Usimdharau Baba yako

Usimdharau Baba yako

Robert Heriel Mtibeli

Platinum Member
Joined
Mar 24, 2018
Posts
40,299
Reaction score
93,336
USIMDHARAU BABA YAKO.

Kwa mkono wa, Robert Heriel

Angalizo: Makala hii inaweza isimfae kila mtu kutokana na Lugha iliyotumika inaweza kuwa kali kwa baadhi ya watu. Ikiwa wewe ni mmoja wa watu ambao haujazoea lugha kali za kukemea basi nakusihi ishia hapa hapa, na kama utaendelea basi ni wazi utakuwa umekaidi na umejijua unauwezo wa kuhimili.

Usipojifunza kuupenda ukweli basi utakuwa mtumwa wa uongo. Ukweli siku zote ndio humweka mtu huru. Na pasipo ukweli hakuna uhuru, na kama mtu anajiona huru pasipo ukweli yu ajidanganya.

Huwezi mdharau Baba na Mama yako ukabaki salama dunia ingalipo. Na hapa nazungumzia Wababa na wamama wanaoshika sheria za Mungu. Hao ndio Baba na hao ndio Mama. Ikiwa Baba au Mama hashiki sheria za Mungu anakosa kibali cha kuwa Baba yako au Mama yako.

Huwezi ukafanya upumbavu na uhuni alafu ukajiita Mama au Baba yangu. Hata maandiko yaliposema; Waheshimu Baba na mama yako ili siku zako zipate kuwa nyingi.

Haikuzungumzia Baba mpumbavu au Mama mpumbavu. Bali ilizungumzia Mzazi anayeshika amri za Mungu. Lazima watu waelewe kuwa binadamu na mnyama wanatofautiana sehemu ndogo tuu, nayo ni akili na maarifa tena ya kumcha Mungu.

Mzazi asiyemcha Mungu akajiita Baba au Mama hana tofauti na Mbuzi kwa mwanaye. Mtoto hawezi kumheshimu mzazi asiyemheshimu Mungu kisa na mkasa alimzaa. Mtoto hawezi kumheshimu mzazi anayemfundisha uhalifu na uovu kwa Mungu aliyeumba mbingu na nchi.

Wewe na Mimi ni Baba lakini haimaanishi sisi ni Mungu. Kusema mzazi ni Mungu wa pili ni kujitoa akili na dalili ya wendawazimu. Kumbuka hata mimi pia ni mzazi na zamani nalikuwa mtoto hivyo kila nikisemacho kinaweza kunihusu mimi mwenyewe au yeyote bila kujali nafasi yake.

Mzazi ni mzazi na anapaswa kupewa heshima yake, lakini ni heshima ipi hiyo na kwa mazingira yapi? Heshima ya Mzazi inazingatia zaidi sheria za Mungu, mzazi anayemcha Mungu kwa kufuata amri na sheria zake huyo ndiye analengwa zaidi. Tofauti na hapo ni upuuzi tuu.

Heshima ya mtu haitokani na sababu ya kukuzaa au kutokukuzaa, haitokani na kuwa na cheo au kutokuwa nacho, haitokani na umri au utajiri wa mtu. Heshima ya mtu ni kutenda matendo mema yampendezayo Mungu.

Kuna Wazazi hasa kina Mama wanajifanya vichaa wakitishia watoto wao, sijui nilikubeba miezi tisa, nakuambia hata ungebeba miaka mia moja hiyo mimba, mtoto hajaambiwa hakuheshimu kwa sababu ulibeba mimba au ulizaa kwa uchungu, bali atakuheshimu kwa sababu ya kumcha Mungu. Hivyo acheni kutishia kwa upuuzi wenu. Kisa miezi tisa ndio muamrishe watoto mambo ya hovyo, hata ungebeba miaka mia moja. Kama humchi Mungu hustahili kuheshimiwa huo ndio ukweli, utake usitake.

Mzazi mwema huwa na tabia njema, humfundisha mtoto tabia njema huku yeye akiwa mfano bora kwa mwanaye. Ukifanya hivi sio mtoto tuu atakayekuheshimu bali hata aliyekuumba atakuheshimu. Lakini sio usingizie kuzaa sijui mimba miezi tisa, Tembo anayebeba miezi kumi na tano hasemi, wewe kujitia ujinga tuu.

Nasisitiza; Baba au Mama ili upewe haki yako ya kuheshimiwa basi lazima nawe uwajibike kumcha Mungu. Hakuna haki pasipo wajibu. Wajibu wa mtoto ni kumheshimu mzazi mcha Mungu ili huyo Mungu ampe maisha marefu yenye Baraka. Hivyo ni haki ya mtoto anayeheshimu wazazi kuishi miaka mingi.

Hata Yesu alipoambiwa Mama na ndugu zako wanamuita, angalie Yesu alichojibu hapo chini, nanukuu;

Mathayo 12:
46 Alipokuwa katika kusema na makutano, tazama, mama yake na ndugu zake walikuwa wakisimama nje, wataka kusema naye. 47Mtu mmoja akamwambia, Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kusema nawe. 48Akajibu, akamwambia yule aliyempasha habari, Mama yangu ni nani? Na ndugu zangu ni akina nani? 49Akawanyoshea mkono wanafunzi wake, akasema, Tazama, Mama yangu na ndugu zangu! 50Kwa maana ye yote atakayeyafanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni, huyu ndiye ndugu yangu, na umbu langu, na mama yangu.

