamini.si vizuri kubeza jambo ambalo huna uhakika wa ukweli wake.yaani hujui kama ni kweli ama si kweli halafu unabeza.hata ukijua kuwa ni uongo,ni vema kutoa ushauri kwa watu kwa lengo la kuwasaidia.tukumbuke wengi wanaokwenda kwa babu ni wale wenye matatizo kiafya,na hiyo ni ktk kuhangaika ili kupata afya.unapokuwa na shida kubwa huwa unasikiliza kila ushauri na kutamani kuufanyia kazi ili upate msaada.TUSIWABEZE WANAOKWENDA KWA BABU,TUSIMBEZE BABU NA TIBA YAKE.BALI TUSAIDIANE KUSHAURIANA.
   
 4. Stevemike

  Stevemike Senior Member

  #4
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Hapa sio mahala pa andiko hili mzee. Soma mt.4:1 na kuendelea uone mazingira ya matumizi ya andiko hili.
   
Loading...