Nafikiri ujumbe huu tumeupata wote sisi wazazi kuwa ili uwe Mama au Baba kwa watoto wetu basi lazima tufuate mapenzi ya Mungu Baba aliyembinguni. Hakuna tunachomiliki hapa duniani, sio mtoto sio mali sio hata huo mwili wako. Lazima hilo tulijue. Sio kutishia watu hapa na upumbavu wako; Mimi Baba yako, mimi Mama yako.

Vijana wa siku hizi nasi tumezidi kuwa wapumbavu na kuzua tafrani kwa kuwadharau wazazi wetu. Hata kama Baadhi ya wazazi wetu ni vichomi lakini lazima tutende kwa hekima na busara.

Maandiko yanasema;
Kumbukumbu la torati 27;
16 Na alaaniwe amdharauye baba yake au mama yake. Na watu wote waseme, Amina.
Inaendelea
Isaya 45;
10. Ole wake amwambiaye baba yake, Wazaa nini? Au mwanamke, Una utungu wa nini?

Kuna baadhi ya vijana tumekuwa na tabia isiyo ya kiungwana, ukishapa elimu kidogo sijui ni shahada sijui ni uzamili au uzamivu unaanza kuleta dharau kwa Baba yako au Mama yako. Jambo hili sio nzuri kwani linaenda kinyume na sheria za Mungu.

Kuna baadhi ya vijana tumekuwa na upuuzi wa kudharau wazazi wetu tukishapata pesa na utajiri kidogo ambao kimsingi ni upuuzi tuu. Unasahau wazazi wako hata kuwahudumia na kuwajali. Mzazi akiongea nawe unaongea hata kama anaongea jambo zuri la kukufanikisha, unajifanya unajua zaidi kuliko Mama au Baba yako huo ni uzwazwa.

Mzazi usimsikilize kama anamambo ya hovyo na upumbavu. Mathalani; Mzazi anayekushauri uovu huyo usimsikilize, kuna wazazi wengine wanakushauri uende kwa waganga wa kishetani hawa usiwasikilize tena onyesha msimamo mkali mpaka waogope. Wakikuambia walikubeba miezi tisa waambie hata mngenibeba miaka elfu nisingewasikiliza upuuzi wenu. Usiogope tena sema kwa kinywa kipana chenye pumzi ya Mungu. Hawana uwezo wa kukufanya kitu zaidi ya kutapa tapa na maneno yao ya kizamani.

Usimdharau Baba yako hata kama alikufanyia jambo baya, Baba kama alishindwa kukufundisha uchaji wa Mungu na tabia njema, akakukimbia wewe na Mama yako. Basi wewe geuka mwalimu wake, mfundishe wewe uchaji wa Mungu na tabia njema. Usimlipe Mabaya Baba yako hata kama alikutenda mabaya, labda atake mwenyewe, kwa sababu kuna wababa mashetani ambao licha ya kukutenda uovu bado anataka kukuangamiza, basi usimpe nafasi sana nawe utende kwa akili atakayokupa Mungu wako.

Baba yako akizaa hata watoto mia moja usimuulize unazaa nini ikiwa anazaa kwa utaratibu yaani havunji sheria za Mungu. Yaani kama anazaa na wake aliowaoa mwambie hata azae watoto elfu ni yeye tu. Lakini sio Baba anazaa kama mnyama kila mwanamke anamzalisha bila kufuata utaratibu huko ni kufanya zinaa. Usikae kimya kumuonya Baba yako ikiwa atatenda makosa, kama wewe huna hekima ya kumuonya basi tafuta wenye hekima wakamuonye.

Nihitimishe kwa kusema; Tupendane, tushike sheria za Mungu kwani hizo ndizo zitatufanya tuwe na kizazi chenye maadili.
Nisisitize; Mzazi hauheshimiwi au siheshimiwi kisa nilizaa au kubeba mimba miezi tisa, bali tunaheshimiwa kwa sababu ya kufanya mapenzi ya Mungu.
Barikiweni

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam
 
Siyo baba yako tu ni wazazi wako wote wawili.

AMRI YA NNE(Kutoka 20:12)
Waheshimu baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
 
Lakini pia vijana muwe na shukrani
Kwa sasa kuoa mke asie na mtoto ni bahati, mwanamke unaamua kwenda kuishi na mume ukiwa na watoto ambao hajawazaa huyo mume watoto wanakuwa wanaambiwa huyu sio baba yenu ni kweli sio baba yao.
Ila kawahudumia toka udogoni hadi ukubwani huku aliekuzaa hajulikani alipo wala hajawahi kukuhudumia kwa cho chote wala humjui kabisa.
Cha ajabu ukubwani unaujua ukweli unashindwa kulipa fadhila kwa alieyekuhumia udogoni kisa mama
 
Kweli Kabisa
 
Back
Top Bottom